David Kafulila: Hakuna siku Serikali itaacha kukopa kwani hata Marekani na China nao wanakopa zaidi ya Tanzania

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029
===
Akiongea katika Kipindi cha DK 45 kinachorushwa "LIVE" na kituo cha runinga cha ITV Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi nchini PPPC Bw David Kafulila alikuwa na haya ya kuwaambia Watanzania,

Akifafanua kuhusu Tanzania kuendelea kukopa na kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo alisema "Kiuchumi na Kibiashara huwezi kukopeshwa kama huna uwezo wa kukopesheka ili mtu au taasisi ikopeshwe kwa masharti mazuri Lazima awe vizuri Kiuchumi hii ni Sayansi ipo kuanzia ngazi ya familia mpaka Ile ya Serikali" alisema Bwana David Kafulila.

Tanzania imepimwa kwa vigezo vyote ukianzia na vile vya World Bank, IMF na hata taasisi za credit rating kama Moody's na Fitch wote wanasema Tanzania deni lake ni himilivu na stahimilivu ndio maana hakuna siku Serikali itaacha kukopa hata Marekani, China, Urusi na Japani wote hawa wanakopa alisisitiza Kafulila.

China Taifa lenye dhahabu nyingi kuliko Taifa lolote Dunia inakopa, Urusu yenye gesi nyingi duniani nayo inakopa Marekani yenye utajiri wa Mafuta duniani nayo inakopa mtu anayesema Tanzania tunarasilimali hivyo tusikope ukweli ni kwamba Tanzania hatuna rasilimali zote zote kuyapiku hayo mataifa lakini na wao wanakopa tatizo sio kukopa labda tatizo liwe unakopa kwaajili ya kufanya nini ila kukopa ili kujenga miradi ya Maendeleo ndio haswa tunapashwa kuendelea kukopa- alisema David Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC-Tanzania.

Sasa msikilize mpaka mwisho.





Your browser is not able to display this video.

===
 
na huo ndo ukweli hamna taifa regardless ukubwa halikopi kwa waliosomea uchumi wanaelewa....ila je export yetu kupata foreign currency iko poa? sector za kuzingatia ni kilimo,mining, tourism,indusries and export, technology, diaspora earnings, import regulation .....maoni yangu
 
Very true, hasa kilimo
 
Huku mtaani kuna mikopo kausha damu, nini maana ya mikopo kausha damu ni mikopo ambayo mzunguko wako wa maingizo,(cash flow),kwa siku ama kwa mwezi ni kidogo kuliko hela za marejesho mfano maingizo yako kwa siku ni elfu 5 halafu marejesho ni elfu 8 huo utakuwa ni mkopo kausha damu, vile vile nasisi kama maingizo yetu pamoja na matumizi ya lazima hayawezeshi kuulipa mkopo utakuwa ni kausha damu
 

Ni kwa nini kuku akitaga mayai yake wewe unachukua na kuyala wakati wewe mayai yako unayaficha kiunoni?
 
Mfano mzuri sana huu😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…