DAS Singida ataka waandishi wa Habari wapeleke CV zao ofisini kwake

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Ali Mwendo amewataka waandishi wa habari Singida wawasilishe CV zao kwake, Mwenyekiti wa Singida Press Club akamjibu sio sahihi kwani wao sio waajiriwa wa Serikali.

Jambo hili ni geni sana itapendeza Waziri wetu Nape aingilie kati
 
Bukoba wametakiwa kujisajili! Nchi ngumu sana hii, hapa wanapima upepo wiki ijayo utasikia imekuwa hoja ya kitaifa-wote kutuma cv au kusajiliwa kwa mkuu wa wilaya au DAS
 
Ali Mwendo amewataka waandishi wa habari Singida wawasilishe CV zao kwake, Mwenyekiti wa Singida Press Club akamjibu sio sahihi kwani wao sio waajiriwa wa Serikali.

Jambo hili ni geni sana itapendeza Waziri wetu Nape aingilie kati
Kwani wakipeleka CV zao kwa DAS watapungukiwa nini? Na wakigoma kupeleka wanaficha nini? Je, kama DAS au Serikali ina lengo zuri kwao? Iweje kila kitu watu wanakuwa negative tu? Maswali ni mengi.
 
Pamoja na kwamba hao viongozi inawezekana wamekosea ila miaka ya karibuni Kuna ujinga mwingi sana kwenye tasnia ya habari.......Hizi FM radio stations Zina waandishi wengi sana wasiojielewa na huwa hawajui nini Cha kuongea hewani
 
Hao waandishi wengi ni zero brain wacha wanyooshwe waombwe hadi tarehe zao za bleed.
Wakati wa uchaguzi wanakuwa machawa wa watu fulani.
 
Kwani wakipeleka CV zao kwa DAS watapungukiwa nini? Na wakigoma kupeleka wanaficha nini? Je, kama DAS au Serikali ina lengo zuri kwao? Iweje kila kitu watu wanakuwa negative tu? Maswali ni mengi.
Kweli, Maswali ni Mengi...
 
Ali Mwendo amewataka waandishi wa habari Singida wawasilishe CV zao kwake, Mwenyekiti wa Singida Press Club akamjibu sio sahihi kwani wao sio waajiriwa wa Serikali.

Jambo hili ni geni sana itapendeza Waziri wetu Nape aingilie kati
Wapeleke CV ofisini kwake kwani anataka kuwaajiri?
 
Kwani wakipeleka CV zao kwa DAS watapungukiwa nini? Na wakigoma kupeleka wanaficha nini? Je, kama DAS au Serikali ina lengo zuri kwao? Iweje kila kitu watu wanakuwa negative tu? Maswali ni mengi.
Serikali kudai CV za waandishi wa habari ni mwanzo wa serikali kuingilia uhuru wa habari.

Kwani huyo DAS anazitakia nini CV za waandishi wa habari?

Governmental overcollection of informationnis a problem.

Inatakiwa kabla taarifa yoyote haijakusanywa, kuwe na maelezo ya kwa nini inakusanywa, kuwe na sababu ya kuhalalisha kukusanya, kuwe na maelezo ya jinsi taarifa zitakavyotunzwa na muda taarifa zitatunzwa kabla ya kufutwa, na jinsi zitakavyofutwa.

RAS katoa maelezo haya yote.
 
Mimi nadhani uyo RC angejenga hoja kabla ya agizo apo tungeanza kujadili hoja sio agizo.Hana mamlaka ya kufanya ivyo.
 
Wapeleke CV ofisini kwake kwani anataka kuwaajiri?
Acha utoto wa kitoto. Hujui kuwa kuna waandishi wengine hawana expore kabisa na mambo yanayoendelea nchini, sembuse Kimataifa?

Uelewa wa wengi wao ni hafifu mno, mpaka mtu unashangaa amekuwaje mtangazaji/mwandishi wa habari.

Wanaogopa nini kupeleka? Walishaambiwa ikifika muda fulani bado hawajakuwa na qualification zilizowekwa na Serikali, waanze kujitafakari.

Kuna baadhi yao wanawaharibia waandishi/watangazaji wazuri wenye uelewa.

DAS yupo sahihi kukazia maelekezo.
 
Serikali kudai CV za waandishi wa habari ni mwanzo wa serikali kuingilia uhuru wa habari.

Kwani huyo DAS anazitakia nini CV za waandishi wa habari?

Governmental overcollection of informationnis a problem.

Inatakiwa kabla taarifa yoyote haijakusanywa, kuwe na maelezo ya kwa nini inakusanywa, kuwe na sababu ya kuhalalisha kukusanya, kuwe na maelezo ya jinsi taarifa zitakavyotunzwa na muda taarifa zitatunzwa kabla ya kufutwa, na jinsi zitakavyofutwa.

RAS katoa maelezo haya yote.
Tii sheria bila shuruti bwasheee.
 
Wapeleke CV sababu wanatoa taarifa kwa ajil.ya public consumption ,kuhoji kuwa sio waajiliwa wa serikali ni ujinga ni sawaa atokee Dr awe anatibu watu tu kwamba yuko huru kwa kuwa sio mwajiliwa wa serikal

Na ifahamike tu habar zinazotolewa na wanahabar zinaaminika sanaa

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Ali Mwendo amewataka waandishi wa habari Singida wawasilishe CV zao kwake, Mwenyekiti wa Singida Press Club akamjibu sio sahihi kwani wao sio waajiriwa wa Serikali.

Jambo hili ni geni sana itapendeza Waziri wetu Nape aingilie kati
Hakika.
CV za mtumishi asiye wake zinamhusu nini? Halafu hata kama mwandishi wa habari ni wa serikali, DAS sio mwajiri wake. Huku ndio kule kule kujimwambafy kama enzi zile. Saikolojikali, hajakubali huyu kama enzi zimebadilika!
 
Wakipitisha paranja kwenye radio hapo watawamaliza maana huko wameja makanjanja

Ova
 
Kwani wakipeleka CV zao kwa DAS watapungukiwa nini? Na wakigoma kupeleka wanaficha nini? Je, kama DAS au Serikali ina lengo zuri kwao? Iweje kila kitu watu wanakuwa negative tu? Maswali ni mengi.
Aeleze kwanza anazitaka za nini?Bila hivyo anazusha maswali mengi kwa waandishi na jamii kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom