Dah jamani hii vita ya ukraine imetukalia vibaya sisi tu au hawa jirani zetu wao wanachimba mafuta? si wanapitisha mafuta hapahapa bandarini kwetu jamani?
Tunaongelea vita lakini hawa jamaa wa Drc congo wana vita na waasi miaka 25 sasa , tunahitaji maombi maalumu nchii hii hali tete sana
View attachment 2214602
View attachment 2214603
Kwanini Shilingi [TZS] thamani yake iko chini kuliko za hawa jirani zetu?
1. ZAMBIA KWACHA: 1KW = 131 TZS..
2. BURUNDI BIF: 1BIF = 1.35TZS..
3. RWANDA FRANC: 1RF = 2.28TZS..
4. DRC CDF: 1CDF = 1.16TZS
5. KENYA SHILING: 1KSH = 20TZS..
.......
We kwa akili yako unadhani kila anayeagiza mafuta anachukulia URUSI?? DRC mafuta yao mengi hutoka ANGOLA na NIGERIA kutokana na wako upande mmoja wa bahari ya ATLANTIC, sasa wewe TZ unawezaje kununua mafuta huko??
Lingine nchi zinazopitisha mafuta kutoka bandari ya TZ mafuta yako juu kama nchi zilizo LAND LOCKED kama ZAMBIA, MALAWI.
Kwenya masuala ya uchumi na biashara lazima utumie akili, sio umetoka huko na degree ya ufugaji nyuki unajikuta ww unajua namna gani uchumi unaendeshwa.
Kenye unaona mafuta bei ya chini kwa kuwa ni karibu, hivyo kila unavyosogea ndio gharama huwa kubwa zaidi. Kwa mfano ukitoka Dar nauli ya Moro ni ndogo kuliko IRINGA.
Huwezi pia kuondoa tozo na kodi kwenye mafuta maana tumeiingiza kwenye bajeti kuu ya serikali.
Lawama na kujiona unaweza kuleta mada haikusaidii
Wewe
CARDLESS unaelewa sababu za bei ya mafuta dieseli & petrol zinazotolewa na viongozi wako wa serikali ya Tanzania..?
Labda hujui au hukumbi. Acha tukukumbushe. Wanatoa sababu kuu tatu;
1. Athari za COVID 19..!!
2. Russia - Ukraine war..!!
3. Hatuchimbi mafuta..!!
##Hakuna sababu ya umbali!
Maswali kwako;
##Je, unadhani hizi nchi ambazo bei za nishati hii iko chini kuliko sisi;
✓ Ziko sayari nyingine ambako hakuna vita ya Russia & Ukraine?
✓ Hawajakumbwa na athari za COVID 19?
✓ Wanachimba mafuta yao..?
##Hizo nchi zinatumia mikakati gani kudhibiti upandaji nishati huu?
## Jibu ni rahisi mno. Rais Samia na serikali yake hawana maarifa wala mkakati ku-stabilize price ili kunusuru wananchi wao..
They will soon pay huge price for their sloppy conduct, neglegency and selfish behavior...!!