==
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila katika ukurasa wake wa X zamani tweeter ameandika haya;-
Kati ya mwaka 1970 na mwaka 1998 wakati misaada toka nje ya Africa ilikuwa ya kiwango cha Juu kuliko wakati wowote ajabu ni katika wakati huo huo umasikini wa bara la Africa ulipaa zaidi na kufikia 66% kutoka 11% kabla ya misaada hiyo ambayo leo Rais wa Marekani Donald Trump ameanza kuipunguza tena.
Mkurugenzi huyo anafafanua zaidi,
Umasikini wa bara la Afrika ulipaa au ulikua zaidi hadi kufikia kilele cha asilimia 66 kutoka asilimia 11 tu baada ya wahisani kuongeza misaada yao kwa bara la Afrika.
===
Lugha nyepesi ya utafiti huu tunasema, Kadiri Wazungu wanavyoisaidia Africa ndio umasikini wa bara la Africa unavyoongezeka hivyo uamuzi wowote wa Donald Trump usiwatetemeshe Wala kuwateteresha Waafrica
===
Baada ya comment hii ya David Kafulila nimejiuliza maswali kadhaa ikiwa Rais Donald Trump wa Marekani kupunguza kwake misaada ya Marekani (USAID ) kwa bara la Africa Je, kutachochea zaidi kukua kwa Uchumi wa bara la Africa wakati huu kwa kutumia PPP kama ilivyokuwa kabla ya miaka ya 1970 au kinyume chake?
"Wakati mwingine kumpiga chura teke ni sawa tu na kumwongezea mwendo"
===