Raffa
Senior Member
- May 28, 2024
- 182
- 120
Kumbe nia ya wazungu kutusaidia nikutaka tuendelee kuwa tegemezi?View attachment 3258108
==
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila katika ukurasa wake wa X zamani tweeter ameandika haya, kati ya mwaka 1970 mpaka mwaka 1998 wakati misaada toka nje ya Africa ilikuwa ya kiwango cha Juu kuliko wakati wowote ule lakini chaajabu ni katika wakati huo huo umasikini wa bara la Africa ulikua na kufikia 66% kutoka 11% kabla ya hiyo misaada.
Mkurugenzi huyu anafafanua zaidi kwa wasiofahamu kwamba,
Umasikini wa bara la Afrika ulipaa au ulikuwa zaidi hadi kufikia kilele Cha asilimia 66 kutoka asilimia 11 tu baada ya wahisani kuongeza misaada yao kwa bara hili la Afrika
Baada ya comment hii ya David Kafulila nimejiuliza maswali kadhaa endapo Rais Donald Trump wa Marekani kupunguza kwake misaada ya Marekani (USAID ) katika bara la Africa Je, kutachochea zaidi kukua kwa kwa Uchumi wa bara la Africa kama ilivyokuwa kabla ya miaka 1970?
Je, huenda hii ndio likawa moja ya lengo la Rais Donald Trump wa Marekani katika kukuza Uchumi wa bara la Africa au ni katika kulidhoofisha bara hili?
"Wakati mwingine kumpiga chura teke ni sawa tu na kumwongezea mwendo"
===
Hakuna kurudi nyuma lazima tupambane