David Kafulila amvaa Luhaga Mpina deni la Taifa

Kuna chama Cha rushwa kama CHADEMA?
 
Kitu kimoja napenda toka kwa Kafulila anaweza akakukibu mpaka ukajiona huna akili kabisa,
🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Umeona ee?!!!!
Tatizo la kuibua mambo kwa lengo la kupata sifa ni kwamba Kuna Kuna umakini flani unakutoka wakati wa kusema, ukishamaliza ndo unajua kuwa Kuna sehemu kumbe ulichemka.
 
Hoja ya msingi ni deni la Taifa kuwa kubwa sana hali inayo sababisha 1/3 ya makusanyo ya kodi kwenda kulipa madeni ya mikopo na riba zake. Mkopo ni mkopo, haijalishi umeingia kwenye mfuko mkubwa wa serikali ama umeenda kwenye mradi moja kwa moja; kimsingi mikopo yote huwa inasajiliwa.
 
Wewe ni kama nani hapo hazina?

Wewe ni CAG mpaka useme hakuna pesa zinazoibiwa?

Kuhusu mkataba wa DP world umeshapelekwa bingeni au zuga zenu maccm kuwafanya eananchi mazuzu?

Ni lini ccm kumekuwepo watu wenye brain usiochakachuliwa?
 
Pesa za kuendeshea Singuda black stars zinatoka hazina
 
Wewe kichwa nazi kweli? Naomba utuoneshe hiyo miradi ya trillion 7 ambayo serkali imejenga au kufanya!
Chawa kama nyinyi ndo mnarudisha nyuma sana maendeleo!
 
Kitu kimoja napenda toka kwa Kafulila anaweza akakukibu mpaka ukajiona huna akili kabisa,
We kweli huna akili, ilitakiwa huyo tumbili wako atoe ushahidi wa hayo anayoyasema ili tujiridhishe kama ni kweli...hapo kaongea kiujumla ni rahisi kusema uongo!.
Atoe lists ya miradi kadhaa na kiasi cha pesa kimetolewa.
Kwa mtu mwenye akili, haya majibu ya tumbili yanazidi kukazia madai ya mpina ni ya kweli kabisa!!.
 
Aisee, issue sio kutetea kila kitu.

Kukopa ni jambo jema tu kama hela inakwenda kwenye matumizi sahihi na mianya wizi na ujinga ujinga havipo.

Unawezaje kutetea kukopa huku ndani ya nchi Kila siku ni kubomoa na kujenga kwasababu ya kukosa plan, unaweza kutetea mikopo kama miradi mingi serious tunashindwa kuiendesha mfano SGR, ATCL, TTCL nk

Unaweza kutetea kukopa wakati matumizi ya serikali yapo juu, watu wanakwiba na kuchezea hela za umma, watu wanatumia hovyo hovyo tu vitu na mambo ya ajabu.

Naamini tunaweza kutetea mikopo kama Kila kitu ndani kinakwenda sawa, na hiyo mikopo kweli tutakuwa tunaihitaji.
 
Majibu yasiyokuwa na akili kabisa Ndio haya! Anaona Kila Mtanzania ni mjinga mjinga. Kwahiyo anathibitisha kwamba ni kweli serikali ya chama chake Ina matumizi mabaya ya fedha za mikopo na zile za wahisani! Kiasi kwamba hawaaminiki tena na jamaa wanaenda field Moja kwa Moja? What a waste
 
Huyu chawa ana jipya gani zaidi ya kutetea tumbo lake kwa waliomteua?
 
Mmh
Chini ya huyu mazeri wako lolote linawezekana...hata ye mwenyewe haelewi!.
 

First things first mimi si fan wa Mpina wala Kafulila. Naangalia mantiki tu.

Suala la namba hujibiwa kwa namba.

Hata kama jibu la Kafulila lina ukweli, jibu limepwaya kwa sababu Mpina kaweka namba, ilitakiwa Kafulila naye aweke namba wakopeshaji wangapi wamepeleka fedha kiasi gani moja kwa noja kwenye miradi.

Kwa sababu, bila namba, jibu la Kafulila linaweza kuwa kweli, lakini tuhuma za Mpina bado zikawa na maana kama kuna gap kati ya fedha za wakopeshaji wanaopeleka fedha zao moja kwa moja kwenye miradi na figure ya Mpina.

Nimeeleweka?

Kwa nini Kafulila hajaweka namba? Ni mzembe? Kafulila si mzembe hivyo.

Hazipo? Namba muhimu kama hizi haziwezi kukosekana serikalini.

Anaficha kitu?

Kitu gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…