Daudi Ballali's Death

Daudi Ballali's Death

Status
Not open for further replies.
magazeti yapi? Tz daima lasema atazikwa huko huko ijumaa.
 
Kama ni kweli taarifa hii, Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi Watanzania katika kulinda na kuhifadhi AMANI ya Nchi yetu. Najaribu kufikiria ushahidi wake (mahakamani) "marehemu" ungeiweka wapi CCM na mustakabali na hatima ya Nchi yetu.
 
Habari hii nimehakikishiwa ni kweli imetolewa na Tanzania Daima kwenye habari zilizopewa umuhimu mkubwa kwenye front cover.Nitaweka extract ya Tanzania Daima soon ili wana JF muweze kuchangia maoni yenu.
 
Najaribu kufikiria ushahidi wake (mahakamani) "marehemu" ungeiweka wapi CCM na mustakabali na hatima ya Nchi yetu.

Mkuu nani amekwambia mstakabali wa nchi hii na amani iliyopo ni CCM? Sio kweli mbona mnadanganywa na manakubali tu? Mstakabali wa nchi hii ni wananchi na kama wananchi tukikataa kupigana hakuna atakaye aanza kumpiga mwenzake, si unaona Zim watu wameamua kuwa kimya wanasubiri awamu ya Pili, ni chama tawala ndio kinapiga na kuua watu, huko kenya watu waliamua kuchukua hatua. Kwa hiyo hata sisi hapa Bongo tukiamua kuwa kimya kutochukua marungu na mapanga tunaweza na wala sio CCM. Jamaani hii notion ya CCM ndio amani na Bila CCM hakuna amani ndiyo imetufikisha hapa, na sasa akina Balali wanakuwa Kondoo wa sadaka kutokana na mfumo wa kifisadi uliojengwa na nyie mnaosema bila hawa watu hakuna Amani.
 
Inakuwaje kila anayehusika na maovu hapa TZ, muda si mrefu utasikia kasha vuta, do!!!, hapana kuna siri jamani,

- Tunamwitaji Balali wetu,

- ama ndiyo ushahidi KWISHA?
 
Kwanza nalia kwamba, kama habari hii ni ya kweli, basi Balali amekwenda huko kuzimuni na siri yote ya ufisadi wa pesa zetu pale BoT; labda kama aliweza kuandaa dossier ya kina na kuliacha kwa mwanasheria wa kuaminika. Mpakla leo ninaimani kuwa Balali alikuwa ni tundu tu la kupitishia kinyesi kile ingawa kwa hali hiyo alikuwa anabaki na mopako wa kinyesi na haikuwa rahisi kwake kujichamba katika mazingira hayo. Najua kuwa kifo cha Balali kitapokewa kwa furaha na vigogo wengi ndani ya mfumo wa utawala wa nchi yetu.

Kinachonishangaza ni huu utabiri wa Mwanakijiji hapa JF:

Kuelekea Summer ya Mwaka jana alitabiri jambo baya kuhusu marehemu AC hapa JF nalo likatokea. Kuelekea Summer ya Mwaka huu akatabiri jambo baya kuhusu huyu bwana Balali ambalo nalo linaelekea kuwa limetokea. Nitafurahi sana kama kuelekea summer ya mwaka kesho Mwanakijiji atatabiri jambo baya kuhusu mafisadi wote wa Tanzania, na litokee .

Mwalimu,

Naamini Mwanakijiji alijua hili na huenda kama kweli amekufa basi hajafa jana na alikufa muda.

Lakini pia inawezekana kuna usanii unafanyika, wanambadilishia vitambulisho na sisi tunaanza kufungwa bao tena na wachezaji ambao tulikuwa tunaamini ni walinzi wa goli letu.

Kuna watu siwasikii wakiongea, inanipa wasiwasi.

I hope hamjamdanganya ndugu yetu Invisible maana naamini Invisible hawezi kuandika bila kuhakikishiwa kabisa na baadhi ya watu wa karibu na Ballali.

Tuombee iwe kweli maana isipothibitishwa basi JF tutakuwa tumefungwa goli la kisigino.
 
naenda kulala poleni.... ila kumbukeni "nyie tuzugeni tu, mtaona maajabu"..! You made your move others are contemplating theirs... and somebody will be checked soon! adios
 
Mkuu nani amekwambia mstakabali wa nchi hii na amani iliyopo ni CCM? Sio kweli mbona mnadanganywa na manakubali tu? Mstakabali wa nchi hii ni wananchi na kama wananchi tukikataa kupigana hakuna atakaye aanza kumpiga mwenzake, si unaona Zim watu wameamua kuwa kimya wanasubiri awamu ya Pili, ni chama tawala ndio kinapiga na kuua watu, huko kenya watu waliamua kuchukua hatua. Kwa hiyo hata sisi hapa Bongo tukiamua kuwa kimya kutochukua marungu na mapanga tunaweza na wala sio CCM. Jamaani hii notion ya CCM ndio amani na Bila CCM hakuna amani ndiyo imetufikisha hapa, na sasa akina Balali wanakuwa Kondoo wa sadaka kutokana na mfumo wa kifisadi uliojengwa na nyie mnaosema bila hawa watu hakuna Amani.

Sikumaanisha hiyo tafsiri ulioitoa hapa Mkuu.
 
Invisible
Tuambie kilichomuua balali, haiwezekani na haituingii akilini hata kidogo, kwa kuwa wewe umeongea na jamaa zake, tell us pleaseeee !!!!!!!!!!!,
 
naenda kulala poleni.... ila kumbukeni "nyie tuzugeni tu, mtaona maajabu"..! You made your move others are contemplating theirs... and somebody will be checked soon! adios

Mkuu mwana kijiji una utaalam wa kusoma Nyota? kwani juzi tuu nilikuwa nawasomea washikaji ile post, yako na leo kila mtu ananipigia kuuliza mkuu inawezekana Jamii mlikuwa tayari mna DATA. hata mimi naanza kuamini kama wewe sio mtaalamu wa Nyota basi ulikuwa na DATA.
 
hii game inayochezwa na ccm/mafisadi naona inazidi kuwa kali kila kukicha.
i am more interested in knowing "what next" kwa upande wa mafisadi, na kwa upande wa anti-mafisadi
 
Mkuu, kuna zaidi usiyoyajua kuhusu hili. Mpe heshima yake marehemu na kama ni kuwambia watanzania NAKUHAKIKISHIA kawambia... Ni suala la muda tu!

YES, nakwambia,,, alisema. Kwa maandishi? Sijui!

SIna maana ya kuto kukuamini, ila kwa sasa sina sympathy nae kama mkuu NYANGUMI, mpaka hapo nitakapo pata habari/ ushahidi alioutoa, kwann asingeruka hewani akiwa hai... ingekuwa nzuri sana hiyo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom