Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bandugu,
Ballali ameaga dunia. I have confirmed this and I have to keep you guys informed.
More news to follow
Hata TBC1 (RTD), RFA na Radio One "wameikwepa" habari hii mchana huu!
Mida hii si mizuri kwa alio Marekani kwani hawajakaa mkao wa kupigiwa simu na kuhojiwa.Invisible tupe updates zozote kama unazo kuhusu Ballali.
Dah, wengi 'wanaikwepa' na wengine wanauliza 'kwanini mmeiweka'?
Lakini Tanzania Daima hawakufanya ajizi, pamoja na kuwa wakati issue hii inatoka walishachapisha gazeti la leo iliwabidi kutoa "Toleo maalum" kuhakikisha hawakai na habari hii.
![]()
![]()
Mida hii si mizuri kwa alio Marekani kwani hawajakaa mkao wa kupigiwa simu na kuhojiwa.
Naomba muda kidogo... I will make sure nakuja na kauli inayoeleweka. Nina maswali 4 nimeyaandaa kuwauliza.
- Ballali kafa Ijumaa kweli au kafa kabla ya hapo?
- Kwanini azikwe Marekani? Ni sehemu ya wosia wake?
- Inasemekana kabla ya kukata roho alimtaja aliyemlisha 'sumu', tunaweza kupatiwa jina la mtu huyo?
- La nne ni siri yangu 🙂
Huu ni uwongo 110%. balali si mtu mdogo namna hii, kama angekutwa na mauti ofisi ya balozi wa tanzania nchini America wangejua na wangetoa taarifa kwani hakuna sababu ya kuficha kifo.
Yaani hadi sasa serikali haijasema lolote.....??
Invisible na Mkjj mmekuwa mnatoa taarifa indirectly. Najua tayari unayo majibu ya maswali yako hapo juu so mwageni mchele hapa, maaana sioni sababu ya kuzunguuuuka wakati ukweli tayari mnaufahamu
Balali ni nani mbona kifo chake kimekuwa siri sana!mbona hayati Rutihinda kifo chake hakikuwa siri na alikuwa Gavana pia?ila serikali ilisema haimtambui balali maana si mfanyakazi wao tena!Balali itakuwa umekufa na siri nzito!
Nanukuu kutoka Tanzania Daima:
"Ndugu mmoja wa Ballali alipoulizwa na Tanzania Daima sababu za kushindwa kutangazwa kwa taarifa za kifo hicho mapema alisema walilazimika kufanya hivyo ili wapate fursa ya kuwasiliana na serikali kwanza na kisha ndugu, jamaa na marafiki wa familia yao kabla ya habari hizo kusambazwa."
Maswali la kujiuliza:
- Balalli si mtumishi wa serikali, lakini kwanini wanafamilia wameona serikali ndio wa kwanza kufahamishwa kuhusu kifo cha Balalli kabla ya ndugu, jamaa na marafiki wa Balalli?
- Kama serikali walikuwa wa kwanza kufahamishwa (that means Ijumaa au Jumamosi, au tuseme Jumapili), kwanini wako kimya mpaka leo hii (Jumatano)?
Kulikoni!!

Kulikoni!![/QUOTE
Issamichuzi ambaye alichelea kuandika habari hizi kwa kisingizio hajapata udhibitisho amesema yafuatayo
Balali Kuzikwa Boston. ....Aliyekuwa gavana wa Benki kuu amefariki dunia siku mbili zilizopita atazikwa siku ya ijumaa huko boston.... anasema habari hizo zimethibishwa rasmi na ndugu wa karibu wa balali waliopo US pia Benki kuu ya Tanzania imedhibitisha..
Nilisikia kwamba aliwaeleza mawakili wake kuhusu sakata zima la BoT pamoja na wahusika wake na yeye alihusika kwa namna gani, ikiwa ni pamoja na kuwapa nyaraka muhimu zinazothibitisha yote hayo. Sasa kama kafa hao mawakili wako wapi walete hizo taarifa humu kwenye jamvi?