David Kafulila: Hakuna siku Serikali itaacha kukopa kwani hata Marekani na China nao wanakopa zaidi ya Tanzania

===
Akiongea katika Kipindi cha DAKIKA 45 kinachorushwa "LIVE" na kituo cha runinga cha ITV Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Serikali na Sekta binafsi PPPC David Kafulila alikuwa na haya ya kuwaambia Watanzania,

Akifafanua kuhusu Tanzania kuendelea kukopa na kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo alisema "Kiuchumi na Kibiashara huwezi kukopeshwa kama huna uwezo wa kukopesheka ili mtu au taasisi akopesheke kwa masharti mazuri Lazima awe vizuri Kiuchumi hili ni Sayansi ipo kuanzia ngazi ya familia mpaka Ile ya Taifa" alisema Bwana David Kafulila.

Tanzania imepimwa kwa vigezo vyote ukianzia na na vile vya World Bank, IMF na hata taasisi za credit rating kama Moody's na Fitch wote wanasema Tanzania deni lake ni himilivu na stahimilivu ndio maana hakuna siku Serikali itaacha kukopa hata Marekani, China, Urusi wote hawa wanakopa alisisitiza Kafulila.

China Taifa lenye dhahabu nyingi kuliko Taifa lolote Dunia inakopa, Urusu yenye gesi nyingi duniani nayo inakopa tatizo sio kukopa labda tatizo liwe unakopa kwaajili ya kufanya nini ila kukopa ili kujenga miradi ya Maendeleo ndio haswa tunapashwa kuendelea kukopa- alisema David Kafulila Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC-Tanzania.

Sasa msikilize mpaka mwisho.

View attachment 3226348
===
Kafulila ndio mwanaCCM pekee ambae amejielekeza kuitetea CCM Kwa hoja sio vihoja, nampongeza
 
"I know the leaders, and I know the idiot" - PK
"If you are a leader, and an idiot, its the disaster" -PK
 
Haijalishi ina harufu ya CCM au ya mavi yako ila wewe ni mpuuzi sana haya maID mengi humu hayawezi kukusaidia kwa lolote lile
Acha umalaya basi nitoe kwenye swaga za kifala Mimi siwezi kuwa CCM kwani kusema Kafulila kirusi wewe imekuuma Nini?
 
Huyo ni mwehu eti kila anayemkubali Kafulila anasema huyo ni Kafulila huo ni Ujinga wa kiwango Cha lami
 
Kwenye kukopa wanashindana na marekani na china ila kwenye maendeleo ukiwauliza utajikuta umetekwa 🤣🤣
Yuko sahihi, hata hapa kuna mtu anakopa bank laki tu ndio uwezo wako na wako watu hata Billion 100 nakopesheka ni kawaida hakuna kitu cha ajabu. Bank inakukopesha kutokana na uwezo wako kiuchumi je unaweza kulipa? System ni ileile mikopo binafsi wanatumia kwa nchi. Mtu binafsi ukitaka wanahakikisha labda 60% unaweza kutoa kwenye income yako huwezi kukopeshwa 100%. Na nchi wanatizama % ngapi nchi inaweza kuhimili deni bila kuathiri nchi. Ndio maana unasikia jana Trump anasema USA wanadeni la Trillion 36, pesa ambayo Africa nzima hatuwezi tukijichanganya. Shida kama unakopa kwa matumizi ya kawaida ya serikali hapo hupewi sababu huwezi kulipa deni. Ni sawa ukakope Bank ili ukanunue gunia la mahindi wewe hukoposheki ni fukara.
 
Huo ni Udumavu badala ya kuzingatia tusimamie mali tulizonazo tupo busy na kukopa fedha kama vile hatuna kitu..asijifananishe na USA ambao leo hii wanakata misaada Duniani tunalalamika.
 
Yuko sahihi, hata hapa kuna mtu anakopa bank laki tu ndio uwezo wako na wako watu hata Billion 100 nakopesheka ni kawaida hakuna kitu cha ajabu. Bank inakukopesha kutokana na uwezo wako kiuchumi je unaweza kulipa? System ni ileile mikopo binafsi wanatumia kwa nchi. Mtu binafsi ukitaka wanahakikisha labda 60% unaweza kutoa kwenye income yako huwezi kukopeshwa 100%. Na nchi wanatizama % ngapi nchi inaweza kuhimili deni bila kuathiri nchi. Ndio maana unasikia jana Trump anasema USA wanadeni la Trillion 36, pesa ambayo Africa nzima hatuwezi tukijichanganya. Shida kama unakopa kwa matumizi ya kawaida ya serikali hapo hupewi sababu huwezi kulipa deni. Ni sawa ukakope Bank ili ukanunue gunia la mahindi wewe hukoposheki ni fukara.
Tatizo sio kukopesheka wala kuhimili deni, tatizo unakopa kufanyia nini?
Yani unachokitetea wewe ni sawa ukute kuna kijana ameachiwa urithi wa ardhi na wazazi alafu badala apambane ajenge kwenye ardhi alizoachiwa, ameamua kila akipata shida kidogo anaenda benki kuchukua mkopo kwa dhamana ya ardhi ileile aliyoachiwa urithi, alafu anaenda kustarehe akijua zikiisha kuna shamba lingine lipo wilaya fulani au mkoa fulani ataweka tena rehani kwa udhamini wa bank.

Kijana huyu ni mpumbavu na mwisho mashamba yakiisha atawehuka au kuwa mtumwa wa watu wengine ili mkono uweze kwenda kinywani.

Bwana Heijah kwa utetezi wako huu huoni una sifa za huyu kijana kabisa?
 
Sasa wewe umehukumu kabisa, ndio maana nimesema hakuna Bank yoyote ikakuposha ila ukanywe kwa starehe na ukifanya hivyo wewe ni mufilisi mtarajiwa huwezi ku recover hiyo land. Sasa kwenye mikopo ya nchi huko wako strickly sana katika masharti. Mimi sitaki kuamini kama serikali imekopa ikalipe mishahara au kustarehe huu ni mjadala mwingine kabisa.

Swali je kukopa ni kosa? jibu hapana na haitafika siku tukaacha kukopa na sababu ziko wazi mahitaji yanakuja kwa haraka kimaendeleo kuliko ukuwaji wa kiuchumi. Je mikopo tunatumia kwenye miradi tuliyokopea? nataka kuamini hivyo ila kama haikuwa hivyo hapo tunahaki ya kusema hapana na waliokopa ndio inabidi waulizwe na waoneshe mkopo umetumika kama dhumuni la mkopo.

Hakuna mkopo unatolewa kujumla tu ndio maana kila mkopo ukitoka wanasema huu unaenda kusaidia elimu au kujenga chuo au anything lakini wanakopa kwa madhumuni, huwezi kwenda kukopa ukasema kwa ajili ya mishahara ukisema hivyo wewe ni umefilisika na pesa yako itaanguka kufungia vitumbua. Hoja hapa je ule mkopo wa kujenga barabara Km 20 kwa mfano ulitumika kujenga Km 20?

Kuhusu huyo kijana hata kama una land haitoshi wewe Bank kukupa mkopo maana Bank haihitaji land inahitaji pesa yake kurudi, kuweka ardhi kama dhamana haikufanyi ukapata mkopo ni lazima uoneshe unakopa kwa ajili ya nini? uwezo wa kurudisha pesa unao? kama biashara onesha mzunguko wako kama muajiriwa onesha slip yako land ni kitu cha mwisho maana kama Bank wanataka ardhi yako usingeulizwa yote hayo kwa kuwa Bank wangekuwa wanaomba ushindwe kulipa ili wachukue ardhi yako, ukishinda kulipa inapigwa mnada na Bank wanachukuwa chao tu sio pesa ya jumla ya kwenye mnada hapa utajuwa Bank wanataka pesa yao kibanda chako.
 
Nina mengi ya kusema tatizo ni mvivu kuandika... Kwa kifupi kuna mataifa yanatoa mkopo bila masharti, alafu mengine yanatoa kwa masharti lakini hela zikishachukuliwa ndio basi tena hawafuati yale masharti.

Alafu ili tuwe salama kwenye hii mikopo hatuhitaji masharti ya wakopeshaji sababu walipaji ni sisi!
Usalama wetu tunahitaji viongozi wawajibikaji wasiopenda rushwa wala kutoa rushwa, wafuatiliaji na bunge lililoko serious tofauti na hili ambalo ni kichekesho.

Watanzania wote tunatakiwa tuwe na wivu na nchi yetu, tuipende na kuitetea.
 
Kaongea nini Cha uongo?
Tatizo la watu wa aina ya Kafulila, ni kurahisisha mambo magumu; na bahati mbaya wanakutana na waandishi wa habari ambao ni lightweight.

Shida ni currency gani unakopea....

USA anakopa kwa Dola, ambayo ni pesa yake.... wewe unakopa kwa Dola ambayo sio pesa yako.
 
Back
Top Bottom