David Kafulila: Msitishike na kupanda au kushuka kwa shilling hata dola ya Marekani ni sarafu ya 10 lakini Marekani ndio kinara wa uchumi wa dunia

David Kafulila: Msitishike na kupanda au kushuka kwa shilling hata dola ya Marekani ni sarafu ya 10 lakini Marekani ndio kinara wa uchumi wa dunia

Shida yetu kubwa ni kwamba hatuna uwiano mzuri wa export na import, ndio maana Uchumi wetu na sarafu vinashuka mno, import ni kubwa sana kiasi kwamba we need foreign currency more ili tuweze kuagiza vitu ndo maana sarafu yetu ipo too weak
Ni kweli hata Kafulila hajakataa ila hoja hapa hatupashawi kusema eti uchumi wa Tanzania haujui kisa stability ya currently,

Nadhani ndicho anachomaanisha Mkogwe Kafulila
 
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha ubia nchini Tanzania PPPC Bwana David Kafulila amewataka Watanzania waache kutishwa na watu wanaosema kupanda au kushuka Kwa shilling ya Tanzania kunaashiria Uchumi wa Tanzania kuwa legelege.

Bwana Kafulila amesema Uchumi wa nchi yoyote Ile duniani ni kapu kubwa lililojaa vitu vingi na halipimwi kwa Parameter/nyanja moja tu ya UIAMARA WA SARAFU kwani kama tukiangalia Uimara wa safaru hata hiyo dola ya Marekani haifanyi vizuri kwenye soko la fedha la Dunia kwani inashika nafasi ya kumi (10).

Kafulila anaendelea kwa kusema pamoja na kwamba dola ya Marekani inashika nafasi ya 10 lakini Marekani ndio anashikilia asilimia 25 ya Uchumi wote wa dunia Kwa lugha nyingine kama sarafu ni kigenzo pekee basi dola ya Marekani ilipashwa kuwa ni namba moja (1) na sio namba kumi (10) kama ilivyo leo.

David Kafulila anasema uchumi wa Tanzania umekua karibu mara saba (7) kutoka US$13 bilioni mwaka 2000 mpaka US$85bilioni mwaka 2025 hapa lazima CCM ipongezwe tu.

Kafulila anaonesha uakisi wa Mpango wa maendeleo wa miaka 25 ijayo ulioandaliwa na awamu ya sita (6) ya Rais Samia yaani 2025-2050 ambapo Tanzania inatarajia kufikia uchumi wa US$700bn ambao nao ni karibu mara saba (7) ya Uchumi wa sasa.
Kapulila kumbe ndiye gavana wa bot?
 
Huyu ana matatizo makubwa sana tena sana..., (siamini kama hana uelewa bali amegeuka kuwa dalali mpindisha ukweli ili mradi tu apitishe hoja zake)

Moja kuwa na sarafu yenye thamani haimaanishi ndio jambo zuri, sababu unaweza ukawa unauza zaidi kwahio sarafu yenye thamani kwako ikawa ni hasara (refer China)

Mbili sisi ambao ni tegemezi na tunatumia dollar kununua kila kitu kupanda kwa dola dhidi ya pesa yetu ni hasara kubwa sababu vitu vitapanda au kwa maana nyingine ile nguvu kazi tunayofanya ili tulipwe shilingi ili tukabadilishe tupate dollar itabidi tuifanye kwa ziada kupata kiasi kile kile kama dollar ingekuwa chini

Tatu USA dollar ndio faida yake sababu anachapisha madollar nyie dunia mnayanunua hivyo ni kama mnampatia mkopo wa bei nafuu


Mwisho kabisa nilishasema hizi story za hata USA anafanya ni being naive...

 
Kafulila afanye kazi kwa utulivu. Ajifunze kutoka kwa Profesa Elisante Ile Gabriel.
 
Huyu ana matatizo makubwa sana tena sana..., (siamini kama hana uelewa bali amegeuka kuwa dalali mpindisha ukweli ili mradi tu apitishe hoja zake)

Moja kuwa na sarafu yenye thamani haimaanishi ndio jambo zuri, sababu unaweza ukawa unauza zaidi kwahio sarafu yenye thamani kwako ikawa ni hasara (refer China)

Mbili sisi ambao ni tegemezi na tunatumia dollar kununua kila kitu kupanda kwa dola dhidi ya pesa yetu ni hasara kubwa sababu vitu vitapanda au kwa maana nyingine ile nguvu kazi tunayofanya ili tulipwe shilingi ili tukabadilishe tupate dollar itabidi tuifanye kwa ziada kupata kiasi kile kile kama dollar ingekuwa chini

Tatu USA dollar ndio faida yake sababu anachapisha madollar nyie dunia mnayanunua hivyo ni kama mnampatia mkopo wa bei nafuu


Mwisho kabisa nilishasema hizi story za hata USA anafanya ni being naive...

Nikimsikiliza Kafulila haya yote uliyoyaandika hajayakataa,

ila amekataa uwianishaji wa uimara wa sarafu yetu na uimara wa uchumi wetu,

Currency Stability sio kigezo Cha mwisho cha uimara wa uchumi wa nchi,

👆👆👆
Nadhani ndivyo alivyomaanisha
 
Huyu Bwana awe anakaa kimya wakati mwingine

Hivi hajui athari za kupanda Kwa Thamani ya dollar dhidi ya shilingi za Tanzania?

Kama ulikuwa unaagiza gari nje ya Nchi Kwa Dollar 5,000 Mwaka 2023 ambapo Thamani ya shilingi yetu ilikuwa ni 2,085 dhidi ya dollar 1

Ina maana ulitakiwa kuwa na shilingi 10,425,000 kuweza kuagiza

Kwasasa kwa Thamani ya shilingi 2,700 dhidi ya dollar 1

Inaonesha unatakiwa kuwa na shilingi 13,500,000 kuweza kuagiza gari ile ile

Ni utofauti wa shilingi 3,075,000 ni zaidi ya ongezeko la asilimia 29.5 🙌

Halafu mtaalamu wetu wa Uchumi Bwana Kafulila haoni utofauti yaani🙌

Hii Nchi inaongozwa na watu wasiojua namna ya kutupambania Wananchi wao hakika
Msikilize vizuri nimekuwekea video
 
Ni kweli hata Kafulila hajakataa ila hoja hapa hatupashawi kusema eti uchumi wa Tanzania haujui kisa stability ya currently,

Nadhani ndicho anachomaanisha Mkogwe Kafulila
Kafulila anawasafisha mno watawala badala ya kuwaambia uhalisia
 
Kafulila anaongea kama yupo peponi, huyu mtu anajua uchumi wa wapi? Kashiba mahindi, nachoona kazi yake anasifia sifia tu, economy is what is on the ground, to citizens, shilingi kushuka ni dalili moja wapo ya uchumi kutoenda vema, mbona kama Kafulila anawaona watu wote vilaza.
Mkuu kwenye group pesa ipo itafute tu
 
Tusitishike vipi kama tunaagiza kutoka nje mpaka viberiti vile vya njiti?? Hawa wasomi wetu wanatia shaka sana na elimu zao
 
Huyu naye, export yetu ni ndogo sana huku import ikiwa ni kubwa sana kutokana na uhaba wa viwanda vidogo vidogo, hili ndo tatizo kubwa la nchi yetu na asitudanganye kuwa Uchumi wetu utafika USD 700 billion within 25 years, Uchumi unaelekea kuwa stagnant Sasa, aache kuwapamba viongozi na awaambie ukweli wa njia ya kurekebisha Uchumi, najua maisha ni magumu sana mtaani hivyo mara nyingi mtu ukipata nafasi huko juu lazima ujifanye kipofu ili kuwapamba watawala which is wrong
Ni kweli hapa kinachotuimoza ni swala la importation ni kubwa zaidi ya exportation Kwamaana tunaimport vitu vingi Sana hasa final products ambazo zingewezwa kuzalishwa apa na viwanda vidogo vidogo vyenye kutokana na mfumo wa Sido..lkn ndo kwanza Sido yenyewe Haina uhai nchini ni km imekufa...chepua ni VETA tunaisahau Sido ambaye angekuwa mkombozi wa viwanda vidogo vidogo..
Bidhaa nyingi Sana zinatoka china na Kenya Kwa ukanda wetu apa Afrika mashariki sie tumebaki na siasa za majitaka.
 
Huyu Bwana awe anakaa kimya wakati mwingine

Hivi hajui athari za kupanda Kwa Thamani ya dollar dhidi ya shilingi za Tanzania?

Kama ulikuwa unaagiza gari nje ya Nchi Kwa Dollar 5,000 Mwaka 2023 ambapo Thamani ya shilingi yetu ilikuwa ni 2,085 dhidi ya dollar 1

Ina maana ulitakiwa kuwa na shilingi 10,425,000 kuweza kuagiza

Kwasasa kwa Thamani ya shilingi 2,700 dhidi ya dollar 1

Inaonesha unatakiwa kuwa na shilingi 13,500,000 kuweza kuagiza gari ile ile

Ni utofauti wa shilingi 3,075,000 ni zaidi ya ongezeko la asilimia 29.5 🙌

Halafu mtaalamu wetu wa Uchumi Bwana Kafulila haoni utofauti yaani🙌

Hii Nchi inaongozwa na watu wasiojua namna ya kutupambania Wananchi wao hakika
Na hiyo kodi kubwa ya TRA ilivyowekwaga kubwa ya 50% ya thamani ya gari huwa ni kwa kumnufaisha nani na inaulazima gani?

Sijawahi kusikia mbunge hata mmoja akichallenge Bungeni hizi kodi na tozo za kisengerenyuma zinavyoumiza waTz ziondoshwe ili watu waishi maisha ya furaha!
 
Ni kweli hapa kinachotuimoza ni swala la importation ni kubwa zaidi ya exportation Kwamaana tunaimport vitu vingi Sana hasa final products ambazo zingewezwa kuzalishwa apa na viwanda vidogo vidogo vyenye kutokana na mfumo wa Sido..lkn ndo kwanza Sido yenyewe Haina uhai nchini ni km imekufa...chepua ni VETA tunaisahau Sido ambaye angekuwa mkombozi wa viwanda vidogo vidogo..
Bidhaa nyingi Sana zinatoka china na Kenya Kwa ukanda wetu apa Afrika mashariki sie tumebaki na siasa za majitaka.
Kweli kabisa, alafu anatokea mtu huko ameshiba kiyoyozi anaanza kusifia na kutetea pasipofaa ili tu apandishwe cheo
 
Back
Top Bottom