Johnpaulthesecond
JF-Expert Member
- Apr 27, 2024
- 503
- 480
==
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila amewataka Watanzania waache kutishwa na watu wanaosema kupanda au kushuka Kwa shilling ya Tanzania kunaashiria Uchumi wa Tanzania kuwa legelege.
Bwana Kafulila amesema Uchumi wa nchi yoyote Ile duniani ni kapu kubwa lililojaa vitu vingi na halipimwi kwa Parameter/nyanja moja tu ya UIAMARA WA SARAFU kwani kama tukiangalia Uimara wa safaru hata hiyo dola ya Marekani haifanyi vizuri kwenye soko la fedha la Dunia kwani inashika nafasi ya kumi (10).
Kafulila anaendelea kwa kusema pamoja na kwamba dola ya Marekani inashika nafasi ya 10 lakini Marekani ndio anashikilia asilimia 25 ya Uchumi wote wa dunia Kwa lugha nyingine kama sarafu ni kigezo pekee basi dola ya Marekani ilipaswa kuwa ni namba moja (1) na sio namba kumi (10) kama ilivyo leo.
David Kafulila anasema uchumi wa Tanzania umekua karibu mara saba (7) kutoka US$13 bilioni mwaka 2000 mpaka US$85bilioni mwaka 2025 hapa lazima CCM ipongezwe tu.
Kafulila anaonesha uakisi wa Mpango wa maendeleo wa miaka 25 ijayo ulioandaliwa na awamu ya sita (6) ya Rais Samia yaani 2025-2050 ambapo Tanzania inatarajia kufikia uchumi wa US$700bn ambao nao ni karibu mara saba (7) ya Uchumi wa sasa.