Dawa ya mseto ya kutibu malaria ipigwe marufuku kama ilivyokuwa kwa chloroquine

Unajiita Mpigania uhuru halafu unakuwa legelege, ungeambiwa unywe mwarobaini kujitibu malaria si ungekufa hapo hapo.
Kitu kinachemshwa unapewa unywe nyingine ujifukizia hakuna dozi maalum ni bidii Yako tu upone.
Artemether lumefantrine ni dawa yenye maudhi kidogo kulinganisha na dawa nyingine za malaria 🦟 lakini unapoona hali yako inazidi kuwa mbaya rudi kituo cha afya
 
Metakelfin ndio zinanisaidiaga ila hizo mseto sijawahi kuzielewa maana zinanyong'onyeza sana na unakuwa lege lege karibu wiki nzima.
Siku hizi Malegendary tunakunywa chai ya Moringa na Kula majani yake kama mboga so maralia tunaisokia kwa jirani tu.
 
Hiyo dawa za mseto mie nilitumia tumbo likavimba kama kitenesei nikawa nashindwa mpaka kupumua ikabidi niende hospitali nikachomwa sindano ya kupunguza tumbo kujaa ,mpaka leo nikiumwa malari natumia artequick
Acha uongo
 
Nadhani unatakiwa kujua dawa inayoendana na mwili wako/damu yako. Dawa ambayo wewe kwako inakutesa kuna mtu anaimeza usiku na asubuhi anaamka na kwenda kazini bila shida.

Mfano mimi napiga Metakelfin bila shida ila kuna mtu ambaye dawa zenye sulphur zinamuendesha hawezi tumia maana inaweza mletea matatizo makubwa sana.

Mimi Aspirin au dawa yenye aspirin kama 'Dawa tatu' au 'Hedex' siwezi meza kwasababu itaniletea maumivu makali ya tumbo kama vidonda vya tumbo so inategemea na damu yako mzee dawa haiwezi pigwa marufuku na kuna watu wanaitumia vizuri na haiwadhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…