Kuwa mkweli...
warumi mwenzako hafichi mahaba yake kwa Jide na ww huna sababu ya kuficha mahaba yako kwa Kiba... and in fact, hakuna tatizo lolote kwa mtu kuwa na mahaba kwa fulani!!! Tatizo lenu wengine, kwavile mnampenda X basi hamtaki kuona Y akichomoza na mkiona kuna dalili za za kwamba Y anataka kuchomoza... basi mtakesha mkiugua maumivu ya pole pole mkitamani asichomoze... salama na uzima wenu unaibuka ghafla mnaposikia kwamba yule msiyetaka ameshindwa kuchomoza... ndipo mtakimbilia kwenye PC kuelezea furaha yenu... hizo ndio tunaita tabia za "kwanini... tabia za heri tukose wote...
Hilo la kauli ya Diamond... sidhani kama kuna mjadala manake umeonesha wazi wala hufahamu unachoongea. Kuhusu Kiba... una bahati mbaya sana kama unadhani kuna mtu anamchukia kama wewe unavyomchukia Diamond!!! Watu wengi wanasikitika kuhusu Kiba coz' wanafahamu he's something lakini anaonekana kama hajui anachofanya. Tofautisha kumchukia mtu na kuumizwa mtu anaposhindwa kufanya kazi... pole sana kama unadhani leo Kiba aki-hit watu tutakufa... sisi wengine tupo flexible, tunapenda vitu vizuri and we don't care hivyo vizuri vinatoa kwa nani... poleni nyie mnaopatwa magonjwa ya vipindi kila mnaposikia Diamond anatoboa... PRESHA JUU!!!!
Mwanzoni unadai kwamba humchukii Diamond bali mbwembwe zake... sasa mbembwe za Diamond zinakupunguzia nini au kama asingeleta hizo mbwembe ungeongezeka nini? Ndio maana tunasema wivu na chuki zisizo na maana!!! Wewe tangaza magari yote dunia hii ni ya kwako, wala hunisumbui... Ray keshasema yeye ndo msanii tajiri kuliko wote Tanzania... mchukie basi, si mbwebwe hizo!!! Hivi wasanii wangapi duniani wanapiga fix na mbwembwe... yaani unaweza kuchukia kv tu anasema ana hiki au kile wakati hana?