View attachment 3258108
==
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila katika ukurasa wake wa X zamani tweeter ameandika haya, kati ya mwaka 1970 mpaka mwaka 1998 misaada toka nje ya Africa ilikuwa ya kiwango cha Juu kuliko wakati wowote ule lakini chaajabu ni katika wakati huo huo umasikini wa bara la Africa ulikua na kufikia 66% kutoka 11%.
Baada ya Rais Trump kupunguza misaada ya Marekani katika bara la Africa Je, kutachochea zaidi kukua kwa Uchumi wa Africa ?
Je, hili ndio lengo la Rais Donald Trump katika kukuza Uchumi wa Africa?
Naamini hii si habari njema kwa wanaofurahia Trump kuinyima misaada Serikali ya CCM kwani ni sawa na kumpiga teke chura.