Mgosi, nafikiri utaratibu ni sawa wa polisi kumtaka mtu aende mwenyewe kituoni ila kuna kasoro katika namna ambavyo Kamanda Sirro anafanya kazi yake.
Sidhani kama polisi wanapaswa kutangaza operesheni zao baada ya orodha kutangazwa hadharani.
Wanapaswa kufanya kazi yao kimyakimya na habari zote ziandikwe watu wakifikishwa mahakamani.
Ila kwa jinsi mambo yanavyokwenda inawabidi pilisi kuweka kila kitu wazi ili asilaumiwe mtu.
Amachosema
Kimweri ni kweli, kila kitu manual manual
Polisi wameshafanya makosa, hawapaswi kufanyia kazi tuhuma kwa majina ya watu hadharani.
Kitendo hicho tu kinatosha kuvuruga uchunguzi na ushahidi
Kutaja watu bila kuwa na ushahidi ni kosa. Katika nchi za wenzetu watu wangevuna mabilioni
Tatu, Mbowe ni kiongozi wa kisiasa Bungeni, katika vyama n.k. Kumfikia kwa simu bila kuanza kutangaza jina lake ni sehemu ya weledi. Kwanini hawakufanya hivyo
Kulikuwa na sababu gani za Sirro kwenda kwenye TV ikiwa Polisi ina intelejensia zote?
Alichokifanya kina sura ya kudhalilisha na kinachukua sura ya kisiasa? Kwanini!
1. Mbowe aliandamwa na Bilicana
2. Akafuatiliwa Hotel zake huko Machame
Yote hayo yalifanyika yakibeba hisia za ''political motivations'' nyuma yake
Leo hata kama Mbowe atakikutwa na lolote tayari kuna makosa yamefanyika
Kosa la kwanza ni hilo la Polisi kuvuruga uchunguzi wao wenyewe.
Huwezi kumtuhumu mtu kabla ya kumpekua.
Hivi kama Mbowe ana kidhibiti si atakuwa ameshaharibu ushahidi kama ni hivyo!
Polisi wanatangaza katika TV halafu wanakwenda kumpekua mtuhumiwa! Jamani! Real
Polisi walitakiwa kufanya kazi zao kimya kimya na kitaalam si kupitia TV kama wanasiasa
Kwa namna yoyote suala zima limechukua sura ya kisiasa na ni ngumu mtu kuamini Mbowe ana makosa hata kama anayo. Polisi wameshafanya kosa na suala zima sasa ni la kisiasa zaidi ya tuhuma
Haya yanafanyika kwa nini? ndio maana wengine tuna hofu kubwa na mustakabali wa Taifa
Upendo, haki utu na ubinadamu sasa ni zawadi tu.
Kinachoonekana ni chuki, visasi na vinyongo. Hakuna taratibu zinaoztuongoza bali utashi tu wa watu
Nakumbuka habari ya kamanda mmoja wa Dar aliyetumika sana kisiasa.
Kesi ilipomkuta akabaki mwenyewe. Wenzake wakihukumiwa kifo alitoka mahakama kuu utadhani siye
Siku hizi ni muumini mzuri sana wa dini, pengine akitubia na kujutia aliyofanya
Kiongozi huyo leo huwezi kumwambia lolote kuhusu haki au dhulma, halali au batili
Sisi si wamoja tena, tumegawanyika, hatuaminiani. Tunaangaliana kama ''maadui'' na si wananchi
Leo akitokea adui wa nje, ni rahisi sana kutuvuruga. Tayari hatuna mshikamano
Tumekuwa Taifa la watu waliobeba vinyongo, chuki na inda vifuani.
Tumekuwa Taifa lisiloheshimu haki za watu, taifa lisilojali upendo. Taifa lisilothamini haki za binadamu
Hatutembei vifua mbele kama Watanzania wa Nyerere, tunatembea vifua vilivyoinuka kwa kujaa chuki, vinyongo, visasi.
Tukae chini na kujiuliza hatma ya haya ni nini? Tunakiachia kizazi kijacho nchi gani?