DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Hahahaha vumilia tu, maji muhimu sana,

Hawa DAWASCO wanachofanya sio kabisa, utashangaa na Siku ya Leo inapita tena

au ndiyo maana leo nawaona Watu wengi sana hapa Coco Beach Mkuu au wengi ndiyo wamekuja ' Kuunganisha ' huku huku na wakirudi makwao wanafikia Kulala tu?
 
au ndiyo maana leo nawaona Watu wengi sana hapa Coco Beach Mkuu au wengi ndiyo wamekuja ' Kuunganisha ' huku huku na wakirudi makwao wanafikia Kulala tu?
Beach zitajaa Leo, wengine Msasani Beach

halafu bado wapo kimya mpaka sasa hivi

Wengine watae
 
Mkuu Mimi Niko kimara,,nataka kuunganisha maji,,tatizo kunawatu walinunua bomba likapita maeneo ya jirani kwangu,,naambiwa kabla sijaunga maji niwaone hao niwalipe,,,je ni halali kuwalipa ili waniruhusu kuunga maji kwangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)
MBONA MBWENI KIJIJINI WATU HAWAJAUNGANISHIWA MAJI LICHA YA KUTUMIA MUDA KARIBU MWAKA MZIMA KUFUATILIA !!! MPAKA INATIA SHAKA ILHALI BOMBA ILIKOISHIA HAIFIKI HATA NUSU KILOMETA!!! JE MNAWASAIDIAJE WAKAZI HAO??????
 
...mmekata maji bila taarifa tangu tarehe 24, mnatutesa sana, not good service not fair at all....
 
Tunalipia huduma kuunganishiwa maji safi, lakini baada ya malipo mnaanza maelezo meengi sana kwamba vifaa hakuna, mara mita hakuna mara mabomba hakuna.

Basi tumesema sasa mje tuu muunganishe maji kama mabomba tunanunua wenyewe nayo pia hamtaki. Hebu tuelezeni tuwaeleweje.

Siku zinazidi kwenda hatuoni maji wala chochote, kabla hatujalipia mlikuwa marafiki baada ya kulipia hamuonekani.
 
Dawasco inabidi mbadilike kiutendaji. Mpo slow hamuendani na kasi ya JPM, bomba linavuja wiki sasa hapa mbezi beach jogoo hakuna jitihada za kuziba pamoja na kuripoti kwenu. Huyo CEO Lugemeja ni bomu pia, anasema namba zinapatikana kwa mameneja uongo mtupu
 
DAWASCO mna mpango gani wa kutuletea maji Mbezi Makabe?? Hamna hata dalili!

Maeneo mengine yanapendelewa sana kama Mbezi Beach ila huku kwetu Mbezi Makabe mbona hamtufikirii?

Kuna changamoto gani kutuletea Maji Mbezi Makabe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mteja wa Dawasco ninakerwa na utaratibu mbovu wa huduma kwa wateja Dawasco Kimara.
1. Mafundi aina ya vibarua ambao mmekuwa mkiwatumia kuunganishia maji wateja wapya, hawa watu wanaokuja kwa wateja ni kero, kama mteja tayari nimelipa gharama zote ofisini kwenu, mnamtuma fundi wenu kwangu ( Mteja), Kitu cha kwanza ataomba namba simu ikishampa namba kinachofuata ni kuomba hela ya nauli. Utasikia boss nilipangiwa kuja kukufungia maji lakini sina nauli hivo ningeomba unitumie nauli. Hii ni kwa wale wanaokuja Field.

2. Ofisini Kama mteja nimelipa bili ya maji kupitia benki au Max malipo ninapokuja kuleta risiti ofisini utasikia tena nenda katoe photo copy pale nje. Kumbuka tayari nimelipa na nimekuletea risiti ni jukumu lako kuingiza risiti yangu kwenye system na kunigongea mhuri wa kuonyesha umepokea then mimi niondoke. Kama hiyo haitoshi nimeshaenda kutoa copy nimekuletea na ninaasume kuwa nimemaliza.

Ajabu utaona record hazionyeshi deni kupungua zaidi ya kuongezeka, unapoamua kurudi Dawasco utaulizwa hivi ulileta risiti? Jibu ni ndiyo hapo tena utaambiwa hebu katoe copy ya hizo copy za risiti uniletee, ahaaaa how many times should I do this?

Mimi kazi yangu ilikuwa nikulipa na kukuletea risiti siyo jukumu langu tena kwenda kutoa copy ya risiti.
 
Kwa kweli hili ni tatizo ukizingatia kunaadministration fees/charges tunayolipa, je kazi ya hii pesa ni nini? Tatizo lingine lipo kwa hawa technicians, yaani mtu anakuja kukagua mtaro ili alete bomba na kuleta bomba ila kuja kuunganisha ni kasheshe! Unaweza kukaa zaidi ya mwezi ukisubiri kuunganishiwa maji wakati bomba umeshafukia tena kwa gharama zako. Kila siku ukimpigia atakuambia nimeshamtuma fundi na anakupatia namba ya fundi. Ukimpigia fundi anakuambia je una vifaa?!!! Atadai kuwa ni kweli technician kampamaagizo isipokuwa hajampa vifaa!
 
Je kwa nini DAWASCO hailengi kuongeza wateja wapya na badala yake inahangaika na wale wale wa siku zote? Hamuoni kuwa kuna fedha nyingi mnaziacha kwa potential customers ambao wanashindwa kupata huduma zenu kwa vile tu hamuendi kwa wananchi?

Fikiria maeneo kama Mbagala Gongolamboto, Kigamboni nk sidhani kama mmeyafikia maeneo hayo
Maeneo mapya wakati haya maeneo ya zamani maji hayatoki? Ule mradi mkubwa wa maji umeishia wapi maana tuliambiwa maji ni mengi ya kupasua mabomba lakini mitaani maji bado ni tatizo kuna maeneo maji yanatoka Mara moja kwa wiki.
 
kipindi hiki maji Ya dawasco ni machafu, yanaharufu Ya kutu jayafai Kunywa hata baada Ya kuyachemsha
 
Back
Top Bottom