Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tutakapomaliza kuitia nchi discipline.. Idadi ya m.a.l.o.f.a ilikuwa kubwa sanaViwanda wanajenga lini sasa??
akili za kuambiwa changanya na zakoTundu kawa mtetezI wa ujinga
Mm ni mtu wa ccm lkn naichukia sana ccm kwa sasa kwa sababu ya serikali yake mbovu inayokandamiza na kutesa watu hasa wapinzani pia ubabe na visasi ambavyo havisaidii chochote, wao wanafikiri kwamba wananchi hatuoni kinachoendelea juu ya mbowe pamoja na wengine, tunajua kabisa na tunaona kwamba ni udharirishaji, lakini kwa hali iliyopo kwa sasa na jinsi watu walivyo kasirika magufuli hawezi kurudi ikulu 2020 tuko pamoja nanyi watu wa chadema hadi watu walioko vijijini wanawaunga mkono na wanasema magufuli badala ya kusaidia watu wana dhiki yy yuko busy kukamata wapinzani, ninacho waomba pangeni safu nzuri inayoaminika mbele ya jamii kuanzia mgombea hadi wengine, na pia hakikisheni mjajijenga vizuri hadi vijijini ambako wanadanganywa kwa urahisi. Nawatakia kila la heri.Na Tundu Lissu usiku huu:
Waheshimiwa habari za usiku huu. Naomba kutoa updates juu ya kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama Mh. Freeman Mbowe. Mimi na Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji tumeshuhudia sehemu ya sachi iliyofanyika nyumbani kwa Mwenyekiti kati ya saa tatu unusu na saa sita usiku huu. Kama nilivyosema kwenye ujumbe wangu wa awali, hii sio vita dhidi ya wafanya biashara ya madawa haramu bali ni vita ya kisiasa dhidi ya sisi wapinzani wa CCM na Rais Magufuli. Kwa uthibitisho wa kauli yangu naomba niwapatie orodha ya vitu walivyokamata polisi nyumbani kwa Mwenyekiti Mbowe. Vitu hivyo vimeorodheshwa kwenye fomu na. DCEA 003 inayoitwa 'Hati ya Ukamataji' iliyotolewa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kama ifuatavyo:
(1) Hati moja ya CHADEMA CHASO kwenda kwa Mwenyekiti ya tarehe 16/7/2013
(2) Picha mbali mbali nane za matukio ya uhalifu - picha za wahalifu wanaoharibu mali
(3) Hati moja ya Rasimu ya Kwanza ya CHADEMA kuhusu uundwaji wa Red Brigade
(4) Hati moja ya kurasa 13 inayoongelea mambo ya Muungano.
Hivi ndivyo vielelezo vilivyokamatwa nyumbani kwa Mwenyekiti vinavyothibitisha kwamba yeye ni muuza unga!!! Kama isingekuwa ukweli kwamba hivi ninavyoandika Mwenyekiti wangu yuko mahabusu Central, hiki kingekuwa kichekesho cha mwaka. Lakini Mwenyekiti anasota mahabusu usiku huu. Huu ndio ushahidi ambao Kamanda Sirro na polisi wake wamekuwa wanamtafutia Mwenyekiti wetu kwa amri ya Paul Makonda. Hatuna budi, katika hali hii, kuomboleza - kama alivyofanya Mwalimu katika kitabu chake 'Uongozi Wetu na Hatma ya Tanzania' - juu ya mahali ilikofikishwa nchi hii yetu. Nitawatumia picha ya orodha hiyo shortly.
Update: Mwenyekiti Mbowe aachiwa
Kama tulivyowajuza kwamba iwapo itatokea jambo lolote la umuhimu kujuzana kabla ya asubuhi tutafanya hivyo, tunapenda kuwatangazia wanachama wetu,wadau,wapenzi, na wapenda haki,amani na demokrasia ya kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe ameachiwa huru punde tu mnamo majira ya SAA saba na robo usiku huu.
Tunawashukuri wote kwa sala,maombi na subira na hivyo kuhitimisha salama SAA KUMI za Mwenyekiti wetu kuwa chini ya Jeshi la Polisi nchini katika kituo kikuu cha Polisi jijini Dar es salaam.
Taarifa za ziada juu ya jambo hili zitatolewa kesho.
Salum Mwalim
Naibu Katibu Mkuu
Chadema
The guilty are always affraid !Ilikuwa lazima apatikane na kukamatwa, Ndio maana nashangaa kwa nini ajifiche...
Kama anaona anachofanya ni sahihi kisheria angeendelea na shuguli zake waziwazi sio kujifichaficha
weekend ipi Mkuu? Uko Tanzania kweli wewe?Suala hili linaleta ukakasi sana, ni aibu kwa jeshi la polisi, naomba haki hii ya kuachiwa watu usiku na siku za weekend iwe extended kwa raia wote wa Tanzania na wageni pia
Kwani red brigade ya chadema IPO Kenya??au lile shamba lao la ujasusi lipo bagamoyo ya somalia..?? Humu mnajifanya kuongea..wakishughulikiwa mnasema chuki za kisiasa..nikuulize swali..kipindi cha kampeni ulikuwa unawaona hawa Jamaa na lowasa ofisi za ufipa?? Hilo ndio jumba lao la kukutana..linaitwa ngome..huingii hovyo hovyo..lina CCTV kila kona..lina story ndefu hilo jengoKwenye bandiko la Lizaboni kuelezea kukamatwa kwa Mheshimiwa Freeman Mbowe Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa ameandika, "Wamemkamata akiwa nje ya geti ya Appartment hiyo ambayo ni miongoni mwa majengo ya siri ( Safe House) yanayomilikiwa na CHADEMA" Linaonekana kama ni neno la kawaida sana lakini ni aina ya maneno ya kizushi na yenye lengo maalum la kujenga uhalali wa ama "woga" au "uhalifu" wa Mbowe.
CHADEMA inamiliki "Safe House" kwenye nchi ambayo CCM kila siku wanasema ina amani, kwa nini? Lizaboni anaweza kutueleza hizo "safe House" zinamilikiwa na CHADEMA tangu lini na kwa nini CHADEMA wawe na nyumba za kujifichia? Lakini pamoja na uhuru wa kujieleza humu JF ni kweli inawezekana mtu kutoa shutuma kubwa kama hiyo kienyeji tu bila hata kujazia nyama zitakazoleta uthibitisho wa hoja yake?
Je hili la "Safe House" halifanani na lile la visu vya CUF ambavyo mpaka leo haijulikani vilikuwa vya nani na lile "Kontena" na visu hivyo lilikwenda wapi? kwa nini tunaanza kujenga taswira kwamba kwenye nchi yetu kuna watu ama wanajificha au wana nyumba za kufichama? Halafu watu wana majengo ya siri katikati ya jiji la Dar es salaam? Nikukumbushe Lizaboni, moto huanza na Cheche!!
Kama habari hii ni ya kweli, basi vita imeshaingiliwa na serikali wajiandae kulipa tu fidia, pia wajiandae kuwaomba msamaha wauza ngada wote, inaonesha wauza ngada washafanya yao mapeema!
Unaanzaje kwenda kumpekua mtu kwake ambaye amekukwepa wiki mbili tangu umuweke hadharani kuwa unamuhitaji kwa mahojiano?
Unakwenda kumpekua nini kwa muda huu ambapo mwenyewe kajisalimisha?
Hata kama jamaa anajihusisha kweli, two weeks ni muda mrefu sana kwa muuza ngada kutomkuta na hatia!
Nimelidharau sana wazo la kwenda kumpekuwa nyumbani kwake, hata hivyo tujiulize, kwani biashara hii watu wanafanyia majumbani kwao?
Mbona nchi hii viongozi mnakera namna hii, mnadhani ni vipi mtashinda kesi hii?
Binafsi naona kama haijakaa sawa.huyu ni kiongozi mkubwa wa upinzani hapa TZ.anadhalilishwa namna hii,na itakuwaje endapo watagundua tuhuma za kuhusika kwake na madawa ya kulevya si za kweli?mtakua mmempotezea muda,mmeharibu jina lake kwenye jamii,na tena mmemdhalilisha.haipendezi kabisa.tuliichagua na kuiamini serikali iliyoko madarakani ili kutuletea maendeleo,kushughulika na kero za wananchi,wala sio kufanya haya yanayoendelea.ukweli ni kwamba kama haya yataendelea basi 2020 ccm mtapata kura za mapunguani tu.hakuna mtu atawachagua tena.tuleteeni maendeleo tumechoka na haya mnayoyafanya mnapoteza muda tu!
Wewe tetra werevu basi.For once acheni chuki za kupandikizwa ,tufanye siasa siyo chuki wala visasi.
.... Ulofa ni kipaji aiseeTundu kawa mtetezI wa ujinga
Na anatetea kijinga pia !Tundu kawa mtetezI wa ujinga
Nimekudharau sana kutumia muda wako kuanzisha thread kwa ajili ya comedian Lizaboni.Kwenye bandiko la Lizaboni kuelezea kukamatwa kwa Mheshimiwa Freeman Mbowe Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa ameandika, "Wamemkamata akiwa nje ya geti ya Appartment hiyo ambayo ni miongoni mwa majengo ya siri ( Safe House) yanayomilikiwa na CHADEMA" Linaonekana kama ni neno la kawaida sana lakini ni aina ya maneno ya kizushi na yenye lengo maalum la kujenga uhalali wa ama "woga" au "uhalifu" wa Mbowe.
CHADEMA inamiliki "Safe House" kwenye nchi ambayo CCM kila siku wanasema ina amani, kwa nini? Lizaboni anaweza kutueleza hizo "safe House" zinamilikiwa na CHADEMA tangu lini na kwa nini CHADEMA wawe na nyumba za kujifichia? Lakini pamoja na uhuru wa kujieleza humu JF ni kweli inawezekana mtu kutoa shutuma kubwa kama hiyo kienyeji tu bila hata kujazia nyama zitakazoleta uthibitisho wa hoja yake?
Je hili la "Safe House" halifanani na lile la visu vya CUF ambavyo mpaka leo haijulikani vilikuwa vya nani na lile "Kontena" na visu hivyo lilikwenda wapi? kwa nini tunaanza kujenga taswira kwamba kwenye nchi yetu kuna watu ama wanajificha au wana nyumba za kufichama? Halafu watu wana majengo ya siri katikati ya jiji la Dar es salaam? Nikukumbushe Lizaboni, moto huanza na Cheche!!
Nadhani aliongelea Good news baada ya kuachiwa. Cc lizaboniWapinzani kunyanyaswa ni good news hebu fafanua