David Kafulila: Taarifa zinaonesha umasikini wa bara la Afrika ulipaa zaidi wakati ambapo misaada ya wahisani ilikuwa juu zaidi

David Kafulila: Taarifa zinaonesha umasikini wa bara la Afrika ulipaa zaidi wakati ambapo misaada ya wahisani ilikuwa juu zaidi

View attachment 3258108
==
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila katika ukurasa wake wa X zamani tweeter ameandika haya, kati ya mwaka 1970 mpaka mwaka 1998 wakati misaada toka nje ya Africa ilikuwa ya kiwango cha Juu kuliko wakati wowote ule lakini chaajabu ni katika wakati huo huo umasikini wa bara la Africa ulikua na kufikia 66% kutoka 11% kabla ya hiyo misaada.

Mkurugenzi huyu anafafanua zaidi kwa wasiofahamu kwamba,

Umasikini wa bara la Afrika ulipaa au ulikuwa zaidi hadi kufikia kilele Cha asilimia 66 kutoka asilimia 11 tu baada ya wahisani kuongeza misaada yao kwa bara hili la Afrika​


Baada ya comment hii ya David Kafulila nimejiuliza maswali kadhaa endapo Rais Donald Trump wa Marekani kupunguza kwake misaada ya Marekani (USAID ) katika bara la Africa Je, kutachochea zaidi kukua kwa kwa Uchumi wa bara la Africa kama ilivyokuwa kabla ya miaka 1970?

Je, huenda hii ndio likawa moja ya lengo la Rais Donald Trump wa Marekani katika kukuza Uchumi wa bara la Africa au ni katika kulidhoofisha bara hili?

"Wakati mwingine kumpiga chura teke ni sawa tu na kumwongezea mwendo"





===
Samia mitano tena
 
Inaendelea na nini wakati kila kitu kimeshikwa na Wachina?
 
Kuna watu wako kwenye payroll wanalipwa mamilioni kumpamba kafulila

Anatafuta cheo gani?
 
Mbinu za Kafulila kutafuta Umaarufu ni za kijinga sana! cha kushangaza amewapa mamlaka hata ya kututisha sisi tunao mchalenji!
 
Umasikini wa Africa tatizo haliwezi kuwa ni misaada ya wazungu ila.ujinga wa waafrica wenyewe.
 
Inaendelea na nini wakati kila kitu kimeshikwa na Wachina?
Hii ya Wachina hata Mimi napendekeza waangaliwe sana hawa watu.

Tunahitaji Wawekezaji lakini sio wa aina yao
 
View attachment 3258108
==
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila katika ukurasa wake wa X zamani tweeter ameandika haya;-

Kati ya mwaka 1970 na mwaka 1998 wakati misaada toka nje ya Africa ilikuwa ya kiwango cha Juu kuliko wakati wowote ajabu ni katika wakati huo huo umasikini wa bara la Africa ulipaa zaidi na kufikia 66% kutoka 11% kabla ya misaada hiyo ambayo leo Rais wa Marekani Donald Trump ameanza kuipunguza tena.

Mkurugenzi huyo anafafanua zaidi,

Umasikini wa bara la Afrika ulipaa au ulikua zaidi hadi kufikia kilele cha asilimia 66 kutoka asilimia 11 tu baada ya wahisani kuongeza misaada yao kwa bara la Afrika.​


===
Lugha nyepesi ya utafiti huu tunasema, Kadiri Wazungu wanavyoisaidia Africa ndio umasikini wa bara la Africa unavyoongezeka hivyo uamuzi wowote wa Donald Trump usiwatetemeshe Wala kuwateteresha Waafrica
===


Baada ya comment hii ya David Kafulila nimejiuliza maswali kadhaa ikiwa Rais Donald Trump wa Marekani kupunguza kwake misaada ya Marekani (USAID ) kwa bara la Africa Je, kutachochea zaidi kukua kwa Uchumi wa bara la Africa wakati huu kwa kutumia PPP kama ilivyokuwa kabla ya miaka ya 1970 au kinyume chake?

"Wakati mwingine kumpiga chura teke ni sawa tu na kumwongezea mwendo"





===
Mimi sio CCM ila Kafulila ni mtu amebarikiwa kwenye hoja, hata kama tutamtukana vipi bado atafikiria nje ya box, tangu hii misaada imeondolewa Hali ya ukimya umetawala hakuna aliyesema Kiuchumi hii inamaanla gani zaidi ya huyu Kafulila, Mimi namuunga mkono ila Mimi kamwe sio CCM.
 
Hii ya Wachina hata Mimi napendekeza waangaliwe sana hawa watu.

Tunahitaji Wawekezaji lakini sio wa aina yao
Wameanza mtindo wa kufungua supernarket wanauza vitu vya kariakoo kwa bei ndogo sana
 
Back
Top Bottom