Dawa ya Uhakika ya Kupunguza Uzito Bajeti Ipo, Sitaki Msaada wa Bure

Dawa ya Uhakika ya Kupunguza Uzito Bajeti Ipo, Sitaki Msaada wa Bure

Kupunguza uzito au kitambi ni simple sana.
Step1: Chukua hiyo pesa uliyonayo uhonge meneja wa benki akupe mkopo
Step2: nunua gari iliyochoka hela nyingne itakayo baki kunywa au kula na marafiki hadii iishe ndan ya wiki mbili uwe umemaliza hela yote umebaki na hiyo gari mkweche then litaanza kusumbua lipak au uza bei hasara ule ziishe. But kumbuka kupunguza nguo zako zote ziwe size ndogo kabisaa maana??!@.
Hapo kitakachobaki ni wewe na kudaiwa na benki tu na huna cha kuwalipa watachukua nyumba au viwanja vyako ubaki empty. Wife atakutoroka ubaki single. Marafiki watakutenga ubaki solo, familia haitakutambua ubaki stupid.
Ndan ya ya wiki moja mawazo, stress mix ujinga ulioufanya vitakukondesha ubaki kichwa tu kazi kwisha.
Duuh
 
Naam mkuu,hiki ndo kinacho fanyika kwa wengi aidha kwa kujua ama kuto kujua..
Mkuu please nifungulie pm nimetuma message imegonga mwamba, na ishu na UTT...hili swali liko private kidogo...natanguliza shukrani 🙏
 
Baharia mbabaishaji namjua hapa anawachora tu hana unene wala nini
Pitia hii tangu Mwaka 2024
Screenshot_20260605-160414.jpg
 
Kichwa cha Habari

Natafuta dawa ya uhakika ya kupunguza uzito (Kilo 105, Futi 6). Ahadi ya malipo ipo, sitaki msaada wa bure.

Wakuu salama,

Nipo hapa nikiwa na nia ya dhati kabisa ya kufanya biashara na mtu mwenye suluhisho la uhakika. Niko siriaz na sijiomba msaada, kama una dawa inayofanya kazi kweli, nitakulipa vizuri sana.

Mimi ni kijana wa miaka 26, nina urefu wa futi 5.5 mpaka 6 hivi, lakini uzito wangu umefika kilo 105. Kiukweli unene huu kuwa chibonge na kitambi umeanza kunikata mawazo na kuondoa muonekano wangu wa ujana

Kabla hamjaniletea yale mapendekezo ya kawaida, naomba niweke wazi mtindo wa maisha yangu ili anayeleta dawa ajue anadili na mazingira gani

Sina muda wa mazoezi, Ratiba yangu ni ngumu Naamka saa 12 asubuhi, naingia kwenye shughuli zangu ambazo asilimia 90 ni kukaa tu kuanzia asubuhi hadi jioni, Nikitoka saa 10 jioni natumia usafiri wa gari hadi nyumbani Hakuna muda wa kutembea wala kukimbia.

Siwezi kuacha kula au kupunguza msosi Hapa tusidanganyane, siwezi kukaa njaa.

Mimi ni mnywaji, Kila siku jioni lazima nitoke kwenda kupata kileo hadi usiku Sinywi bia, mimi ni mtu wa pombe kali na sibadili brand matumizi yangu ni Hanschoice kila siku. Na kama mnavyojua, pombe kali inataka msosi mzito mzito, kwa hiyo suala la Diet hapa halipo.

Kutokana na mazingira hayo, suluhisho pekee ninalolitaka ni dawa maalum ya kukata wese na kupunguza mwili bila kunitegemea mimi nifanye kazi ya ziada ya kukimbia au kushinda njaa.
Kama wewe ni una duka la dawa za asili/kisasa, au una siri ya dawa yoyote ya uhakika ambayo imeshawahi kukata kitambi na uzito kwa mtu mwenye mtindo wa maisha kama wangu
Shusha nondo zako hapa chini jinsi dawa yako inavyofanya kazi.

Njoo PM tufanye biashara. Gharama sio tatizo, ilimradi tu isiwe utapeli na iwe na matokeo yanayoonekana.

Nawasilisha kwa heshima wakuu.
Chemsha maji lita moja na mchanganyiko wa Majani 10-15 ya Mpera na Limau (katakata) then kunywa asubuhi na usiku kwa siku 14 then pima uzito na uje utoe ushahidi hapa kama umepungua ama la.
 
Ukiwa umesimama unaoga ukiiangalia unaiona kweli ??! 🤣🤣🤣🤣 Wewe ulitakiwa uchinjwe umenona sana mzeee
 
Yani unaingia kwenye reli na kutoka mkuu,una nia ya dhati ya kupunguza uzito lakini hutak kupunguza kula,mmmhh??? Sasa ungeweka pia vyakula unavyokula sana ni aina gan tungeweza kukushauri jambo,labda kwa uchache punguza machapat chapati asubuh kula mayai ya kuchemsha,mboga mboga,nyama piga,punguza vinywaji vitamu kama sukari,ila cha mwisho nunua baiskeli uwe unaendesha siku moja moja katika mizunguko yako hasa weekend,cha ziada sasa najua utashangaa sana ila fanyia kazi anza kulala chini achana na godoro,kama unahofia barid tandika mkeka weka na blanket lala chinikitandani panda tu kufanya tendo ukimaliza rudi chini,utaona mabadiliko ukifanyia kaz haya nloandika
Nyie ndio wagumu kuelewa. Dogo kajiweka wazi vizuri kabisa. Kawaambia kama dawa yenu ni kupunguza kula hiyo dawa baki nayo. Kwani shida iko wapi hapo? Ksbb hawezi kupunguza kusenga. Safi sana.

Pili kuna mwingine hapo juu kasema vibonge hawafoki foki wapole. Hata dogo hajafoka wala kuchamba,ila kawachana tu live mapema ksbb wote mlikuwa mnakuja na aina moja ya ushauri kupunguza ama kuanza kumpiga mawe. Kwa hiyo dogo kaona isiwe kesi kaona aanze kuwachana kigumu ili msije na taarabu zenu mlizozizoea kupunguza kula au kumrushia mawe.

Pia kaweka wazi hataki shobo sijui bure. Yeye yuko njema. Kwa hiyo wewe kama huna utapeli uko fresh ingiza gear zako ifanye kazi sawa sawa,lamba chako.
Nimependa sana dogo kashusha nondo wazi kabisa then kachoma ndani.

In search dawa za aina anazomaanisha dogo zipo kibwena hasa huko mamtoni bila kufanya
surgery. Japo kibongo bongo kuna mmoja nimempitia juzi kati hapo mtandaoni kwa kutumia TUNDA LA APPLE UNALIKATA KATIKATI UNATUMIA KIPANDE KIPANDE +MAGANDA YA LIMAO MOJA+KINGINE CHA TATU NIMESAHAU. HUO MCHANGANYIKO UNAUONGEZEA MAJI VIJIKO VITATU UNAKUNYWA HUO KILA SIKU. KWA WIKI UNAPUNGUZA KILO 10
 
Back
Top Bottom