Dawa ya mseto ya kutibu malaria ipigwe marufuku kama ilivyokuwa kwa chloroquine

Wewe hata hauumwi malaria, umekunywa hiyo Mseto kimakosa tu, umedanganywa kwa kufanya BS kwa hivyo vi maabara uchwara vya mtaani kwako ukaambiwa una malaria, na jinsi ambavyo ulikuwa na hamu na hayo majibu. Ndugu nenda kafanye mRDT, na vipimo vingine kama urinalysis, H.pylori test, ili upate bainisho la tatizo lako
 
Katika dawa watu wanazichukulia poa ni mseto ila kwangu mimi ndiyo dawa bora sana kwa kutibu malaria
Hiyo ni dawa Bora kabisa Kwa malaria watu wanaogopa kwakua inavidonge vingi sana lakini ukimaliza na malaria kwisha
 
Unaijua malaria au unaisikia kuna mtu wangu wa karibu alienda kupima malaria akakutwa alijikuta ana-tundukiwa trip tisa za quinine we huijui malaria vizuri
 
Hiyo amodiaquine watoto wa 2000 hawaijui hii. sijaisikia muda mrefu km bado ipo kwenye mzunguko. dawa ya kitemi sana hiyo. ukinywa tu na yenyewe inakuongezea ugonjwa, usipokaa sawa unanyooka iviivi mchana kweupe.
 
Hivi kile kiwanda kilichojengwa Kibaha kwa lengo la kudhibiti mazalia ya mbu, kwa lengo la kuukomesha kabisa huo ugonjwa; kiliishia wapi!!!
 
isije ikawa malaria imekupanda kichwani ndo maana umeandika hiki ulichokiandika.....maana sio akili ya kawaida yaani dawa ipigwe marufuku kwa sababu yako wewe tu.
 
Wewe utakuwa una matatizo mengine lakini mseto ndio the best dawa na prophylaxis ya malaria
 
Hiyo amodiaquine watoto wa 2000 hawaijui hii. sijaisikia muda mrefu km bado ipo kwenye mzunguko. dawa ya kitemi sana hiyo. ukinywa tu na yenyewe inakuongezea ugonjwa, usipokaa sawa unanyooka iviivi mchana kweupe.
Mpaka masikio husikii ile dawa ilikua yakiuaji ndo maana haikudumu sana sokoni
 
isije ikawa malaria imekupanda kichwani ndo maana umeandika hiki ulichokiandika.....maana sio akili ya kawaida yaani dawa ipigwe marufuku kwa sababu yako wewe tu.
Hapana malaria ikipata kichwani mfano ukiwa kitandani unahisi kama kitanda kimegeuka juu unakua unajishika ili usianguke
 
Zipi wewe ndio mtumiaji pekee sisi sio watumiaji?
Artemether and lumefantrine may cause side effects.
  • headache.
  • dizziness.
  • weakness.
  • muscle or joint pain.
  • tiredness.
  • difficulty falling asleep or staying asleep.
  • vomiting.
  • loss of appetite.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…