David Kafulila: Taarifa zinaonesha umasikini wa bara la Afrika ulipaa zaidi wakati ambapo misaada ya wahisani ilikuwa juu zaidi

YAY

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2024
Posts
362
Reaction score
381

==
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila katika ukurasa wake wa X zamani tweeter ameandika haya;-

Kati ya mwaka 1970 na mwaka 1998 wakati misaada toka nje ya Africa ilikuwa ya kiwango cha Juu kuliko wakati wowote ajabu ni katika wakati huo huo umasikini wa bara la Africa ulipaa zaidi na kufikia 66% kutoka 11% kabla ya misaada hiyo ambayo leo Rais wa Marekani Donald Trump ameanza kuipunguza tena.

Mkurugenzi huyo anafafanua zaidi,

Umasikini wa bara la Afrika ulipaa au ulikua zaidi hadi kufikia kilele cha asilimia 66 kutoka asilimia 11 tu baada ya wahisani kuongeza misaada yao kwa bara la Afrika.​


===
Lugha nyepesi ya utafiti huu tunasema, Kadiri Wazungu wanavyoisaidia Africa ndio umasikini wa bara la Africa unavyoongezeka hivyo uamuzi wowote wa Donald Trump usiwatetemeshe Wala kuwateteresha Waafrica
===


Baada ya comment hii ya David Kafulila nimejiuliza maswali kadhaa ikiwa Rais Donald Trump wa Marekani kupunguza kwake misaada ya Marekani (USAID ) kwa bara la Africa Je, kutachochea zaidi kukua kwa Uchumi wa bara la Africa wakati huu kwa kutumia PPP kama ilivyokuwa kabla ya miaka ya 1970 au kinyume chake?

"Wakati mwingine kumpiga chura teke ni sawa tu na kumwongezea mwendo"





===
 
What is he doing now?
Same same?

Wakati waafrika kwa kipindi chote cha miaka zaid ya 15 baada ya uhuru waliachiwa resources na Agricultural products processing industries...

Wakaanza kuziua kwa kukabidhi washkaji zao waliopigania uhuru,

Fast forward viwanda vingi vikageuka ma godown...

Wajanja kama Kenya wakawaacha wakoloni wa kuviendeleza.., lakini wakawa na wao kama nchi hawanufaiki navyo.. vimekuwa maduka ya wanasiasa..

Nchi nyingine zikarudisha wakoloni baadae kwa njia za uwekezaji...

Kwenye mashamba na viwanda wakapewa bei za bure, wakajiingiza kwenye mikopo mkubwa wakatumia rasili mali zetu kama dhamana..

Wakaachana na production wakaenda kwenye trading.... 🤔.

Mikopo Africa wala haitusiaidii wananchi, mara nying almost 40% n itechnology and admin costs ambazo zinarud kwako... The other 60% ni Warsha na Makongomano...

We can live and stretch without hizo aid, lakini tusiwe na kibri kama cha mika flani hapa tukawambia....

Kazi za kufanya ni kuendeleza kilimo na bidii kwenye elimu ya Ufundi..

Diplomacy iendelee na tuikazanie huku tukipambana kuondokana. Na misaada kwa kias kikubwa..

Btw.. pesa za matumiz ya kawaida ndio hubeba 80% ya Bajeti... Tukijibana tunaweza.
 

Trump ni "mpango wa Mwenyezi Mungu"....

Confessions of an Economic Hitman- John Perkins .

Trump has opened up a Pandora box ,the directions we plan as a next step should be well organized and calculated ,it's high time for these developing countries to cut down unnecessary expenditures and to invest hugely in agriculture sector.....
 
Na Bado, Trump akazie hapohapo
Kuna misaada ambayo ilikuwa ni kama imelazimishwa tyu.

Trump sio mtu wa kwanza kutaka misaada isitishwe, hiyo ni dhana potofu.

Wapo waafrica wengi na hata wazungu kabla hata Trump hajaingia kwenye siasa, walikuwa na matumai ya kwamba , Misaada ikisitishwa, basi upo uwezekano wa kuchochea maendeleo katika Nchi masikini.

Mwana uchumi nguli Angus Deaton aliweza kutoa mfano, akanena

" serikali nyingi hutegemea watu wao kwa kodi ili kujiendesha na kutoa huduma kwa watu wao.

Serikali zinazopata pesa zao zote kutokana na misaada, hazina hiyo(kutegemea kodi badala ya misaada) hata kidogo na nadhani hiyo ni very Corrosive"

Misaada mingine ilikuwa kama kausha damu unayoiona kitaa, haijengi.

Usimtwishe Trump ukuu ambao hana.
 
Matamshi ya Kafulila yako backed up with data.

Kifupi yana Ukweli usiopingika.
 
Wakati ule yeye anapigisha muziki kwenye kipaimara pale Buzebazeba Kigoma hali ilikuwaje?
 
Ili nchi iwe tajiri lazima iwezeshe wananchi wake wazalishe na kuuza nje. Pia itumie maliasili zake kwa kupitia wananchi/raia wake badala ya kukabidhi wageni.
Fikra potofu za viongozi wengi wa Africa ni kwamba nchi yaweza kuwa tajiri huku asilimia kubwa ya wananchi wakiwa masikini.
 
Umeongea vitu vikubwa sana
 
Talk huwa haipíki rice. Hiyo misaada wangeanza kuikataa waafrika wenyewe ingemake sense. Sasa wanasubiri waisitishe ndipo waanze kuikandia.
 
Ukweli unaweza kuwepo katika kipindi, yaani ni lini umaskini wa Afrika uliongezeka, LAKINI, sikubaliani kuwa umaskini huo ulitokana na kupewa misaada.

Korea Kusini, baada ya vita ilipewa misaada mingi na USA, na leo ni Taifa tajiri, likiwa na GDP kubwa kuliko Russia.

Ujerumani baada ya vita kuu ya Dunia, ilipewa misaada mikubwa na USA, leo ndiyo nchi yenye uchumi mkubwa kuliko nchi zote za Ulaya.

Hong Kong, baada ya mgogoro wake na China Mainland, ilipewa misaada mingi na Ulaya, leo ni tajiri.

Urusi, mwishoni mwa miaka 1980 ilichoka kiasi cha kufilisika, mwanzoni mwa miaka ya 1990 ikapewa msaada na Marekani na Ulaya, leo Urusi haina uchumi wa kutegemea Taifa jingine.

UKWELI
Umaskini wa Afrika haujasababishwa na misaada, kwa kiasi kikubwa ni kutokana na poor leadership na atitude ya watu wake.

Naunga mkono Afrika kutopewa misaada kwa sababu Waafrika hawajitambui. Fikiria nchi inaenda kukopa pesa nje, halafu nchi hiyo hiyo, inatumia bilioni 300 kuchapisha mabango ya picha ya Rais, kununua magoli, kutalii na wasanii nje ya nchi, rasilimali zake zilizojengwa kwa mikopo kama bandari inawapa waarabu bure, viwanja vya ndege vilivyojengwa kwa pesa ya mikopo, inawapa waarabu bure, mbuga za wanyama na misitu, vitu walivyotengenezewa na Mungu, nchi inawapa waarabu bure!! Afrika isipewe misaada wala mikopo kwa sababu waafrika hawajitambui. Pesa za misaada zinaishia kwenye mambo ya kininga, kama vile kutengeneza machawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…