Habari za mida hii wanajamvi.
Bila kuwachelewesha niende kwenye mada. Hawa vijana wanaosoma mita kwakweli Mimi binafsi wananichanganya mana juzi nilipata dharura kidogo nikawa nimerudi kwangu mapema, in fact nilirudi baada Tu ya kufika kazini, lakini cha kushangaza mida ya SAA 7 mchana alikuja kijana aliyejitambulisha kama amekuja kusoma mita, Mimi nilikua ndani lakini mke wangu aliyemfungulia aliwahi ndani kuniambia hebu njoo umuone huyu anayedai in msoma mita mbona kama hafananii.
Nilipotoka kwenda kumuona nilielewa mke wangu alichokua anasema maana alikua amevaa jeans na T-shirt na smart phone Tu ndio anatumia, sasa nikashangaa Hamna uniform, Hanna kitambulisho, Hanna chochote, halafu ukiangalia midomo yake niliona ni mtumiaji wa mihadarati maana mdomo umeungua, sasa Mimi sikutaka kuanzisha kitu halafu ikawa tofauti, nikammark halafu akaenda.
Hivi ndivyo wanavyokuwa hawa wasoma mita au huyu wa kesi yangu hakuwa mtu wa idara ya maji kweli
Inabidi idara ya maji wafanye mchakato wa kufanya vijana wao wafahamike vizuri maana Mimi ngeweza kumfungulia mbwa halafu ikaja kuwa kesi