DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Utakuja kuuliwa kwa upuuzi wako..mtu hana kitambulisho yeyote alafu unamruhusu kuingia ndani..!?umekosea sana mkuu.usirudie tena.
 
ndugu mwananchi je uko mkoa gani ulikopata hiyo kadhia? kwa upande wa dawasco wasoma mita wetu wanavaa shati la blue au jeupe na huwa na vitambulisho vya kazi au permit job kwa wale vibarua. tafadhali wakati mwingine usisite kuwasiliana nasi kupitia huduma kwa wateja dawasco 0800110064 kama una mashaka na msoma mita wako.
 
Kama mteja wa Dawasco ninakerwa na utaratibu mbovu wa huduma kwa wateja Dawasco Kimara.

1. Mafundi aina ya vibarua ambao mmekuwa mkiwatumia kuunganishia maji wateja wapya, hawa watu wanaokuja kwa wateja ni kero, kama mteja tayari nimelipa gharama zote ofisini kwenu, mnamtuma fundi wenu kwangu ( Mteja), Kitu cha kwanza ataomba namba simu ikishampa namba kinachofuata ni kuomba hela ya nauli. Utasikia boss nilipangiwa kuja kukufungia maji lakini sina nauli hivo ningeomba unitumie nauli. Hii ni kwa wale wanaokuja Field.

2. Ofisini Kama mteja nimelipa bili ya maji kupitia benki au Max malipo ninapokuja kuleta risiti ofisini utasikia tena nenda katoe photo copy pale nje. Kumbuka tayari nimelipa na nimekuletea risiti ni jukumu lako kuingiza risiti yangu kwenye system na kunigongea mhuri wa kuonyesha umepokea then mimi niondoke. Kama hiyo haitoshi nimeshaenda kutoa copy nimekuletea na ninaasume kuwa nimemaliza.

Ajabu utaona record hazionyeshi deni kupungua zaidi ya kuongezeka, unapoamua kurudi Dawasco utaulizwa hivi ulileta risiti? Jibu ni ndiyo hapo tena utaambiwa hebu katoe copy ya hizo copy za risiti uniletee, ahaaaa how many times should I do this?

Mimi kazi yangu ilikuwa nikulipa na kukuletea risiti siyo jukumu langu tena kwenda kutoa copy ya risiti.
 
Dawasco sio wabunifu kabisa, eti wana afisa biashara, sijui hata kazi yake ni nn wakati kuna nyumba nyingi tuu wangeweza kutuunganishia maji wapate mapato makubwa. Hili shirika sijui kama lina viongozi wasomi, maeneo ya hapa mbezi beach jogoo juu mpaka kinzudi kuelekea goba ni hela ngapi wangepata? Eti tunamtua mwanamke ndoo kichwani, uongo mtupu! Wake up!
 
Kula tano mkuu, yale yale ya kufanya kazi kwa mazoea, sidhani toka lianzishwe hili shirika kama limewapa serikali faida! Ni hasara mwanzo mwisho, yote sababu hata wakipata hasara mishahara iko pale pale, lianze kuendeshwa kifaida, watu sales wakae ki commission, hakuna sales, hakuna malipo, wakipata hasara ile kwenye mishahara yao na retrenchment juu, utaona watakavyopiga kazi..
 
Nimetoa maombi/maoni yangu haya tangu tarehe 23/06/17 kuhusu maji Makoka lakini mpaka leo majibu hola. Mtumishi wa DAWASCO anayejibu hoja/maombi anaonekeana anaingia hapa kwenye huu uzi na kutoka lakini hajibu hoja sijui ni kwa nini. Hii inapoteza umuhimu wa uzi. Nafikiri ni muda muafaka sasa kama alivyosema mchangiaji hapo juu kuwa serikali iondoe ruzuku kwenye mashirika kama DAWASCO, NHC, TANESCO, ATCL ili yajiendeshe kibiashara bila kutegemea serikali ndipo wafanyakazi walau watachangamka. Kwa jinsi ilivyo sasa watu wanajua mishahara ipo tu hawawezi kufanya kazi kwa ufanisi.Maji na umeme vikiunganishwa kwa watu wengi zaidi wananchi watalipia hivyo zitapatikana pesa za kuendesha haya mashirika.
 
Kwanza napenda kuwapongeza sana DAWASCO kwa utaratibu huu mzuri sasa hebu tuelezen barabara ya Goba ya mbezi mnaleta maji lini?
 
DAWASCO niwaulize hii thread mmeiweka ya nini basi mbona hamtoi majibu ya malalamiko ya watu humu
nimeandika wee kuhusu tatizo la maji ya Dawasco k

Bunju B njia ya kwenda Mabwepande karibu na Nyumba za mradi wa Nyumba za watumishi wa serikali TBA ,mbona mko kimya..wenzenu tunaumia tunateseka maji ni ya taabu,tujibuni basi kuliko kukaa kimya..au mpaka tukamuone Mh Raisi ndo mtakuja
 
Pole sana Kapuchi. Mimi mwenyewe nimeulizia maji Makoka kwa Mkuwa mpaka leo karibu mwezi hakuna majibu.Tumejaza fomu tangu mwaka jana mwishoni lakini mpaka leo hatujaunganishiwa maji. Baada ya kupata majibu yasiyoridhisha kutoka kwa meneja wa tabata nikaona walau hapa jamvini nitapata majibu sahihi lakini wapi. Mjibu hoja wa dawasco anaonekana anaingia hapa kwenye huu uzi na kutoka lakini hajibu chochote kwa ujumla hamna mrejesho. Ni wakati sasa kwa engineer Luhemeja kuja mwenyewe kutupatia majibu ya hoja zetu. Ni niwaombe tena serikali iyape muda haya mashirika ikifika mwaka fulani mwezi fulani yajitegemee kwa kila kitu yasipewe ruzuku hata shilingi moja yaipunguzie serikali kuu mzigo hapo ndipo watafanya kazi tofauti na sasa utendaji wao unalegalega. Hivi inashindikina nini kwa Dawasco kwenda kujifunza kidogo kwa Tanseco japo wao hawajafanya vizuri lakini walau kazi yao inaonekana na hata uzi wao humu jamvini upo active kiasi.
 
Hili shirika DAWASCO limeoza kuanzia chini mpaka juu, yaani ni kufumua uongozi wote, kuhakiki vyeti, kuweka management structures mpya kabisa na za kisasa, sio wale wapuuzi wa enzi za SU na kutumia magari kubeba migomba!
Likirekebishwa hili laweza kuitengenezea hela serikali ya magufuli hela kuliko madini yetu! Ndio..
Asilimia 85-90 ya miili yetu ni maji, tunaweza kuishi bila kula nyama, kuku, samaki au wali au ugali, LAKINI SIO MAJI, WANASHINDWA KIVIPI??!!!πŸ™πŸ™πŸ™πŸ˜‘πŸ˜‘πŸ˜‘
 
Kwa kweli Dawasco mnapaswa kutubu na kubadilika.....vilio vya watu wenye kero za maji ni vingi
mimimnawashauri kwa kuanzia shighulikieni malalamiko ya wadau walioowaelezea kero zao humu ndani kwenye hii thread kama kweli mna nia ya dhati ya kutatua kero za maji katika mji wa Dar es Salaam
kinachotuudhi ni kuwa mmeweka hii thread tutoe malalamiko,mapendekezo na adha zetu ,lakini aliyeweka uzi huu hatuambii chochote amekaa kimya kuhusu kero hizo
sasa tunajiuliza hii thread ni ya nini...au malengo yenu ya kuianzisha ni nini
 
Mna mpango gani wa kusambaza maji kwa wakazi wa Mbezi Msakuzi na Mpiji?
 
Kwakweli ninyi ni jipu mnastahili kuvunjwa kwa kugeuza maji kuwa ni kitegauchumi na sio necessity kwasababu mmepsndisha bei mara dufu na kuyafaya maji kuwa ni ghali mno, sijui hivyo vigezo vya bei mnavitoa wapi, mdhibiti nae amekuwa mfu asie na memo. Hamkustahili kuyageuza maji kuwa dhahabu. Hivi hii nchi ingekua jangwa ingekuaje? Na hapo ni watanzania wasiozidi asilimia 20 tu ndio wanatumia maji ya bomba, vipi watakapofikia asilimia 95 kama misri.??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
maji yanakatika sana kwa wiki ayaweza toka mara 3 usiku tu au mara 1 asubuhi mwezi sasa,mna nini?
 
Wakazi wa Salasala tulikuwa na ushirika wa watumia maji salasala, ushirka huu uliweza kutupatia maji mara tatu kwa wiki. mwaka jana tukarudishwa dawasco, imekuwa shida tunapata maji mara moja kwa wiki siku ya jumapili, mbaya zaidi maji mara kwa mara wanatoa kwa muda mfupi siku hiyo ya jumapili haizidi masaa matatu. sasa inabidi tununue kwa wenye magari, tunajiuliza mfungua maji ana uhusiano na wauza maji kwenye magari. hebu fuatilieni na sisi tunafuatilia tukipata ukweli tutweka wazi humu humu kwenye JF.
 
Nimelipa kuunganishiwa maji tokea tarehe 29/05/17 Kwa ajili ya kuunganishiwa maji. Lakini mpaka leo sijaunganishiwa, nimeenda DAWASCO Boko nimeambiwa hawana mipira ikiwa tayari watanipigia.
Kama mnajua kuwa mipira haitoshi kwanini mnawaambia wateja walipe??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…