miaka kadhaa nyuma kumekua na shutuma kwa serikali kufumbia macho masuala kadhaa yenye maslahi kwa taifa likiwemo hili la taifa kuangamia na madawa ya kulevya, ziku za karibuni serikali ya awamu ya nne imejizatiti kutokomeza miongoni mwa majinamizi yaliyokua yanaonekana vikwazo kwenye awamu zilizopita mbali na lile la ufisadi ambalo makomandoo wa chadema walikua wanaliweka mbele kama sera tambulishi kwao, sambamba na hilo shuhuda zinaendelea kutanabaisha kwa kujionea vijana wasanii wa filamu wanamuziki na wafanyabiashara maarufu waliokua wanaonewa haya na awamu zilizopita sasa wanatangazwa mubashara kwa kufanya biashara au kutumia madawa haya.....kilichonisukuma kuandika uzi huu ni pale makomandoo wenzangu wa chadema wanapotoka mapovu eti kwa kutajwa mwenyekiti wa chama chao kwa tuhuma za kujihusisha na ngada....kwani kwa mbowe kua mwenyekiti wa chama pekee kunaweza kumpa utakatifu wa kujitoa kwenye uhusika wa ngada?...kwa ushauri tu tuiweke nchi yetu mbele na si mtu wala kitu tuache mahaba yaliyopindukia ya kiushabiki tu na kama ingekua si kuiweka nchi mbele basi ccm makonda angeanza kumuonea haya ccm zungu na kutokumtaja kabisa...tubadilikeni jamani watu wote ni sawa na wana haki na wajibu sawa kwa jamii sio kunya anye kuku akinya bata kahara....nawasilisha