David Kafulila: Miaka 25 ijayo Serikali itajenga Uchumi wa $700bn. Pato la kila mmoja wetu litafikia TZS 20M

David Kafulila: Miaka 25 ijayo Serikali itajenga Uchumi wa $700bn. Pato la kila mmoja wetu litafikia TZS 20M

View attachment 3199594
===
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Ubia nchi Tanzània PPPC Mhe David Kafulila amewaeleza Watanzania kuwa lazima wafahamu kesho ya Tanzània lao ni bora sana kama tu hali ya Umoja na mshikamamo itaendelea kuwa ilivyo leo.

David Kafulila anasema, Tanzania kwa kushirikiana na sekta binafsi ( PPP) ya ndani au nje ya Tanzania wataipeleka kwa Kasi Tanzania kwenye Uchumi wa viwango vya juu kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo kwa miaka 25 ijayo ( 2025-2050 )

Mtakumbuka, David Kafulila amekuwa ni Mtendaji na mwanasiasa anayejikita zaidi kwenye kutetea hoja za Serikali yake kwa namba na "fact" zenye kueleweka na watu wa Kada zote kitu kinachomfanya awe ni Mtendaji wa Serikali anayefuatiliwa zaidi mitandaoni kwa sasa.

Mkurugenzi Mtendaji huyu anasema Tanzània mpaka kufikia mwaka 2050 inatarajia kujenga Uchumi wa $700bn ambao ni karibu mara mbili ya Uchumi wote wa Africa ya Kusini ya leo ambayo Leo ni karibu $380bn.

Kafulila anasema si kazi rahisi kujenga Uchumi wa $700bn kutoka Uchumi wa sasa wa Tanzania wa $85bn kazi ambayo kamwe haiwezi ikatekelezwa kwa Kodi na Mikopo pekee hivyo sekta binafsi haepukiki kwenye safari hii ya ujenzi wa Uchumi mkubwa kwa kipindi kifupi cha miaka 25.

Mkurugenzi Mtendaji huyu anaendelea kwa kusema jambo hili linawezekana bila mashaka yoyote kwani hata nchi ya Vietnam mwaka 1990 ilikuwa na Uchumi wa $6.4bn lakini leo Vietnam wana Uchumi wa zaidi ya $460bn karibu mara themanini (X 80) zaidi.

Kama hivyo ndivyo kwanini Tanzania tusiweze Vietnam wao Wana nini?

View attachment 3196797

====
Hii ni kama story za "... receive a house receive a car..."
 
Uchumi wa gdp ya usd billion 700 kumbuka afrika hakuna nchi ambayo imefikia mpaka sahivi
Wewe Tanzania una-mpango gani wa kuufikia

Ni ngumu sana kuendelea as long uchumi wetu ni demand side economy ambao unategemea bidhaa za ku-import ili nchi iendelee lazima iwe ni demand side economics
 
Wameshindwa wapi? Shule ipi ya huko kwenu Haina matundu ya vyoo?
Nani kakwambia matundu ya vyoo ni salama kwa afya, Wenzenu wanatumia vyoo vya flushing ninyi bado huko kwenu Tandahimba mnafikiria matundu ya vyoo ambavyo siyo salama. Kweli nchi hii ina watu wajinga kama wewe, yaani bado mpo nyuma kweli kweli. Sasa ni hiyo USAID imekata misaada na hayo matundu ya vyoo yataadimika.
 
Nchi za Asia zimeweza kufanya mapinduzi kwa sababu wako serious mimi sijaona kama sisi tuko serious kama wao.
Ukitaka kujua hilo we tazama miradi yetu, mwendo kasi, sgr na hii ni miradi midogo.
Tazama mitaara yetu ya elimu. Unajua maendeleo sio miracles, ni planning.
Mfano china ilisomesha vijana wengi nje waliorudi kusukuma uchumi.
Kuna vitu kibao tunakabiliana navyo vidogo kwa kuvitazama lakini vinaturudisha nyuma. Umeme unakatika katika bila sababu za msingi wakati ni engine ya uchumi.
Kodi zisizo na miguu wala mikono yani serikali inataka inyonye watu wale wale tu. Naanzisha biashara leo natakiwa kulipa kodi wakati hata faida sijaipata bado.
Tuombe uzima ila bado mimi sijaona userious wa hili jambo.
Kweli kuna vitu havijazingatiwa:
Mfano:
Elimu,tumeendelea na mfumo kuwa na wanafunzi wanaomaliza shule wengi hawawezi kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza,wengine wamefaulu huku hawajui kusoma na kuandika.Mfumo wa "English medium" kwa shule za umma,ni kwa wachache,kama Taifa tumefanya unafiki,hatujadili,na wananchi hawapewi ukweli ni kwa nini Serikali inapata kigugumizi(kiu ya kila mwananchi ni kuwa nao wanataka watoto wao wasome shule za English medium),itasaidia kuwa nguvu yenye uwelewa na tayari kufanya kazi na wawekezaji wanaotajwa kuwa ndio kichochea cha ukuaji wa uchumi.

Kilimo,kama nchi tunalima kilimo cha kawaida ,nimefuatilia mazao ya biashara bado tunaachwa sana,tuangalie mfano zao la korosho,bado wakulima hawajawa wepesi kubadili miche mipya,miti ya mikorosho ni ya zamani bado Ivory Coast ametuzidi katika uzalishaji wa zao hili,Wizara husika wakajifunze Ivory Coast wanafanyeje na kufanikiwa katika kilimo hiki(wao kwa mwaka wanazalisha tani 970,000,sisi tunazalisha tani 400,000).
Zao la kahawa limekosa usimamizi,nchi zingine wanalima na kuendelea kuuza sisi zao wakulima wanalikimbia!

Tunakila aina nzuri ya hali ya hewa ya kuwezesha kulima mazao yenye thamani kubwa kama cocoa,vanilla n.k lakini Taarifa na ukweli haujadiliwi hata kwenye "vision 2050!!"

Barabara za kiwango cha lami kuunganisha Wilaya na Mikoa kasi imekuwa ni ndogo, na haizungumzwi kwenye vision 2050!

Kweli GDP zinazokadiriwa haziwezi kufikiwa kama mambo hayo ambayo tunayafanya kila mwaka hatuyaboreshi(Elimu,barabara,kilimo)
 
Ukiangalia South Africa ya Leo kwa Miundo mbinu ile na Maendleo yale kwa Nchi kama Tanzania kwa Miaka 25 iyajo ni Mingi Snaaaa kama Selikali ipo Seriously ikitaka inawezekana Bila Shida ila kwa Selikali hizi za Kifisadi Kufanya Vitu kusubili Uchaguzi ndio Wafanye Au Wafungue Mradi watasubili Sanaa maendeleo ya Kweli Hayataki Siasa Kidogo Alijaribu Magufuri ila wengine hawa Siasa ndio Shida,siasa kwa Nchi za Africa ndio Umaskini unaosababisha Nchi haiendlei
 
Masikini Tanzania bandari ya bagamoyo mafisadi waichukua
 
Attachments

  • 20250213_171101.jpg
    20250213_171101.jpg
    104.5 KB · Views: 2
Shida yetu ni kuishi kwenye dunia ambayo elimu kwetu ni mzaha.

Yaani kiongozi anaweza kwenda kwenye media na kujiropokea tu.

Kama uchumi wa Tanzania leo ni $85 million, ili kufikia $700 million katika muda miaka 25 ijayo. Kwa mantiki hiyo GDP growth inatakiwa roughly 10.5% annually kwa miaka 25 mfulululizo.

GDP growth itatokana na sector zipi, serikali wana dira ya miaka 25 na Kafulila nae anamipango yake PPP (huo uwekezaji wake huko vipi in line na dira ya taifa anajua mwenyewe).

Uchumi wa Tanzania leo unakuwa kwa kiwango cha chini ya 5% na sehemu kubwa ya ukuaji kwenye circular equation ni mikopo ya serikali na sehemu kubwa ya hela watu wamezitafuna (hazijaingia kwenye uchumi).

Achilia mbali ufisadi the mere fact uchumi unakuwa kwa 5% ina maana kuanzia mwaka ujao inabidi uwe unakuwa kwa 10.5% uoni kama hawa watu wanajiropokea tu.

Hata sijui uwa wanaongeaga vitu gani huko nchi zilizoendelea wakikutana na wataalamu wa kweli. Asilimia kubwa ukiwasikiliza wanapwaya sana hawa watu.
 
Nakumbuka 2000 wakati wa Mkapa walitoa projection ya maendeleo ya Tanzania kwa miaka 25 ijayo(2025), hopes were very high, promises were made, Tanzania would be the new Switzerland, ona sasa kiko wapi...hadi leo matundu ya vyoo ni mtihani mkubwa kwa watawala, matundu ya vyoo, can you imagine!!
Tutafikaje wakati Simbachawene ansema 60% ya watumishi wanalipwa lakini hawafanyi kazi
 
Ivi zile Noah tunapata lini? Ivi waliozaliwa baada ya lile tamko watapata mgao? To be fair wasipate, Ila waliokuwa hai wakati ule na sasa wamefariki bila kupata wanastahili kupata kupitia wasimamizi wa mirathi
 
View attachment 3199594
===
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Ubia nchi Tanzània PPPC Mhe David Kafulila amewaeleza Watanzania kuwa lazima wafahamu kesho ya Tanzània lao ni bora sana kama tu hali ya Umoja na mshikamamo itaendelea kuwa ilivyo leo.

David Kafulila anasema, Tanzania kwa kushirikiana na sekta binafsi ( PPP) ya ndani au nje ya Tanzania wataipeleka kwa Kasi Tanzania kwenye Uchumi wa viwango vya juu kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo kwa miaka 25 ijayo ( 2025-2050 )

Mtakumbuka, David Kafulila amekuwa ni Mtendaji na mwanasiasa anayejikita zaidi kwenye kutetea hoja za Serikali yake kwa namba na "fact" zenye kueleweka na watu wa Kada zote kitu kinachomfanya awe ni Mtendaji wa Serikali anayefuatiliwa zaidi mitandaoni kwa sasa.

Mkurugenzi Mtendaji huyu anasema Tanzània mpaka kufikia mwaka 2050 inatarajia kujenga Uchumi wa $700bn ambao ni karibu mara mbili ya Uchumi wote wa Africa ya Kusini ya leo ambayo Leo ni karibu $380bn.

Kafulila anasema si kazi rahisi kujenga Uchumi wa $700bn kutoka Uchumi wa sasa wa Tanzania wa $85bn kazi ambayo kamwe haiwezi ikatekelezwa kwa Kodi na Mikopo pekee hivyo sekta binafsi haepukiki kwenye safari hii ya ujenzi wa Uchumi mkubwa kwa kipindi kifupi cha miaka 25.

Mkurugenzi Mtendaji huyu anaendelea kwa kusema jambo hili linawezekana bila mashaka yoyote kwani hata nchi ya Vietnam mwaka 1990 ilikuwa na Uchumi wa $6.4bn lakini leo Vietnam wana Uchumi wa zaidi ya $460bn karibu mara themanini (X 80) zaidi.

Kama hivyo ndivyo kwanini Tanzania tusiweze Vietnam wao Wana nini?

View attachment 3196797

====
Ingawa mchanganuo wake umekaa kinadharia sana lakini kauli yake inaleta morali
 
Nakumbuka 2000 wakati wa Mkapa walitoa projection ya maendeleo ya Tanzania kwa miaka 25 ijayo(2025), hopes were very high, promises were made, Tanzania would be the new Switzerland, ona sasa kiko wapi...hadi leo matundu ya vyoo ni mtihani mkubwa kwa watawala, matundu ya vyoo, can you imagine!!
Ukitaka kuelewa hii vizuri nenda kaipitie Ile Dira ya 2000
 
Back
Top Bottom