Dawa ya Uhakika ya Kupunguza Uzito Bajeti Ipo, Sitaki Msaada wa Bure

Dawa ya Uhakika ya Kupunguza Uzito Bajeti Ipo, Sitaki Msaada wa Bure

Attachments

  • 580348ab-10cc-4982-9fa0-c9411b6659aa.jpeg
    580348ab-10cc-4982-9fa0-c9411b6659aa.jpeg
    207.8 KB · Views: 16
Kichwa cha Habari

Natafuta dawa ya uhakika ya kupunguza uzito (Kilo 105, Futi 6). Ahadi ya malipo ipo, sitaki msaada wa bure.

Wakuu salama,

Nipo hapa nikiwa na nia ya dhati kabisa ya kufanya biashara na mtu mwenye suluhisho la uhakika. Niko siriaz na sijiomba msaada, kama una dawa inayofanya kazi kweli, nitakulipa vizuri sana.

Mimi ni kijana wa miaka 26, nina urefu wa futi 5.5 mpaka 6 hivi, lakini uzito wangu umefika kilo 105. Kiukweli unene huu kuwa chibonge na kitambi umeanza kunikata mawazo na kuondoa muonekano wangu wa ujana

Kabla hamjaniletea yale mapendekezo ya kawaida, naomba niweke wazi mtindo wa maisha yangu ili anayeleta dawa ajue anadili na mazingira gani

Sina muda wa mazoezi, Ratiba yangu ni ngumu Naamka saa 12 asubuhi, naingia kwenye shughuli zangu ambazo asilimia 90 ni kukaa tu kuanzia asubuhi hadi jioni, Nikitoka saa 10 jioni natumia usafiri wa gari hadi nyumbani Hakuna muda wa kutembea wala kukimbia.

Siwezi kuacha kula au kupunguza msosi Hapa tusidanganyane, siwezi kukaa njaa.

Mimi ni mnywaji, Kila siku jioni lazima nitoke kwenda kupata kileo hadi usiku Sinywi bia, mimi ni mtu wa pombe kali na sibadili brand matumizi yangu ni Hanschoice kila siku. Na kama mnavyojua, pombe kali inataka msosi mzito mzito, kwa hiyo suala la Diet hapa halipo.

Kutokana na mazingira hayo, suluhisho pekee ninalolitaka ni dawa maalum ya kukata wese na kupunguza mwili bila kunitegemea mimi nifanye kazi ya ziada ya kukimbia au kushinda njaa.
Kama wewe ni una duka la dawa za asili/kisasa, au una siri ya dawa yoyote ya uhakika ambayo imeshawahi kukata kitambi na uzito kwa mtu mwenye mtindo wa maisha kama wangu
Shusha nondo zako hapa chini jinsi dawa yako inavyofanya kazi.

Njoo PM tufanye biashara. Gharama sio tatizo, ilimradi tu isiwe utapeli na iwe na matokeo yanayoonekana.

Nawasilisha kwa heshima wakuu.
Ushapungua
 
Kuna vimbegu hivyo ni balaa ukila kimoja 7naharisha siku nzima bei ya kimoja ni elf 5 tu ukitumia siku nne unapungua
 
Funga masaa 18. Diner kula saa 12 jioni, chai kanywe saa 5 au 6 kesho yake. Rudia mtindo huo siku 90, usipopungua, achana na zoezi la kupungua. kwa dawa za mimea tiba tuwasiliane kwa 0713 039 875. Pia zingatia elimu ya ulaji sahihi (Ketogenic-mfano kuondoa sukari na kupunguza wanga huku ukiongeza protein ) na mtindo wa maisha (kama kulala masaa 6, kufanya kazi ya kutoka jasho kwa siku, kupunguza stress)
 
Back
Top Bottom