Hii sio dharula mzee, hata USA bei iko juu, hii ishu ya bei iko Dunia nzima kutokana na uhaba wa bidhaa yenyewe. Bei ya mafuta ni kitu kinachopanda na kushuka, huwezi toa kodi eti kisa mafuta yamepanda, kodi itaendelea kukusanywa vile vile.
Mtakubali kupunguzwa mishahara au kupunguzwa dawa na vifaa tiba hospitalini pia??
Tunapaswa kutoa elimu juu ya namna uchumi unaenda, hili si suala la CCM au CHADEMA au ACT ni national matters, hivyo lazima tuelewe chanzo chake na effect yake. Ni suala la muda tu kila kitu kitarudi kwenye hali yale ya kawaida.
Tusiwe watu wa kulalamika sana, Price ya mafuta sio kwamba ifanane kwa nchi zote, hata hapa Afrika mashariki, bei ya mchele iko tofauti baina yetu, ni kutokana na uwekezaji nk.
Kwa mfano Kenya wao hutumia kiasi kikubwa mno cha mafuta ukilinganisha na sisi hivyo lazima watapata punguzo la bei as we know kadiri unavyonunua mzigo mkubwa ndipo disccount hupatikana.