David Kafulila: Miaka 25 ijayo Serikali itajenga Uchumi wa $700bn. Pato la kila mmoja wetu litafikia TZS 20M

Hii ni kama story za "... receive a house receive a car..."
 
Uchumi wa gdp ya usd billion 700 kumbuka afrika hakuna nchi ambayo imefikia mpaka sahivi
Wewe Tanzania una-mpango gani wa kuufikia

Ni ngumu sana kuendelea as long uchumi wetu ni demand side economy ambao unategemea bidhaa za ku-import ili nchi iendelee lazima iwe ni demand side economics
 
20M siyo shida, thamani ya shilingi ikiwa ipoje wakati huo?
 
Wameshindwa wapi? Shule ipi ya huko kwenu Haina matundu ya vyoo?
Nani kakwambia matundu ya vyoo ni salama kwa afya, Wenzenu wanatumia vyoo vya flushing ninyi bado huko kwenu Tandahimba mnafikiria matundu ya vyoo ambavyo siyo salama. Kweli nchi hii ina watu wajinga kama wewe, yaani bado mpo nyuma kweli kweli. Sasa ni hiyo USAID imekata misaada na hayo matundu ya vyoo yataadimika.
 
Kweli kuna vitu havijazingatiwa:
Mfano:
Elimu,tumeendelea na mfumo kuwa na wanafunzi wanaomaliza shule wengi hawawezi kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza,wengine wamefaulu huku hawajui kusoma na kuandika.Mfumo wa "English medium" kwa shule za umma,ni kwa wachache,kama Taifa tumefanya unafiki,hatujadili,na wananchi hawapewi ukweli ni kwa nini Serikali inapata kigugumizi(kiu ya kila mwananchi ni kuwa nao wanataka watoto wao wasome shule za English medium),itasaidia kuwa nguvu yenye uwelewa na tayari kufanya kazi na wawekezaji wanaotajwa kuwa ndio kichochea cha ukuaji wa uchumi.

Kilimo,kama nchi tunalima kilimo cha kawaida ,nimefuatilia mazao ya biashara bado tunaachwa sana,tuangalie mfano zao la korosho,bado wakulima hawajawa wepesi kubadili miche mipya,miti ya mikorosho ni ya zamani bado Ivory Coast ametuzidi katika uzalishaji wa zao hili,Wizara husika wakajifunze Ivory Coast wanafanyeje na kufanikiwa katika kilimo hiki(wao kwa mwaka wanazalisha tani 970,000,sisi tunazalisha tani 400,000).
Zao la kahawa limekosa usimamizi,nchi zingine wanalima na kuendelea kuuza sisi zao wakulima wanalikimbia!

Tunakila aina nzuri ya hali ya hewa ya kuwezesha kulima mazao yenye thamani kubwa kama cocoa,vanilla n.k lakini Taarifa na ukweli haujadiliwi hata kwenye "vision 2050!!"

Barabara za kiwango cha lami kuunganisha Wilaya na Mikoa kasi imekuwa ni ndogo, na haizungumzwi kwenye vision 2050!

Kweli GDP zinazokadiriwa haziwezi kufikiwa kama mambo hayo ambayo tunayafanya kila mwaka hatuyaboreshi(Elimu,barabara,kilimo)
 
Ukiangalia South Africa ya Leo kwa Miundo mbinu ile na Maendleo yale kwa Nchi kama Tanzania kwa Miaka 25 iyajo ni Mingi Snaaaa kama Selikali ipo Seriously ikitaka inawezekana Bila Shida ila kwa Selikali hizi za Kifisadi Kufanya Vitu kusubili Uchaguzi ndio Wafanye Au Wafungue Mradi watasubili Sanaa maendeleo ya Kweli Hayataki Siasa Kidogo Alijaribu Magufuri ila wengine hawa Siasa ndio Shida,siasa kwa Nchi za Africa ndio Umaskini unaosababisha Nchi haiendlei
 
Masikini Tanzania bandari ya bagamoyo mafisadi waichukua
 

Attachments

  • 20250213_171101.jpg
    104.5 KB · Views: 2
Shida yetu ni kuishi kwenye dunia ambayo elimu kwetu ni mzaha.

Yaani kiongozi anaweza kwenda kwenye media na kujiropokea tu.

Kama uchumi wa Tanzania leo ni $85 million, ili kufikia $700 million katika muda miaka 25 ijayo. Kwa mantiki hiyo GDP growth inatakiwa roughly 10.5% annually kwa miaka 25 mfulululizo.

GDP growth itatokana na sector zipi, serikali wana dira ya miaka 25 na Kafulila nae anamipango yake PPP (huo uwekezaji wake huko vipi in line na dira ya taifa anajua mwenyewe).

Uchumi wa Tanzania leo unakuwa kwa kiwango cha chini ya 5% na sehemu kubwa ya ukuaji kwenye circular equation ni mikopo ya serikali na sehemu kubwa ya hela watu wamezitafuna (hazijaingia kwenye uchumi).

Achilia mbali ufisadi the mere fact uchumi unakuwa kwa 5% ina maana kuanzia mwaka ujao inabidi uwe unakuwa kwa 10.5% uoni kama hawa watu wanajiropokea tu.

Hata sijui uwa wanaongeaga vitu gani huko nchi zilizoendelea wakikutana na wataalamu wa kweli. Asilimia kubwa ukiwasikiliza wanapwaya sana hawa watu.
 
Tutafikaje wakati Simbachawene ansema 60% ya watumishi wanalipwa lakini hawafanyi kazi
 
Ivi zile Noah tunapata lini? Ivi waliozaliwa baada ya lile tamko watapata mgao? To be fair wasipate, Ila waliokuwa hai wakati ule na sasa wamefariki bila kupata wanastahili kupata kupitia wasimamizi wa mirathi
 
Ingawa mchanganuo wake umekaa kinadharia sana lakini kauli yake inaleta morali
 
Ukitaka kuelewa hii vizuri nenda kaipitie Ile Dira ya 2000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…