Mchanganuo wa video clip hii kwa nionavyo:-
1. Wema hajakanusha kwamba hahusiki na madawa yakulevya -moja kwa moja yuko guilty!.
2. Anategemea favor, influence ya mfumo kumweka huru. .
3. Anasema wazungu wameachiwa mbona wao ndio wamebaki, kwa hiyo anataka aachwe huru waendelee kama watakavyo.
4. Anataja na mateja wengine "Agness".
5. Nimegundua shule ni ufunguo wa maisha.
a) mtu gani mweye elimu yake japo kidogo angesema "tumesikia anataka uwaziri....". Huu si ujuhan sana? Kutaka uwaziri kwa mtu na kushindwa kujitetea kwa mtuhumiwa kuna husiana nini? Kwa hiyo aachwe tu aendelee kuua watu kwa sababu hakuna kiongozi anayeonyesha kujali? Uwaziri wa Makonda utakuja kwa kazi zake, lakini hakuna uzalendo wa mtu utathibitiska kwa kuwaogopa waharifu kwa sababu wana macho ya kutisha.
b). Sijawahi kufikiria mtu katila level hii, anaweza kuwa na akili za kitoto kwamba fulani mbona kaachwa? Akidhani kwamba kwa kuwa mwingine hajakamatwa kwa kuwa ni "mwanamke wa rc na kamjengea nyumba sijui kampangishia nyumba makongo", kutapelekea kumwondolea hatia ya mashitaka.
Nani washauri wa Wema? Mbona mnawamcha anaangamia huku mkiona? Mpeni maarifa na hekima basi japo kidogo. Au na wshauri wake ni wa kiwango cha ngono, kujionyesha na kugombana tu?
Pole kwa Watanzania wote!