David Kafulila: Shirika la ndege ATCL chini ya Rais Samia halijawahi kuleta hasara za kiuchumi ila za kihasibu tu

Tuwekeee financial statements za shirika zilizokaguliwa na CAG halafu tuamue wenyewe kama ni accounting profit/loss au ni Economic profit/loss.
 
Kafulila aache porojo. ATC ipate hasara kiuhasibu (kifedha) halafu isiwe na effect kiuchumi!? Hakuna uhasibu bila fedha na wala uchumi hauwezi kuwa mzuri bila fedha. Hao watalii wataimarishaje uchumi ikuwa hela wanayotoa badala ya kujenga miundombinu inayo weka mazingira mazuri ya uwekezaji inaenda kufidia hasara ya kiuhasibu iliyotokea ATC ili shirika hilo lisife.
 
Hata wakati Magufuli yupo madarakani ATCL lilikuwa halipati hasara ila alivyoondoka CAG akafumua kwenye Mshono ,hata kipindi hichi cha Hangaya alipati hasara tutakuja kujua akishaondoka madarakani..
 
Unaweza kutukana matusi ya dunia nzima
 
Watalii wenyewe wanakuja na kuondoka na Emirates Air au Ethiopian Air.
 
Kafulila yupo njema sana kwenye ujenzi wa hoja. Uzi wa aina hii wachangiaji wanakuwa wachache wengi wapo kule kwa yule kasuku Polepole na wengine wanamsoma Mange, tunapenda mambo mepesi mepesi yasiyoumiza vichwa vyetu.
 
Wewe mpuuzi tu jikite kwenye hoja na mantiki inayozungumzwa punguza kushabikia udaku unakuongezea chuki kichwani mwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…