Data: Bei za mafuta DRC, Burundi, Rwanda, Zambia ziko chini

Sidhani kama una uelewa wowote wa kile umeandika hapa.

Unavyolinganisha bei ya bidhaa kati ya nchi na nchi tumia International currency, hapo tunatumia USD kupima bei halisi.

Kwako wewe, 5,000 Ya Kenya ni nafuu kuliko 50,000 ya TANZANIA kisa namba ya Kenya kuonekana ndogo??

Hao Zambia bei yake ni USD 1.555 Kwa Petrol na TANZANIA ni 1.354 kwa petrol.
Haya tuambie wapi kuna bei kubwa??
 
Mnaenda kote huko kufanya nini? Zanzibar hali iko hivi

View attachment 2214979
Aisee..

This is very interesting..

✓ Labda Zanzibar Wanachimba mafuta...!

✓ Labda Zanzibar hawakuwahi kukumbwa na athari za COVID 19...!

✓ Labda Zanzibar wako sayari ya Mars ambako Russia Ukraine war haipiganwi...!

Yaani huu ni ushahidi rahisi sana wa kuwaumbua viongozi wa serikali ya Rais Samia na CCM. Sijui wanasemaje kwa hili..?

CARDLESS tusaidie tafadhali. Achana na Zambia, DRC au Kenya au Rwanda au BURUNDI ama kokote. Ni humu humu nchini Zanzibar...!
 

Hapa Zanzibar vipi mheshimiwa?
 
Zanzibar ni Nchi kama nchi zingine, wao kama serikali yao SMZ wamechagua kuwa hawatokuwa na tozo mbalimbali kwenya mafuta. Na hata bajeti yao imeakisi huo utaratibu. ZANZIBAR wao uchumi wao unategemea zaidi utalii, na exportation ya karafuu.

Zanzibar mafuta bei nafuu zaidi kwa kuamua kuwa wao hawatotoza kodi katika mafuta.
Sasa impact yake ni nini.
1. Mapato yao ni madogo kiasi kwamba hata bajeti yao huwa ni ndogo hali inayopelekea mzunguko wa pesa kuwa mdogo, mishahara midogo zaidi.

2. Zanzibar kuwa na miundombinu hafifu zaidi katika nchi hizi mbili, Barabara sehemu nyingine hakuna hasa PEMBA.

3. Kutokana na mazingira yao ya kisiwa kuna magari machache sana hivyo kuimpose kodi kwenye mafuta isingewaletea afavantage as most of their cars ni za SMZ.

UPANDE WA TANZANIA BARA, ni tofauti kabisa na kule Zenji.
1. Kuna vyombo vingi vya usafiri hivyo kuweka kodi kwenye mafuta ni uhakika wa kukusanya kodi na tozo mbalimbali katika kusaidia mahitaji muhimu ya nchi yetu hasa miundombinu nk.

2. Bajeti yetu inategemea chanzo cha mafuta kwa kiwango kikubwa kutokana na uhakika wake, hivyo bei itakuwa juu tu.

Kama utapata muda wa kufanya hesabu jaribu kuangalia ongezeko la asilimia ya bei za mafuta kati ya Zanzibar na Bara ndio utaona hiki nikisemacho kuwa effect ya URUSI vs UKRAINE, umbali nk vinachangia bei kuwa juu.

Unaweza ona TZ bara bei ni 3160 na Zanzibar ni 2670 lkn kiasilimia Zanzibar ikwa bei yake imepanda kwa asilimia kubwa kuliko Tanzania Bara.
 
CARDLESS wewe ndiyo hujanielewa...

Iweje uchukue bei ya Kenya au Zambia au kokote in $ uzidishe na TZS..?

Kwani Wakenya, Wazambia, na kwingine huko wanalipia mafuta hayo kwa Shilingi ya Tanzania au kwa pesa za nchi zao..?

Je, thamani ya pesa zao kwa $ unaijua..?

Mimi sijakuekewa pia. Hebu nieleweshe tena labda nitakuletea..
 
Kuna bidhaa bei yake iko determined na USD mzee, bei ya bidhaa hatuzipimi hivyo unavyofikiria wewe.

Ili kupata bei halisi badilisha hizo fedha za madafu kwenda kwenye USD ndipo utaona bei halisi ni zipi.

Ushawahi ona gari inauzwa kwa KWACHA/SHILINGI/MITIKASHI au RAND kule Japani?

Tambua kuwa duniani medium of exchange ni fedha na fedha ambazo ziko katika line ya kutambulika kimataifa au base ya bidhaa zote basi ni USD, POUND, EURO na YEN. Hivyo bidhaa yoyote ili kujua thamani halisi kati ya nchi na nchi basi lazima uiweke kwenye pesa hizo ambapo utaona uwiano unaoeleweka.
Mfano. Zambia mafuta ni USD 1.555 na TZ ni USD 1.354.
Ukiangalia hapo utaona kuwa kumbe TZ mafuta ni rahisi ni kuliko Zambia, lkn ukitumia pesa za Nchi husika utaona kama mtu wa Zambia amechukua kiasi kidogo cha pesa kulipia kumbe ni kikubwa mno kwa kwao.

Mfano mwingine mishahara ya wafanyakazi wengi Afrika Kusini ni RAND 10000 hadi 20000 kwa mwezi, lkn huku TZ ni Shilingi Mil 1 hadi mil 6. Sasa ili kupata uhalisia wa kiwango hiko unabadilisha kwenda kwenye dola, yaan wote tungekuwa tunatumia USD je yupi angetumia Dola chache katika kulipia huduma hiyo.
 
Ukweli ni kwamba Tanzania inaongoza kwa Utitiri wa Kodi kuliko nchi zote za East Africa...!

Hatukatai tulipe Kodi...!

Nchi kama Kenya Serikali ya Uhuru imekubari kutoa Ruzuku kwenye Mafuta ili Mabadiriko haya ya Bei ya Mafuta yasimuumize mwananchi moja kwa moja!!!

Kwani Serikali ya Tanzania hii Nchi imekopeshwa na nani mpaka inashindwa kufanya Maamuzi muhimu kama haya ( Kwa kipindi tu mpaka Bei ya mafuta ikikaa sawa) kwa ajiri ya Mwananchi wa Kawaida...!?
 
Congo DRC,Rwanda,Burundi na Uganda sehemu kubwa ya shehena za nafuta yao yanapitia kwetu
Uongo mkubwa sana, tena saaaana, nenda katafiti au kasome vizuri utajionea, hapa ni UGANDA ndio hitumia sana Bandari hii kupitisha mafuta. Ila Rwanda na Burundi hutumia zaidi Mombasa, na DRC wana bandari yao ingawa iko mbali, hivyo bidhaa nyingi za Kinshansa hutumia bandari ya upande wa Bahari ya Atlantiki.
 
Kenya uchumi wake unatuzidi sisi karibu mara mbili yake, hivyo wao wana stock kubwa ya fedha za kigeni nk. Kwa wao wanaweza kubalance sisi nchi yetu ina uchumi mdogo zaidi. Hata bajeti yetu imezidiwa karibu mara 2 na ile ya Kenya.
Mbona hulinganishi na UGANDA ambao tumewazidi kila kitu.
 

Looh, ndiyo sababu hizi mnazoweza kutuambia wananchi? Magari machache? Barabara mbovu Pemba na blaah blaah zingine.!!??? Really?
Ndugu CARDLESS bado hueleweki. Sina shaka yoyote kubwa unatetea hali kwa mtazamo wa kisiasa. Na ndivyo wanavyofanya viongozi wa serikali hii..!

Hebu rudia tena kusoma sababu za huko Zanzibar unazozitoa mwenyewe. Ni siasa tupu!!..

Hebu fikiri juu ya sababu hii uliyotoa kwa huko Zanzibar vs Tanganyika..

✓ Uchache wa magari Zanzibar..

✓ Uwingi wa Magari Tanganyika..

Katika akili ya kawaida, mtu aweza kujiuliza, ni wapi ambako wananchi wangepigwa kodi kubwa zaidi ili serikali kupata pesa ya kujiendesha..?

Jibu, ni kule kwenye magari machache..!

Vipi nchi zingine kuliko na bei nafuu Zambia, Kenya, Mozambique, Rwanda nk, kuna magari machache siyo..???
 
Point ni kwamba why hzo ni land locked countries lkn kwao mafuta yapo chini,huoni kuna tatizo mahali hapo?

Halafu uache kuita waongo usiowajua,mimi naishi along high way ya kwenda mikoani kabisa,kila siku nayaona malori ya mafuta nchi hizo mamia kwa mamia yakiwa yamebeba mafuta kuelekea huko,utasemaje nadanganya?

Tuache mahaba tuongee ukweli,utitiri wa matozo kwenye mafuta umezidi sana nchi hii na ndio unaopelekea mlaji wa mwisho kuathirika.
 

Watu wanapiga dili mkuu…msikilize Shabiby hapa…watu wanalamba asali

 
Kuishi barabarani ndio kitu gani wewe PIMBI?? Mimi nakuelekeza kitu halisi wewe unaanza unaishi karibu na barabara we vipi.?

Rwanda na Burundi hutumia kiasi kidogo mno cha mizigo yao kupitisha bandari ya Dar, mizigo mingi hupitia bandari ya Mombasa kama ulikuwa hujui ndio ufahamu leo hii. Rwanda na Burundi pia bidhaa nyingi hutoka DRC sio kama unavyodhania ww kuwa bandari yetu ni hub kwa hapa East Africa. Mombasa Port ndio bandari kubwa kwa ukanda wetu, kuanzia teknolojia na ufanisi.

Wapi ambapo umeona magari ya Burundi ya Mafuta mamia kwa mamia yanapeleka mafuta huko Burundi? Watu tunadrive na hatukutani na uwingi huo zaidi ya gari 10 hadi 20 na tena sio kila siku inatokeaga tu.

Usifananishe magari ya kupeleka ngano za Azam ukasema mafuta.

Rwanda, Burundi, DRC majibu yametolewa pitia posts za juu.

Malawi, Zimbabwe, Zambia, Uganda hao wanabei kubwa sana kuliko sisi.
 
Watu wanapiga dili mkuu…msikilize Shabiby hapa…watu wanalamba asali

Mpaka naingia kaburini, nitakufa nikiwa naamini maisha haya ni watanzania wenyewe tunayataka.

Ni kama kuwa na mwanamke anaeonesha dalili zote hakutaki ila we bado umeganda tu kama zezeta(limbwata)
 
Unajua maana ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima? Mshahara ni matumizi yasiyo ya lazima? Unajua unachoongea Boss au unaleta ubishi wa mshipa?
 
Mkuu hongera kwa kuonyesha hii kitu...yaani hizo cost...zote mwananch ndy anapambana nazo...kodi nyingi hapo hazna miguu wala nini. Mwanasiasa akikuwambia anakuhurumia nawee ukakubali ujue umelala ubongo mpaka aibu..wale wa bunge mule hakuna hata moja mwenye kugusa hili.hayo makodi wakiyafuta 50%kila kipengele..mafuta bei itarudi 2300...Wanakimbilia eti wKakope ili wananchi mzgo ukawaelemee tena kulila madeni na riba juu. Yani thinking capability imekimbilia kukopa tu...Hii nchi hii!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…