Mada ilimhusu DAS, sio RAS. Huelewi tofauti yao, acha kukariri mambo.
Tofauti yao ni;
DAS ## Katibu Tawala Wilaya.
RAS ## Katibu Tawala Mkoa.
Kwa hiyo umekiri na unajua kuwa kuna sheria inayompa kiongozi fulani (sio DAS) mamlaka ya kuangalia CV za waandishi waliopo ndani ya Wilaya au Mikoa.
Ungekuwa unajua maana ya maneno deligate, accountabilty na responsibilty katika medani za utawala, usingejibu ki-leimani hivi pamoja na kuwa mbishi kama watu wa mwambao wa Ziwa Tanganyika.
Kwa hiyo, agizo hilo la DAS (baada ya kuwa deligated) wa Singida ni sahihi kwa kuwa anakazia hili;
Kiwango cha Elimu kwa Waandishi wa Habari ni Diploma, Sheria iliyosainiwa na Rais Novemba 16, 2016 ambapo siku mbili baadaye ilichapishwa kwenye gazeti la serikali baada ya muswada wake kupitishwa na Mkutano wa 5 wa bunge mwezi Novemba 2016.