David Kafulila: Shirika la ndege ATCL chini ya Rais Samia halijawahi kuleta hasara za kiuchumi ila za kihasibu tu

Kwa hiyo ndg za ATCL zisingekuwepo hawa Watalii wasingekuja Tanzania?
 
View attachment 3461458
Dar es salaaam, Akiongea mbele ya wachambuzi wa habari na uchumi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Nchini (PPPC), Bw. David Kafulila amesema moja ya sekta inayofanya nchi ikue kiuchumi ni pamoja na Rasilimali za nchi.

Aidha, Kafulila alisema kuwa mbali na maji, Awamu ya Sita imefanya makubwa katika sekta ya utalii, hasa upande wa watalii wa ndani, na hili limekuwa chachu ya ukuaji wa mapato ya Taifa. Ongezeko kubwa la mapato linaonesha wazi kuwa ubora wa vivutio na huduma za utalii nchini umeimarika.

Mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita,
​
  • Watalii wameongezeka kutoka milioni 1.4 mwaka 2020 hadi zaidi ya milioni 5.3 mwaka 2024.​
  • Mapato ya utalii wa nje yameongezeka kutoka dola milioni 700 hadi dola bilioni 3.9 (zaidi ya Sh. trilioni 10).​
  • Mapato ya utalii wa ndani yameongezeka kutoka Sh. bilioni 46.3 hadi bilioni 209.8.​
Kuhusu mjadala wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kafulila alifafanua kuwa kuna tofauti kati ya accounting loss (hasara ya kihasibu) na economic loss/profit (faida au hasara halisi ya kiuchumi).

Kwa mujibu wake, hata kama kihasibu ATCL inaonekana kupata hasara, ndege zake zimekuwa zikileta maelfu ya watalii walioliletea Taifa faida ya zaidi ya dola bilioni 3.9. Hii ni faida ya kiuchumi kubwa mno kuliko hasara ndogo ya kimaandishi inayotajwa na CAG.

​
Wewe Kafulila akili yako siyo sahihi, tuna watu wa ovyo sana nchi hii. unaongea uongo na unajua wazi kuwa unadanganya. Ndiyo maana yule jamaa alimwita lile jina baya.
 
Kafulila alisomea nini?
Kwanini wanawapa ma fomfoo kazi za kutumia akili nyingi?
Huyu si kama bajaji au mshamba fulani bungeni mwenye kelele nyingi.
Kwa akili hii unategemea mke wako hatakuacha?
Hata uwe na pesa kama huna akili ya kupambanua mambo tegemea kuachwa na mke.
 
Ndio watalii wanakuja kuangalia shirika la ndege la taifa linavyoendeshwa kwa hasara lakini bado linaendelea kuwepo kwa gharama za walipa Kodi. Huu nap kwa Tanzania ni utalii tosha. Wengi wa watalii wanakuja na ndege za mashirika mengi kuja kulitalii shirika letu la ndege.
 
View attachment 3461458
Dar es salaaam, Akiongea mbele ya wachambuzi wa habari na uchumi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Nchini (PPPC), Bw. David Kafulila amesema moja ya sekta inayofanya nchi ikue kiuchumi ni pamoja na Rasilimali za nchi.

Aidha, Kafulila alisema kuwa mbali na maji, Awamu ya Sita imefanya makubwa katika sekta ya utalii, hasa upande wa watalii wa ndani, na hili limekuwa chachu ya ukuaji wa mapato ya Taifa. Ongezeko kubwa la mapato linaonesha wazi kuwa ubora wa vivutio na huduma za utalii nchini umeimarika.

Mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita,
​
  • Watalii wameongezeka kutoka milioni 1.4 mwaka 2020 hadi zaidi ya milioni 5.3 mwaka 2024.​
  • Mapato ya utalii wa nje yameongezeka kutoka dola milioni 700 hadi dola bilioni 3.9 (zaidi ya Sh. trilioni 10).​
  • Mapato ya utalii wa ndani yameongezeka kutoka Sh. bilioni 46.3 hadi bilioni 209.8.​
Kuhusu mjadala wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kafulila alifafanua kuwa kuna tofauti kati ya accounting loss (hasara ya kihasibu) na economic loss/profit (faida au hasara halisi ya kiuchumi).

Kwa mujibu wake, hata kama kihasibu ATCL inaonekana kupata hasara, ndege zake zimekuwa zikileta maelfu ya watalii walioliletea Taifa faida ya zaidi ya dola bilioni 3.9. Hii ni faida ya kiuchumi kubwa mno kuliko hasara ndogo ya kimaandishi inayotajwa na CAG.

​
Hivi kuna "hasara" ambayo siyo "hasara" ?
 
Hawa ndio walituambia, deni tuliangalie kwa Dolla, kwa Tzs linakuwa kubwa!!
 
Kwa hiyo hasara ikiwa ya kihasibu inageuka kuwa faida?.

Habari kama hizi ziwe zinaishia TBC huko.
 
Back
Top Bottom