Kafulila anadanganya, kazi yake ni kupiga debe sio kusimama katika ukweli.Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila hivi ndivyo alivyoandika baada ya baadhi ya Watanzania kushangaa kauli ya Rais Samia Suluhu kuhusu Tanzània kununua Umeme nje ya nchi, Ethiopia.
Mkurugenzi Kafulila anasema pamoja na kwamba nchi kubwa na tajiri duniani kama Marekani ( USA ), Ujerumani, Norway, Sweden au Australia wanaumeme mwingi kiasi Cha kuuza nje ya nchi zao bado na wao kwa Upande mwingine wa nchi zao wananunua umeme kutoka nje ya nchi zao.
Soma Pia: Rais Samia: Serikali itanunua Umeme nje maalum kwa Mikoa ya Kaskazini
Kafulila anasema kuwa baadhi ya maeneo ya nchi yetu hasa maeneo ya mipakani gharama ya kuzalisha, kusafirisha na kufikisha umeme maeneo hayo ni kubwa pengine kuliko gharama ya kuuvuta na kuununua umeme toka nchi za jirani.
Katika nadhariia ya umeme power loss ni kitu kisichokwepeka na kinachokubalika ni sawa na Lori linalotembea kuna vyuma na parts vinasagika hivyo baada ya muda huwa vinabadilishwa. Hivyo mwenye gari anapochaji gharama za uchukuzi wa miizigo anaweka pia gharama za uchakavu ili baadae aweze kununua speak pale zitakapokuwa zimechakaa.
Umeme unaposafirishwa hata ndani ya wilaya moja au toka nyumba moja kwenda nyumba nyingine kuna power loss inatokea ambayo kitaalamu ni ( I squared times R). Ni kweli jinsi umbali unavyoongezeka ndivyo power loss nayo inaongezeka lakini ni kwa kiasi kidogo sana.
Kukabiliana na hilo la power loss, umeme unapozalishwa hatua ya kwanza unapandishwa juu sana mfano kutoka 33 KV zilizozalishwa kwenda 220 KV kwa kutumia step up transformer kabla ya kusafirishwa; hivyo unasafirishwa katika very high voltage; kitendo hiki kinasababisha current( I) ipungue sana hivyo kushusha power loss kitaalamu ( kumbuka formula ya power loss kihesabu za umeme ni (I times I times R). Umeme ukifika unakoenda unashushwa voltage kwa kutumia step down transformer hadi kiwango kidogo cha voltage mfano 11 KV katika sub stations, nao unasafirishwa ndani ya mji hadi majumbani na kushushwa tena kwa kutumia step down transformer zilizoko katika nguzo za umeme ili kuwa 415 Volts. Kitendo cha kupunguza voltage hupandisha current ( I ). Hizi ndio technique zinazotumika kudhibiti power loss kitaalam.
Ndio maana miaka yote huko nyuma umeme wa kidatu ulisafirishwa hadi Mwanza, Mbeya na maeneo ya mipakani kama Tarime ambapo ni zaidi ya km 1300 lakini tulikuwa hatusikii hizi ngonjera za power loss. Jiulize kwa nini sasa Kafulila na wengine wanapigia kelele ngonjera za power loss.
Mfumo wa tarrif wa kutoza gharama za.matumizi ya umeme unazingatia gharama zote kuanzia uzalishaji, usafirishaji, usambazaji, matengenezo, uchakavu,. Pia gharama walizotozwa watumiaji zililingana. TANESCO tangu mwaka 1991 imekuwa ikikumbwa na ubadhirifu mbalimbali unaotokana na mikataba isiyozingafia maslahi ya nchi na hiyo ndiyo ilifanya gharama za umeme ziwe juu kulinganisha na nchi zingine
Kafulila aelewe hata kuutoa umeme toka kwenye nguzo hadi ofisini au nyumbani kwake kuna power loss pia. Ni kama nilivyoeleza juu kwa kutumia mfano wa gari ya mizigo inapobeba mizigo.
Kingine, umeme unapozalishwa toka vyanzo mbalimbali unachanganywa katika grid ya Taifa ni kama maji yanavyochanganyika na kuwa kitu kimoja kwa sababu dunia nzima umeme unazalishwa katika makundi matatu tu yanayoitwa kitaalamu three phases huwa zinakuwa labelled Red, blue & yellow phases. Sasa wanaposema tunauza umeme wa mpakani sio sahihi kwa sababu umeme unakuwa umechanganyika kama maji huwezi kuutenga kuwa huu ni umeme wa pangani na huu ni wa kidatu na huu ni wa Rusumo nk hivyo ninauza umeme wa Rusumo siuzi umeme wa kidatu.
Hivyo concept ya power loss inayotumiwa sasa ni vehicle tu ya kuhalalisha maamuzi mabovu na ni hoja mufilisi.