DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Yaani kunakuwa na likeji za maji mpaka zinakela. Kuna madimbwi ukiona utadhani ya mvua, lakini mvua haijanyesha kwanini? Kumbe ndio likeji zenu za maji. Jamani ebu waache kufanya kazi kwa mazoea. Pili hii mitalo ya kufukia mabambo mnachimba mifupi mmno jamani, sm 30!!
 
Habari, dawasco tabata shule wanagoma kupokea risiti ya malipo kisa ni ndogo wanataka zile kubwa, nililipia crdb mini-branch, ni shilingi elfu 50 sasa Najiuliza ina maana elfu 50 yangu ndo imekwenda na maji au?
 
DAWASCO Tunashukuru kwa huduma yenu Je Maeneo ya Kimara suka MOA/Arsenal kuelekea Saranga maji yatafika lini?Tumeshajaza fomu Surveyor kaja ila hatuoni maendeleo yeyote
 
Habari Comrades..

Mara kadhaa watu wa Dawasco wa ofisi ya Kimara wamekuwa na tabia za ajabu kabisa.
Wanapita mitaani wanapoishi Wananchi wakikuta sehemu maji yanavuja (leakage) au bomba limekatika, badala ya kuparekebisha, wanachimba wanakata maji.

Wanajua mhusika wa hilo bomba lazima atajitokeza ili waende wajadiliane nae kuhusu matengenezo ya bomba husika. Hapo utaambiwa sijui zinatakiwa konekta, sijui mpira na vifaa vingine kibao. Bado hapo hawajasema hela yao..
Rushwa tupu.

Kwanini mnapoyazungukia mabomba yenu msiyatengeneze ili huduma isisimame kwa wateja?? Kwanini gharama ya matengenezo adaiwe mteja wakati mabomba mengi yanaharibika kutokana na Miundombinu mibovu ya Dawasco wenyewe hasa mara baada ya kipindi cha mvua??? ?

Naomba wahusika waimulike Dawasco ya Kimara. Pamejaa uzembe na rushwa tupu.
 
Dawa yao iko jikoni mkuu kashamla kichwa bosi wao kiaina jana akiwa pwani rungu hili litawafikia mpaka hawa wafunga koki maana ndio wasumbufu sana.
 
ndugu mteja namba zetu zinapatikana siku zote kwa saa 24. tafadhali wasiliana na huduma kwa wateja dawasco 0800110064
Issue sio kwamba hazipatikani, bali mara nyingi huita bila kupokelewa!
 
Hivi kweli Dawasco mmeshindwa kusambaza maji mbezi ya kimara????? Yaani maji yanaishia barabara. Kuu ya lami tu ukiingia ndani kidogo tu mabomba gani yake sijui mmeweka vyembamba seriously??? Vinajipasukia vyenyewe tu....

Halafu mnajitanabainisha kuwa shida ya maji itakuwa historia [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] ..
 
Hivi DAWASCO mbona nikipiga simu maji yanavuja inakuwa kama nawakera? Lakini nikichelewa tu kulipa bili ya Mwezi siku tatu mmeshakata Maji???
tafadhali tujulishe eneo lenye uvujaji nasi tutaifanyia kazi
 
Nawashukuru sana kwa huduma ya malipo kwa mtandao.
Kule Bagamoyo nalipia huduma kwa ufanisi mkubwa, na nileo tu nimelipia bili yangu baada ya kukumbushwa kwa sms!
Mnatumia mtandao kwa ufanisi mkubwa!
 
DAWASCO kuna engineer wenu Bagamoyo anatuzinguwa sana BunjuB, anataka rushwa ili eti aje kufanya estimates! Tushafanya maombi na kila kitu ni yeye aje tu kupima, kutandandazwe mabomba mangapi na wapi na ufundi, huyu bwana twataka kumpambanisha na takukuru kabisa, analeta zile za nyuma bila rushwa hafanyi kazi..Tusaidie mkuu..
 
SISI MAKOKA KISUKURU KWA MKUWA MNATUFIKIRIAJE MAANA TUMEACHWA KAMA KISIWA VILE. MAJI YALIYOTOKEA MAKOKA MWISHO YAMEISHIA KWA KISANGA. MAJI YALIYOTOKA MAJI CHUMVI YAMEISHIA SHULE YA MOUNT ZION YAKAELEKEA JUMBA LA DHAHABU. SISI TULIOBAKI HAPO KATIKATI KWANZA TUPO TAYARI KULIPIA KUUNGANISHIWA BILA HATA YA MKOPO. TUMESHALIPA NA RISITI TUNAZO TOKA MWAKA JANA MWISHONI. SURVEYOR AMESHAPITA MARA KIBAO HAKUNA CHA MAANA. TUMESHAEENDA KWA MENEJA WA TABATA MARA KIBAO LAKINI HAKUNA JIBU LOLOTE LA MAANA. KWA HIYO TUNAOMBA MUKURUGENZI WA DAWASCO ENGINEER LUHEMEJA KAMA YUPO JAMII FORUMS AFIKE MAKOKA KWA MKUWA LABDA TUTAPATA MAJI.
 
Habari za mida hii wanajamvi.

Bila kuwachelewesha niende kwenye mada. Hawa vijana wanaosoma mita kwakweli Mimi binafsi wananichanganya mana juzi nilipata dharura kidogo nikawa nimerudi kwangu mapema, in fact nilirudi baada Tu ya kufika kazini, lakini cha kushangaza mida ya SAA 7 mchana alikuja kijana aliyejitambulisha kama amekuja kusoma mita, Mimi nilikua ndani lakini mke wangu aliyemfungulia aliwahi ndani kuniambia hebu njoo umuone huyu anayedai in msoma mita mbona kama hafananii.

Nilipotoka kwenda kumuona nilielewa mke wangu alichokua anasema maana alikua amevaa jeans na T-shirt na smart phone Tu ndio anatumia, sasa nikashangaa Hamna uniform, Hanna kitambulisho, Hanna chochote, halafu ukiangalia midomo yake niliona ni mtumiaji wa mihadarati maana mdomo umeungua, sasa Mimi sikutaka kuanzisha kitu halafu ikawa tofauti, nikammark halafu akaenda.

Hivi ndivyo wanavyokuwa hawa wasoma mita au huyu wa kesi yangu hakuwa mtu wa idara ya maji kweli

Inabidi idara ya maji wafanye mchakato wa kufanya vijana wao wafahamike vizuri maana Mimi ngeweza kumfungulia mbwa halafu ikaja kuwa kesi
 
ulishindwaje kumuomba kitambulisho? na kukipiga picha halafu uwaulize idara ya maji juu ya huyo mtu...

kama hujafanya hayo basi utakuwa hujapevuka kiakili na hudeserve kuwa na mke...
 
Kama ni msoma mita wa DAWASCO wapo humu watapita wakujibu mkuu kwamba wasoma mita wanatakiwa wawe na vigezo gani.
 
Habari za mida hii wanajamvi.

Bila kuwachelewesha niende kwenye mada. Hawa vijana wanaosoma mita kwakweli Mimi binafsi wananichanganya mana juzi nilipata dharura kidogo nikawa nimerudi kwangu mapema, in fact nilirudi baada Tu ya kufika kazini, lakini cha kushangaza mida ya SAA 7 mchana alikuja kijana aliyejitambulisha kama amekuja kusoma mita, Mimi nilikua ndani lakini mke wangu aliyemfungulia aliwahi ndani kuniambia hebu njoo umuone huyu anayedai in msoma mita mbona kama hafananii.

Nilipotoka kwenda kumuona nilielewa mke wangu alichokua anasema maana alikua amevaa jeans na T-shirt na smart phone Tu ndio anatumia, sasa nikashangaa Hamna uniform, Hanna kitambulisho, Hanna chochote, halafu ukiangalia midomo yake niliona ni mtumiaji wa mihadarati maana mdomo umeungua, sasa Mimi sikutaka kuanzisha kitu halafu ikawa tofauti, nikammark halafu akaenda.

Hivi ndivyo wanavyokuwa hawa wasoma mita au huyu wa kesi yangu hakuwa mtu wa idara ya maji kweli

Inabidi idara ya maji wafanye mchakato wa kufanya vijana wao wafahamike vizuri maana Mimi ngeweza kumfungulia mbwa halafu ikaja kuwa kesi

Unamuingizaje mtu ndani bila kukuonyesha id mkuu

nahofu kuendeleza zaidi maana n kosa kubwa
 
Haidhuru kitu.

Ada ya maji humlipi yeye.
Siku nyingine unaweza ukamuuliza tu kama ana ID.

Toka utoto wangu nilikuwa naona watu wa kusoma meter ya maji wanakuja home wamevaa kawaida kawaida tu.
 
Back
Top Bottom