David Kafulila: Hakuna siku Serikali itaacha kukopa kwani hata Marekani na China nao wanakopa zaidi ya Tanzania

David Kafulila: Hakuna siku Serikali itaacha kukopa kwani hata Marekani na China nao wanakopa zaidi ya Tanzania

===
Akiongea katika Kipindi cha DAKIKA 45 kinachorushwa "LIVE" na kituo cha runinga cha ITV Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi PPPC David Kafulila alikuwa na haya ya kuwaambia Watanzania,

Akifafanua kuhusu Tanzania kuendelea kukopa na kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo alisema "Kiuchumi na Kibiashara huwezi kukopeshwa kama huna uwezo wa kukopesheka ili mtu au taasisi akopesheke kwa masharti mazuri Lazima awe vizuri Kiuchumi hili ni Sayansi ipo kuanzia ngazi ya familia mpaka Ile ya Taifa" alisema Bwana David Kafulila.

Tanzania imepimwa kwa vigezo vyote ukianzia na na vile vya World Bank, IMF na hata taasisi za credit rating kama Moody's na Fitch wote wanasema Tanzania deni lake ni himilivu na stahimilivu ndio maana hakuna siku Serikali itaacha kukopa hata Marekani, China, Urusi wote hawa wanakopa alisisitiza Kafulila.

China Taifa lenye dhahabu nyingi kuliko Taifa lolote Dunia inakopa, Urusu yenye gesi nyingi duniani nayo inakopa tatizo sio kukopa labda tatizo liwe unakopa kwaajili ya kufanya nini ila kukopa ili kujenga miradi ya Maendeleo ndio haswa tunapashwa kuendelea kukopa- alisema David Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC-Tanzania.

Sasa msikilize mpaka mwisho.



View attachment 3224599


===
Huyu jamaa anajua sana kunyoosha maneno Mpina natamani apite hapa
 
Kwenye kukopa wanashindana na marekani na china ila kwenye maendeleo ukiwauliza utajikuta umetekwa 🤣🤣
Sio kweli, Mwigulu Aliwahi waambia Bungeni kwamba ishu sio kukopa ishu iwe zimetumika wapi
 
Shida sio kukopa. Tatizo wanazifanyia nini baada ya kukopa?
 
Wanakopa kufanya nini maana Chalamila katuambia tuwafanyie upasuaji wake zetu, gloves hospitali hakuna muda wote
 
Back
Top Bottom