DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Hahahaha vumilia tu, maji muhimu sana,

Hawa DAWASCO wanachofanya sio kabisa, utashangaa na Siku ya Leo inapita tena

au ndiyo maana leo nawaona Watu wengi sana hapa Coco Beach Mkuu au wengi ndiyo wamekuja ' Kuunganisha ' huku huku na wakirudi makwao wanafikia Kulala tu?
 
au ndiyo maana leo nawaona Watu wengi sana hapa Coco Beach Mkuu au wengi ndiyo wamekuja ' Kuunganisha ' huku huku na wakirudi makwao wanafikia Kulala tu?
Beach zitajaa Leo, wengine Msasani Beach

halafu bado wapo kimya mpaka sasa hivi

Wengine watae
 
Mkuu Mimi Niko kimara,,nataka kuunganisha maji,,tatizo kunawatu walinunua bomba likapita maeneo ya jirani kwangu,,naambiwa kabla sijaunga maji niwaone hao niwalipe,,,je ni halali kuwalipa ili waniruhusu kuunga maji kwangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MBONA MBWENI KIJIJINI WATU HAWAJAUNGANISHIWA MAJI LICHA YA KUTUMIA MUDA KARIBU MWAKA MZIMA KUFUATILIA !!! MPAKA INATIA SHAKA ILHALI BOMBA ILIKOISHIA HAIFIKI HATA NUSU KILOMETA!!! JE MNAWASAIDIAJE WAKAZI HAO??????
 
...mmekata maji bila taarifa tangu tarehe 24, mnatutesa sana, not good service not fair at all....
 
Tunalipia huduma kuunganishiwa maji safi, lakini baada ya malipo mnaanza maelezo meengi sana kwamba vifaa hakuna, mara mita hakuna mara mabomba hakuna.

Basi tumesema sasa mje tuu muunganishe maji kama mabomba tunanunua wenyewe nayo pia hamtaki. Hebu tuelezeni tuwaeleweje.

Siku zinazidi kwenda hatuoni maji wala chochote, kabla hatujalipia mlikuwa marafiki baada ya kulipia hamuonekani.
 
Dawasco inabidi mbadilike kiutendaji. Mpo slow hamuendani na kasi ya JPM, bomba linavuja wiki sasa hapa mbezi beach jogoo hakuna jitihada za kuziba pamoja na kuripoti kwenu. Huyo CEO Lugemeja ni bomu pia, anasema namba zinapatikana kwa mameneja uongo mtupu
 
DAWASCO mna mpango gani wa kutuletea maji Mbezi Makabe?? Hamna hata dalili!

Maeneo mengine yanapendelewa sana kama Mbezi Beach ila huku kwetu Mbezi Makabe mbona hamtufikirii?

Kuna changamoto gani kutuletea Maji Mbezi Makabe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 

Kwa kweli hili ni tatizo ukizingatia kunaadministration fees/charges tunayolipa, je kazi ya hii pesa ni nini? Tatizo lingine lipo kwa hawa technicians, yaani mtu anakuja kukagua mtaro ili alete bomba na kuleta bomba ila kuja kuunganisha ni kasheshe! Unaweza kukaa zaidi ya mwezi ukisubiri kuunganishiwa maji wakati bomba umeshafukia tena kwa gharama zako. Kila siku ukimpigia atakuambia nimeshamtuma fundi na anakupatia namba ya fundi. Ukimpigia fundi anakuambia je una vifaa?!!! Atadai kuwa ni kweli technician kampamaagizo isipokuwa hajampa vifaa!
 
Maeneo mapya wakati haya maeneo ya zamani maji hayatoki? Ule mradi mkubwa wa maji umeishia wapi maana tuliambiwa maji ni mengi ya kupasua mabomba lakini mitaani maji bado ni tatizo kuna maeneo maji yanatoka Mara moja kwa wiki.
 
kipindi hiki maji Ya dawasco ni machafu, yanaharufu Ya kutu jayafai Kunywa hata baada Ya kuyachemsha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…