Dawa ya Uhakika ya Kupunguza Uzito Bajeti Ipo, Sitaki Msaada wa Bure

Dawa ya Uhakika ya Kupunguza Uzito Bajeti Ipo, Sitaki Msaada wa Bure

Wakati mwingine mtu mwembamba akiona hapewi atention sana hujifanya ni mnene anatafuta dawa ya kupungua ili nae aonekane. Sasa wewe na wembamba wako huo nikikupa dawa zangu za kupunguza unene si utafariki? Wakati mwingine madogo punguzeni sifa au mnataka tuwapeleke milembe?
Lete dawa
 
Nikiwa Trainer wako nitakuchota sana mitama na kukung'uta mibanzi ya usoni hadi ufurahi na roho yako!

Haiwezekani umpangie Trainer nini cha Kufanya!
[emoji23][emoji23]
 
kunayo sliming tea na fat bunner,, hiyo sliming tea ni majani unatakiwa uchanganye kwenye maji then unakunywa asubuhi na jioni,, fat bunner ni capsule zenyewe unakunywa kakidonge kamoja kwa siku,,, bei ya sliming tea ni 100k per pact ila hiyo fat bunner ni elf 30 kwa kopo,,, Haya chagua unataka kipi hapo then useme upo wapi umtumiwe
 
Kichwa cha Habari

Natafuta dawa ya uhakika ya kupunguza uzito (Kilo 105, Futi 6). Ahadi ya malipo ipo, sitaki msaada wa bure.

Wakuu salama,

Nipo hapa nikiwa na nia ya dhati kabisa ya kufanya biashara na mtu mwenye suluhisho la uhakika. Niko siriaz na sijiomba msaada, kama una dawa inayofanya kazi kweli, nitakulipa vizuri sana.

Mimi ni kijana wa miaka 26, nina urefu wa futi 5.5 mpaka 6 hivi, lakini uzito wangu umefika kilo 105. Kiukweli unene huu kuwa chibonge na kitambi umeanza kunikata mawazo na kuondoa muonekano wangu wa ujana

Kabla hamjaniletea yale mapendekezo ya kawaida, naomba niweke wazi mtindo wa maisha yangu ili anayeleta dawa ajue anadili na mazingira gani

Sina muda wa mazoezi, Ratiba yangu ni ngumu Naamka saa 12 asubuhi, naingia kwenye shughuli zangu ambazo asilimia 90 ni kukaa tu kuanzia asubuhi hadi jioni, Nikitoka saa 10 jioni natumia usafiri wa gari hadi nyumbani Hakuna muda wa kutembea wala kukimbia.

Siwezi kuacha kula au kupunguza msosi Hapa tusidanganyane, siwezi kukaa njaa.

Mimi ni mnywaji, Kila siku jioni lazima nitoke kwenda kupata kileo hadi usiku Sinywi bia, mimi ni mtu wa pombe kali na sibadili brand matumizi yangu ni Hanschoice kila siku. Na kama mnavyojua, pombe kali inataka msosi mzito mzito, kwa hiyo suala la Diet hapa halipo.

Kutokana na mazingira hayo, suluhisho pekee ninalolitaka ni dawa maalum ya kukata wese na kupunguza mwili bila kunitegemea mimi nifanye kazi ya ziada ya kukimbia au kushinda njaa.
Kama wewe ni una duka la dawa za asili/kisasa, au una siri ya dawa yoyote ya uhakika ambayo imeshawahi kukata kitambi na uzito kwa mtu mwenye mtindo wa maisha kama wangu
Shusha nondo zako hapa chini jinsi dawa yako inavyofanya kazi.

Njoo PM tufanye biashara. Gharama sio tatizo, ilimradi tu isiwe utapeli na iwe na matokeo yanayoonekana.

Nawasilisha kwa heshima wakuu.
Kwanza kabla ya ushauri wewe una urefu wa 5'5'' hakuna urefu wa mpaka 6'... ww ni mfupi na kwa uzito wako ni kibonge nyanya.

Pili tambua hakuna dawa ya kupunguza uzito ila kuna dawa ya kukufanya ukonde kwa muda ambapo itafanya mwili wako kuwa na metabolism ya juu au kufanya uharishe sana na kupoteza maji mwilini hii itafanya upungue huo unaosema uzito.

Tatu, elewa ili kupunguza uzito inabidi calorie unazochoma mwilini ziwe kubwa kuliko unazoingiza na ulizohifadhi mwilini. Mwili wa binadamu ni kama gari tu unatumia energy. Energy ikitumika kubwa wese lazima likate.

Kwa style ya maisha yako

1. Kunywa pombe
2. Kula sana
3. Kutofanya mazoezi
4. Kukaa muda mrefu

Kupungua hata kilo mbili kwa mwaka labda uende kwa Mwamposa umchangie sadaka au kakope kausha damu...

Kwa kifupi kwa umri wako wewe ni kibonge haswa haswa na minyama uzembe. Bila diet na mazoezi ya kukaza hayo manyama ww endelea na lifestyle yako na jiandae kutomb%*a, magonhwa ya kisukari moyo figo...
Na ukiendekeza madawa hayo ya uzito utaharisha mpaka NZUTU ivimbe...

All the best na kuweka puto pale Mloganzila...
 
kunayo sliming tea na fat bunner,, hiyo sliming tea ni majani unatakiwa uchanganye kwenye maji then unakunywa asubuhi na jioni,, fat bunner ni capsule zenyewe unakunywa kakidonge kamoja kwa siku,,, bei ya sliming tea ni 100k per pact ila hiyo fat bunner ni elf 30 kwa kopo,,, Haya chagua unataka kipi hapo then useme upo wapi umtumiwe
Nipo Moro nataka vyote
 
Kwanza kabla ya ushauri wewe una urefu wa 5'5'' hakuna urefu wa mpaka 6'... ww ni mfupi na kwa uzito wako ni kibonge nyanya.

Pili tambua hakuna dawa ya kupunguza uzito ila kuna dawa ya kukufanya ukonde kwa muda ambapo itafanya mwili wako kuwa na metabolism ya juu au kufanya uharishe sana na kupoteza maji mwilini hii itafanya upungue huo unaosema uzito.

Tatu, elewa ili kupunguza uzito inabidi calorie unazochoma mwilini ziwe kubwa kuliko unazoingiza na ulizohifadhi mwilini. Mwili wa binadamu ni kama gari tu unatumia energy. Energy ikitumika kubwa wese lazima likate.

Kwa style ya maisha yako

1. Kunywa pombe
2. Kula sana
3. Kutofanya mazoezi
4. Kukaa muda mrefu

Kupungua hata kilo mbili kwa mwaka labda uende kwa Mwamposa umchangie sadaka au kakope kausha damu...

Kwa kifupi kwa umri wako wewe ni kibonge haswa haswa na minyama uzembe. Bila diet na mazoezi ya kukaza hayo manyama ww endelea na lifestyle yako na jiandae kutomb%*a, magonhwa ya kisukari moyo figo...
Na ukiendekeza madawa hayo ya uzito utaharisha mpaka NZUTU ivimbe...

All the best na kuweka puto pale Mloganzila...
Duh
 
Yani uchome calorie na usipungue? Mazoezi ya aina gani hayo? Unafanya cardio au unabeba vyuma tu?
Vitu vingine hatuhitaji kubishana mkuu,,unaweza kufanya utafiti wewe mwenyewe. Maandiko yapo mengi sana hata hapa Jukwaani..huko utaelezwa kitaalamu zaidi,aina ya zoezi na kiwango cha calories utazo choma.

Imagine mtu anatakiwa afanye aina fulani ya zoezi kwa masaa mawili ili achome kalories 200. Na akitoka pale anakula tena chakula chenye kalories 1000.

Ndo maana wengi walio fanya mazoezi kwa kutarget kupungua hawakupungua,aidha waliongeza uzito ama alipungua kg moja tu kwa miezi 6.

Njia sahihi ni ku cut down kalories intake,,yaani mwili uutengenezee upungufu wa calories kwa kuto introduce chakula kwa kipindi fulani. kwa kufanya intermediate fasting.
 
Mkuu hakuna dawa ya kupunguza unene,hakuna, yaani eti unywe kidonge halafu usijinyime kula au kufanya mazoezi eti uzito upungue,hiyo dawa haipo,kama ipo ni sumu mfano Ozempic ni sumu inayoleta upofu.
Kuna msemo wa kiingereza unasema " you can't eat your cake and have it" na hicho ndo unachokitaka wewe. Yaani hutaki kuumia halafu unataka upungue,nakwambia tu haiwezekani.
Ratiba yako ya kazi hata sio ngumu,,unaweza kuamka saa kumi na moja alfajiri ukafanya mazoezi hadi saa kumi na mbili. Pia unatoka kazini mapema sana,unaweza kufanya mazoezi baada ya kutoka kazini hata masaa mawili kila siku,ni wewe hujataka.
Pia nadhani unakula vyakula vibaya eg vyenye mafuta mengi,pia hapo kwenye pombe,sidhani kama ukipunguza kunywa pombe hata siku moja utakufa au utaumwa.
Kupunguza uzito ni kitendo ambacho sio rahisi na lazima ulipie gharama,hakuna shortcut,haipo.
Mwisho: Nakuchana live ,kama hutaki kujinyima ili upungue pressure na sukari vitakufundisha ujinyime kwa lazima. Kama hutaki kujinyima pombe ili upungue,pressure na kisukari vitakufundisha kujinyima pombe kwa lazima. Hapo bado hujaambiwa una matatizo ya uzazi mbegu zimekuwa nyepesi kwa kula hovyo hovyo, na hayo matatizo ya afya siku hizi yanawakumba vijana wadogo miaka 29 kushuka chini.
Chaguo ni lako,jinyime na ufanye mazoezi sasahivi au subiri baada ya miaka kadhaa magonjwa yakulazimishe kufanya mazoezi na kula vyakula vinavyotakiwa.
Have a nice day.
 
Vitu vingine hatuhitaji kubishana mkuu,,unaweza kufanya utafiti wewe mwenyewe. Maandiko yapo mengi sana hata hapa Jukwaani..huko utaelezwa kitaalamu zaidi,aina ya zoezi na kiwango cha calories utazo choma.

Imagine mtu anatakiwa afanye aina fulani ya zoezi kwa masaa mawili ili achome kalories 200. Na akitoka pale anakula tena chakula chenye kalories 1000.

Ndo maana wengi walio fanya mazoezi kwa kutarget kupungua hawakupungua,aidha waliongeza uzito ama alipungua kg moja tu kwa miezi 6.

Njia sahihi ni ku cut down kalories intake,,yaani mwili uutengenezee upungufu wa calories kwa kuto introduce chakula kwa kipindi fulani. kwa kufanya intermediate fasting.
Nakubaliana na wewe mkuu sikatai.

Mazoezi pekee hayapunguzi uzito kwa ufanisi bila kuzingatia chakula unachokula. Lakini haiondoi ukweli ili kuchoma calorie lazima ufanye mazoezi ambapo result yake ni kupunguza uzito.

Kuna option 3
1. Mazoezi makali pekee - uzito upungua taratibu sana.
2. Diet pekee - uzito upungua kwa haraka ila ukiacha unarudi kwa haraka.
3. Mazoezi+Diet uzito upungua kwa ufanisi na kuwa na mwili mkakamavu na hudumu kwa muda mrefu.

So chaguo ni lako.
 
Uko sahihi ndugu...tunacho pinga ni kwamba mtu anafanya mazoezi na kweli anachoma kalories 500 kwa mfano...same time anakula chakula chenye total calories 1500..

Tafsiri yake ni nini?
 
Kilo 105 futi 6 umri 26 aisee utatoboa kweli?

Hili jambo ni hatari sana fanya sana mazoezi kimbiza upepo ruka kamba inua vyuma weight ishuke hiyo.
 
Uko sahihi ndugu...tunacho pinga ni kwamba mtu anafanya mazoezi na kweli anachoma kalories 500 kwa mfano...same time anakula chakula chenye total calories 1500..

Tafsiri yake ni nini?
Hamna anachofanya hapo. Ni anakaza mwili tu kuwa fiti ila hawezi punguza uzito.
 
Back
Top Bottom