Daudi Ballali's Death

Status
Not open for further replies.
Huu ni uwongo 110%. balali si mtu mdogo namna hii, kama angekutwa na mauti ofisi ya balozi wa tanzania nchini America wangejua na wangetoa taarifa kwani hakuna sababu ya kuficha kifo.
 
Bandugu,

Ballali ameaga dunia. I have confirmed this and I have to keep you guys informed.

More news to follow

Jee kuna kauwezekano kuwa kashughulikiwa asimwage mtama? au ndio "natural causes" ?
 
Hata TBC1 (RTD), RFA na Radio One "wameikwepa" habari hii mchana huu!

Dah, wengi 'wanaikwepa' na wengine wanauliza 'kwanini mmeiweka'?

Lakini Tanzania Daima hawakufanya ajizi, pamoja na kuwa wakati issue hii inatoka walishachapisha gazeti la leo iliwabidi kutoa "Toleo maalum" kuhakikisha hawakai na habari hii.



 
Invisible tupe updates zozote kama unazo kuhusu Ballali.
Mida hii si mizuri kwa alio Marekani kwani hawajakaa mkao wa kupigiwa simu na kuhojiwa.

Naomba muda kidogo... I will make sure nakuja na kauli inayoeleweka. Nina maswali 4 nimeyaandaa kuwauliza.

  1. Ballali kafa Ijumaa kweli au kafa kabla ya hapo?
  2. Kwanini azikwe Marekani? Ni sehemu ya wosia wake?
  3. Inasemekana kabla ya kukata roho alimtaja aliyemlisha 'sumu', tunaweza kupatiwa jina la mtu huyo?
  4. La nne ni siri yangu 🙂
 

bado hanisababishi kuona kwamba hii habari yote haikupandikizwa, tena na serikali ilitusimdai balali kuja kutoa ushahidi

hata kama source ni familia, bado wanaweza kuwa wametishiwa, au labda balali alitekwa nao na sasa wamewapelekea tuu taarifa nduguze
 

Invisible na Mkjj mmekuwa mnatoa taarifa indirectly. Najua tayari unayo majibu ya maswali yako hapo juu so mwageni mchele hapa, maaana sioni sababu ya kuzunguuuuka wakati ukweli tayari mnaufahamu
 
Huu ni uwongo 110%. balali si mtu mdogo namna hii, kama angekutwa na mauti ofisi ya balozi wa tanzania nchini America wangejua na wangetoa taarifa kwani hakuna sababu ya kuficha kifo.

Kama kweli ndo hivyo mbona hiyo ofisi haijui alikokuwa anatibiwa na alipokuwa anaishi????
 
Yaani hadi sasa serikali haijasema lolote.....??

Haiwezi kusema lolote maana haina majibu ya maswali mengi yatakayofuatia baada ya kutoa taarifa yake. Lakini pili watasema wao sio wasemaji wa familia yake so sio kazi yao kutoa taarifa
 
good work invisible lete hizo nyeti baba still waiting, but to me is not sounding good balali kuzikwa US.

Nahisi utapata majibu muafaka.
 
Invisible na Mkjj mmekuwa mnatoa taarifa indirectly. Najua tayari unayo majibu ya maswali yako hapo juu so mwageni mchele hapa, maaana sioni sababu ya kuzunguuuuka wakati ukweli tayari mnaufahamu

Slogan ya WE DARE O TALK OPENLY imetolewa ndo mana jamaa wanasuasua, mi nlishasisitizwa irudishwe jamani
 
Balali ni nani mbona kifo chake kimekuwa siri sana!mbona hayati Rutihinda kifo chake hakikuwa siri na alikuwa Gavana pia?ila serikali ilisema haimtambui balali maana si mfanyakazi wao tena!Balali itakuwa umekufa na siri nzito!

Kama serikali ilisema Balali sio mfanyakazi wa Serikali tena, na walisema hawawezi kuzungumzia kuhusu ugonjwa wake vivyo hivyo watasema kuhusu kifo chake, kwamba wao sio wasemaji wa familia yake ama hawajapata vielelezo kutoka serikali ua Marekani kuthibitisha kifo chake.
 
Nanukuu kutoka Tanzania Daima:
"Ndugu mmoja wa Ballali alipoulizwa na Tanzania Daima sababu za kushindwa kutangazwa kwa taarifa za kifo hicho mapema alisema walilazimika kufanya hivyo ili wapate fursa ya kuwasiliana na serikali kwanza na kisha ndugu, jamaa na marafiki wa familia yao kabla ya habari hizo kusambazwa."

Maswali la kujiuliza:
- Balalli si mtumishi wa serikali, lakini kwanini wanafamilia wameona serikali ndio wa kwanza kufahamishwa kuhusu kifo cha Balalli kabla ya ndugu, jamaa na marafiki wa Balalli?
- Kama serikali walikuwa wa kwanza kufahamishwa (that means Ijumaa au Jumamosi, au tuseme Jumapili), kwanini wako kimya mpaka leo hii (Jumatano)?

Kulikoni!!
 
Leo tuu watu hawa wamejiunga, kwasbb JF inatoa habari kwanza, nikimbilio la wanaoipenda nchi yao na hapa YOU DARE TO TALK OPENLY

KARIBUNI SANA, sasa kazi ni moja tuu... mpaka kieleweke

nelly20 21-05
winlamarwa 21-05
atibu 21-05
mwasigo 21-05
Tujisenti 21-05
 

Ngoja mimi nikalale maana maswali ni mengi mno kuliko majibu.

Huwa wanasema msiba haujifichi. Hakuna kitu kama kufiwa.

Yaani mtu anafiwa na baba au mama au mme wake eti ananymaza hili aweze kuitaarifu serikali? Hapa ni Changa tu, kama ni kutaka kubadili jina sasa litabatilika. Rudisha Balali ajibu tuhuma zake tu.

Hii ndiyo mara yangu ya kwanza kusikia statement za namna hii.
 
 
Kwa mazingira yalivyo sasa sio rahisi ndugu zake wakauleta mwili wake hapa Tz kuuzika.
Watazika huko huko labda watakuja kuuhamishia huku miaka ijayo kama alivyofanyiwa Mobutu na sasa nasikia Idd Amin naye maandalizi yanafanyika!
UFISADI una gharama zake. Aliowasaidia kutajirika na kupata madaraka WANASEMAJE?
 

Inawezekana hao mawakili hawakufaidika isivyo halali na fedha hizo hizo za EPA??
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…