Dawa ya mseto ya kutibu malaria ipigwe marufuku kama ilivyokuwa kwa chloroquine

Dawa ya mseto ya kutibu malaria ipigwe marufuku kama ilivyokuwa kwa chloroquine

Unajiita Mpigania uhuru halafu unakuwa legelege, ungeambiwa unywe mwarobaini kujitibu malaria si ungekufa hapo hapo.
Kitu kinachemshwa unapewa unywe nyingine ujifukizia hakuna dozi maalum ni bidii Yako tu upone.
Artemether lumefantrine ni dawa yenye maudhi kidogo kulinganisha na dawa nyingine za malaria 🦟 lakini unapoona hali yako inazidi kuwa mbaya rudi kituo cha afya
 
Miaka ya 2000's niliumwa malaria nikanywa amodiaquine ziko kama tatu hazizidi tano ila sitakaa nisahau ile experience ilikua unachungulia kaburi ile dawa iliongeza maumivu maradufu bora mchana usiku ndo maamuvi yaanapewa greenlight hulalali mwili ulichoka na nguvu zote ziliniishia

Week hii mwanzoni nimeumwa malaria nikasema acha ntumie mseto aisee mpaka sahivi najuta kwanini nilikubali mseto ni masaa 24 tokea nimalize mpaka sahivi
  • Mwili umechoka
  • Sina hamu ya kula yaani kula ni kwa mbinde
  • Mdomo mchungu kupita maelezo
  • Nikihema natoa harufu ya dawa za mseto
Hapana aisee hii dawa ipigwe marafuku kama ilivyokua kwa chloroquine na amodaquine ambazo hazitumiki tena
Ni bora ningekunywa quinine sio kwa mateso haya

Kwenye medicine kuna kitu kinaitwa pharmacovigiliance dawa ikishakuwa approval inafuatiliwa kama kuna severe side effects ambazo hazikuwa notice kipindi cha clinical trials ndo maana leo hii chloroquine au amodaquine hazitumiki tena
Metakelfin ndio zinanisaidiaga ila hizo mseto sijawahi kuzielewa maana zinanyong'onyeza sana na unakuwa lege lege karibu wiki nzima.
Siku hizi Malegendary tunakunywa chai ya Moringa na Kula majani yake kama mboga so maralia tunaisokia kwa jirani tu.
 
Hiyo dawa za mseto mie nilitumia tumbo likavimba kama kitenesei nikawa nashindwa mpaka kupumua ikabidi niende hospitali nikachomwa sindano ya kupunguza tumbo kujaa ,mpaka leo nikiumwa malari natumia artequick
Acha uongo
 
Nadhani unatakiwa kujua dawa inayoendana na mwili wako/damu yako. Dawa ambayo wewe kwako inakutesa kuna mtu anaimeza usiku na asubuhi anaamka na kwenda kazini bila shida.

Mfano mimi napiga Metakelfin bila shida ila kuna mtu ambaye dawa zenye sulphur zinamuendesha hawezi tumia maana inaweza mletea matatizo makubwa sana.

Mimi Aspirin au dawa yenye aspirin kama 'Dawa tatu' au 'Hedex' siwezi meza kwasababu itaniletea maumivu makali ya tumbo kama vidonda vya tumbo so inategemea na damu yako mzee dawa haiwezi pigwa marufuku na kuna watu wanaitumia vizuri na haiwadhuru.
 
Back
Top Bottom