David Kafulila ni hazina kwa Taifa letu, anapaswa kutumiwa vyema kwa maslahi mapana ya nchi

David Kafulila ni hazina kwa Taifa letu, anapaswa kutumiwa vyema kwa maslahi mapana ya nchi

Sina Cha kuongeza ila Kafulila katika Siasa zake kapitia mapito magumu sana.

Tangu enzi za BAVICHA
Tangu enzi za Escrow
Tangu enzi za Mbatia

Niwakumbushe kidogo,
Katika Uchaguzi wa BAVICHA Ulikuwa na ushindani mkubwa kuwahi kushuhudiwa kati ya Heche na Kafulila,
Kafulila akashinda Uchaguzi ile kwa tofauti kubwa sana ya kura Mbowe akamwambia Dk Slaa afute Uchaguzi ule.😭

Kafulila akakasirika akajiunga na NCCR ya Mbati na baadae kuwa Mbunge wa Kigoma Kask.

Baadae ndio akaibuka na kashfa ya Escrow then Wazee wa Escrow wakamfuta Kafulila na zaidi ya 2bl alipogoma wakacheza na Mbatia ili amfukuze Uanachama Mbatia akamfukuza Kafulila Uanachama 😭

Tanzania Kama kunamwanasiasa kapambana sana basi ni David Kafulila.

Tatizo lake kubwa ni Uzalendo na Uadilifu na Kuichukia rushwa kwa Maneno na Matendo.
Mheshimiwa Kafulila amepitia Mambo magumu sana na majaribu makubwa sana . lakini cha kutia moyo ni kuwa bado Mheshimiwa Kafulila ameendelea kusimama imara na kwa uzalendo wake mkubwa pasipo kusaliti misingi yake ya kusimamia ukweli.
 
Wewe kwenye siasa hizi umezijulia kipindi hiki cha awamu ya sita,hujui historia ya vyama vingi,wewe umejikita kusifia sifia ili upate mkate wako wa siku.
Ningependa kukwambia kuwa mimi nimeanza siasa muda mrefu sana na naifahamu vyema siasa ya nchi hii na historia yake. Hata hapa JF nimekuwa mfuatiliaji wa muda mrefu sana tangia mwaka 2013 japo nimekuja kujiunga 2022. Kwa hiyo mijadala yote iliyokuwa ikiendeshwa na aina mzee mwanakijiji mimi nilikuwepo hapa nafuatilia. Mama Tibaijuka anajiunga JF 2014 mimi nilikuwepo hapa nafuatilia . Kwa hiyo usinichukulie poapoa.
 
Sina Cha kuongeza ila Kafulila katika Siasa zake kapitia mapito magumu sana.

Tangu enzi za BAVICHA
Tangu enzi za Escrow
Tangu enzi za Mbatia

Niwakumbushe kidogo,
Katika Uchaguzi wa BAVICHA Ulikuwa na ushindani mkubwa kuwahi kushuhudiwa kati ya Heche na Kafulila,
Kafulila akashinda Uchaguzi ile kwa tofauti kubwa sana ya kura Mbowe akamwambia Dk Slaa afute Uchaguzi ule.😭

Kafulila akakasirika akajiunga na NCCR ya Mbati na baadae kuwa Mbunge wa Kigoma Kask.

Baadae ndio akaibuka na kashfa ya Escrow then Wazee wa Escrow wakamfuta Kafulila na zaidi ya 2bl alipogoma wakacheza na Mbatia ili amfukuze Uanachama Mbatia akamfukuza Kafulila Uanachama 😭

Tanzania Kama kunamwanasiasa kapambana sana basi ni David Kafulila.

Tatizo lake kubwa ni Uzalendo na Uadilifu na Kuichukia rushwa kwa Maneno na Matendo.
Nimelia aisee hii.😭😭😭😭
 
Ningependa kukwambia kuwa mimi nimeanza siasa muda mrefu sana na naifahamu vyema siasa ya nchi hii na historia yake. Hata hapa JF nimekuwa mfuatiliaji wa muda mrefu sana tangia mwaka 2013 japo nimekuja kujiunga 2022. Kwa hiyo mijadala yote iliyokuwa ikiendeshwa na aina mzee mwanakijiji mimi nilikuwepo hapa nafuatilia. Mama Tibaijuka anajiunga JF 2014 mimi nilikuwepo hapa nafuatilia . Kwa hiyo usinichukulie poapoa.
Siyo nakuchukulia poa ila aina ya michango yako inakuchora hivyo,au ndiyo ushabiki wako umekupofusha huoni kitu chochote zaidi ya kile unachopenda wewe vingine vyote kwako ni hakuna.
 
Siyo nakuchukulia poa ila aina ya michango yako inakuchora hivyo,au ndiyo ushabiki wako umekupofusha huoni kitu chochote zaidi ya kile unachopenda wewe vingine vyote kwako ni hakuna.
Sasa watu kama CHADEMA unaona wana hoja gani zaidi ya hoja za ubaguzi na chuki tu?
 
Upofu wako umeona ubaguzi. Nikikuambia ufafanue wamembagua nani unajaza kurasa kueleza upotoshaji wako. Uzushi huu uongo na upotoshaji wako unaishia humu humu.
Kwaninhukuzisikia kauli chafu za kibuguzi zilizokuwa zinatolewa na Lissu? Au wewe ni kiziwi husikia chochote kile.
 
Acha kupotosha wewe na akili yako hiyo ya kushindwa kuelewa mambo katika uhalisia wake.
Wewe ndiye huelewi kitu. Kero za muungano zitokanazo na muundo wa muungano zinalalamikiwa na wananchi wa pande zote za muungano kila zikizungumzwa wahafidhina wa CCM wasema ni ubaguzi. Kufumbia macho kero hizi ndiyo kifo cha huu muungano. Wewe umekariri tu sikulaumu.
 
Endelea tu na unoko,uzushi na uongo wako hapo😃😃😃 . CHADEMA mmechoka sana na kuvurugwa akili zenu. Mmejaa msongo wa mawazo muda wote😃😃😃.mkisikia jina la Kafulila mnabaki mnatetemeka utafikiri wagonjwa wa homa kali.
Kafulila tumemkuza kwako wewe ni kiumbe kipya CHAMA chenu kinaongoza inchi na Bado mnashindia kahawa Lumumba je mngekua Wana Chadema kama Mimi sijui tungewakuta wapi jikomboe kijana kwanini ukubali kutimia vibaya mwili wako kisa njaa ndogo ndogo
 
Mheshimiwa David Kafulila Ni mzalendo wa kweli .ndio maana unaona anazungumzwa na watu wengi sana kumtia moyo.

Kafanya nini kumfanya awe Mzalendo wa kweli .... Alipokuwa upande wa pili alikuwa TUMBIRI .... Leo ni Mzalendo wa kweli. Mnafurahisha sana.
 
Kafanya nini kumfanya awe Mzalendo wa kweli .... Alipokuwa upande wa pili alikuwa TUMBIRI .... Leo ni Mzalendo wa kweli. Mnafurahisha sana.
Mheshimiwa Kafulila hajawahi kubadilika wala kusaliti misimamo yake. Ni yeye yule yule Kafulila wa wakati wote na muda wote.kwake spedi ni spedi na wala siyo kijiko kikubwa.
 
Kafulila tumemkuza kwako wewe ni kiumbe kipya CHAMA chenu kinaongoza inchi na Bado mnashindia kahawa Lumumba je mngekua Wana Chadema kama Mimi sijui tungewakuta wapi jikomboe kijana kwanini ukubali kutimia vibaya mwili wako kisa njaa ndogo ndogo
😃😃😃Hujawahi kuwa na akili hata siku moja wewe. Nani kakwambia nipo Lumumba kushindia kahawa😃😃. Hivi bado mnabugia viroba
 
Mheshimiwa Kafulila hajawahi kubadilika wala kusaliti misimamo yake. Ni yeye yule yule Kafulila wa wakati wote na muda wote.kwake spedi ni spedi na wala siyo kijiko kikubwa.

Sijasema amebadilika. Ni nyie maCCM. Alipokuwa upande mwingine mkamwita Tumbiri... Leo yuko kwenu anakuwa jembe. Anyway, mimi namfahamu vizuri tena kwa karibu kuliko wewe.
 
Sijasema amebadilika. Ni nyie maCCM. Alipokuwa upande mwingine mkamwita Tumbiri... Leo yuko kwenu anakuwa jembe. Anyway, mimi namfahamu vizuri tena kwa karibu kuliko wewe.
Kama unamfahamu usisite kumuelezea ili na sisi tumfahamu zaidi
 
Sijasema amebadilika. Ni nyie maCCM. Alipokuwa upande mwingine mkamwita Tumbiri... Leo yuko kwenu anakuwa jembe. Anyway, mimi namfahamu vizuri tena kwa karibu kuliko wewe.
Mheshimiwa Kafulila Anafahamika na Taifa zima kuwa ni mzalendo asiye tiliwa mashaka. Ni mtu aliyenyooka kama rula .
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeendelea kumfuatilia na kufuatilia mahojiano mbalimbali ambayo amekuwa akifanya na ambayo amefanya kupitia vyombo vya habari kuelezea mambo mbalimbali kuanzia uchumi,uwekezaji,biashara na mengine mengi. kila mtu pasipo kujali itikadi yake ya Kiasia au chama chake anakili kuwa Mheshimiwa David Kafulila Ni Hazina kubwa kwa Taifa letu na anapaswa kutumiwa vyema kwa maslahi mapana kwa Taifa letu.

Nimeona namna anavyoitetea na kuisemea vyema serikali yetu chini ya Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa ufasaha ,hoja ,takwimu na ushahidi wa kiutafiti na wa ukweli. Anaeleza kwa lugha nyepesi ambayo watu wanamuelewa vyema sana huku mitaani na kuielewa vyema sana serikali yetu kupitia ufafanuzi wake anao utoa.

Anaeleza kwa utulivu,upole na unyenyekevu mkubwa sana. Angalia namna alivyoelezea juu ya Deni la Taifa,ongezeko la watalii hapa nchini ,suala la ajira na ukuaji wa uchumi wetu. Akaeleza kuwa pamoja na kwamba watu wanasema Deni limekuwa lakini uchumi wetu umekuwa zaidi ndani ya Muda mfupi wa Rais Samia kutoka Dolla Billioni 66 mpaka Dolla Billion 85. Akaeleza pia kuwa kukopa siyo dhambi bali inategemea unakopa kwa ajili ya nini.akasema kama unakopa kwa ajili ya kulipa mishahara hapo ndio inakuwa tatizo.

Mheshimiwa Kafulila amekuwa mtetezi mkubwa sana wa Rais Samia na serikali yake kupitia vyombo vya habari na mitandao. Anaifanya kazi hiyo kwa weledi na uzalendo mkubwa sana.anawafumbua macho watu wengi sana ambao wengi walikuwa wamepofushwa akili na macho na upotoshaji wa baadhi ya watu wenye nia mbaya na chuki binafsi na Mheshimiwa Rais na Serikali yake.

Mheshimiwa David Kafulila amefanikiwa kwa hoja nzito na kwa lugha rahisi na kwa takwimu kuzizima na kuzisambaratisha kabisa kama mvuke hoja za upinzani walizokuwa wanazitumia kupotosha wananchi hususan wale wasio na uelewa wa baadhi ya mambo hususani ya kiuchumi.

Mheshimiwa David Kafulila mbali na usomi wake mkubwa lakini unamuona ni mtu mnyenyekevu na mzalendo wa kweli kwa Taifa letu. Ni mtu na kiongozi aliye nyooka kama rula. Hanaga kupinda pinda. Ni mtu ambaye kwake nyeupe ni nyeupe na nyeusi ni nyeusi. Hata umshambulie kwa lugha kali utaona yeye amebakia katika utulivu na kujibu kwa hoja. Katika hili mnaweza kurejea mapambano ya hoja bungeni wakati wa sakata la Escrow namna alivyokuwa mtulivu katika kutoa hoja na kutetea hoja zake.

Mheshimiwa David Kafulila Ni chuma na kiongoz anayekubalika kwa hoja zake na watu wa vyama vyote iwe upinzani na ndani ya chama chetu cha CCM.kwa sababu yeye wakati wote husimama katika hoja na kuitetea hoja kwa takwimu.

Mheshimiwa Rais Aendelee kumtumia Mheshimiwa Kafulila kwa sababu ana mapenzi mema na Taifa letu na ni mzalendo na amekuwa mtetezi wake kwa yote ayafanyayo. wakati unakuta wengine wamejikausha tu pale serikali inaposhambuliwa kwa hoja za upotoshaji. Mheshimiwa Kafulila amekataa kabisa kivitendo kukaa kimya pale anapoona kuna watu wanapotosha mambo kwa lengo la kuichongaisha serikali na wananchi au kuifanya serikali ichukiwe na wananchi.amekuwa akitoka hadharani na kujibu mapigo kwa hoja na takwimu na kusambaratisha kabisa mijadala ya kiuopotoshaji.

Mheshimiwa David Kafulila Ni Hazina kwa Taifa letu tunayepaswa kumtumia kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Ni mtu safi, mzalendo na mchapa kazi kwelikweli. Ndio maana huwezi ukamkuta na doa la rushwa au ufisadi au matumizi mabaya ya madaraka katika maeneo mbalimbali aliyoitumikia Taifa letu. Zaidi utakuta alama njema za kiutendaji alizoziacha katika maeneo aliyopita na kukumbukwa kwa uchapakazi wake ulioleta matokeo chanya.

Watanzania tunapaswa kuwatia moyo na kuwaunga mkono wazalendo aina ya Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan na David Kafulila. Tukikaa kimya tukaacha wakashambuliwa na wenye maslahi yao binafsi tutakuwa tunawakatisha tamaa na kuwapa ushindi mafisadi na wenye kulinyonya Taifa letu kwa mirija.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Huyu hakika ni Mzalendo wa kweli Asante sana Lucas Mwashambwa
 
Back
Top Bottom