DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASCO, sijapata jibu la Swali Langu Zaidi ya Wiki Mbili Sasa. U spesheli wa Uzi huu ni nini??

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama zile No tu ukipiga unaambiwa nenda ofisini itakua huku jf???
Sijaona huduma mbovu kama za hawa watu
Calculator zinazofanya hesabu za bili zao sijui ni za mwaka gani
 
SINA IMANI KABISA NA WASOMA MITA WA DAWASA PWANI
Mimi ni mteja mzuri wa DAWASA na nalipa bills zangu za maji kila mwezi.Jambo la kushangaza ni gharama ninazoletewa ni kubwa mno kulingana na matumizi ya kawaida kabisa hapa nyumbani. Nilichogundua hawa wasomaji wa mita wanabambikia badala ya kusoma units halisi zilizotumika kwa mwezi husika kama ni units 5 yeye anaongeza anazojua yeye.Hasa DAWASA Pwani ni wazembe mno mabomba mengi yanavujisha maji kwa wingi na maji mengi yanapotea lakini hawajali kabisa na mara nyingi wanapita na bajaji zao na wanaona lakini no action taken.Ili kuthibitisha haya ninayoongea DAWASA HQ tumeni wapelelezi wenu waje kuona uzembe wa watendaji wa DAWASA Pwani.Eneo nalozungumzia ni hapa P/Ndege hii barabara ya MAGEREZA njooni nayo hadi hapa shule ya msingi Twendepamoja muone maji yanavyopotea. Kuna uwezekano tunabambikiwa bills kufidia maji yanayopotea kwa kuvuja,haiwezekani mimi matumizi ya kawaida na hakuna sehemu inayovuja hapa kwangu halafu niletewe bill ya Tshs 40,000/= haki ya Mungu nitakwenda kwa Mh. Mbarawa kwenda kumueleza haya madudu nina access ya kumuona na nitamueleza utendaji mbovu wa DAWASA Pwani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Meneja mkuu nisaidie kibaha pwani wamenibambikia unit 100 hewa ambazo wanasema za mita ya zamani ?kuthibitisha wameshindwa but wanalazimisha shs 165,000/= zilipwe na hata meneja kaandikiwa barua 2 hajibu.Hivi nyie mkoje?ankara zaonyesha nalipa vema bill za @ nwezi 2018/19 na sidaiwi.Naomba ajitokeze mtu mmoja aliye na Mungu atatue hili,asante a/c 28317201 mwendapole
Tel 0776380301/0679811266

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanaomba kuunganishiwa maji kwa matumizi ya ndani, lakini matumizi yao ni kwa ajili ya kuuza. Mnawatambuaje hao? Wapo wengi sana sizani kama mnawatambua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
DAWASA
Ni wiki 2 tangu complain yangu # 644 itoke na hamjatoa jibu lolote, sijui tuwape jina gani ninyi mnaotesa jamii kwa kuwabambikia unit wateja ili muonekane mnakusanya mapato makubwa???? Shame

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Head office yenu kuna mdada mweupe reception mfupi hajui kujibu wateja na wala hatoi msaada pili kuna mdada ndani ni bosi wao yupo chumba pekee yake ukienda kwake hana mda na mtu utakaa kwenye viti lakini yeye yupo kuangalia internet

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimelipa bill Dawasco Kawe tarehe 13/02/2020 sidaiwi hata kidogo

Lakini jana wamepita mafundi wa Dawasco wamekata maji kwenye kianzio cha maji mtaa mzima , ili fundi wa Dawasco aje kuludisha wanataka nilipe elfu 60 DAWASA wakati wamekata wakati Mimi sidaiwi

Kwa hiyo mmekua Mkikata hata kwa waliolipa ili mkusanye elfu 60 60 za ufundi , wakuu hii si ni Rushwa hii ? Hamuogopi hata serikali ya Maghufuli
 
Nakaa Mikocheni kwa Warioba mtaa daima leo ni siku ya kumi na moja maji hayatoki kuna tatizo gani? Hii hali haivumuliki jamani ni mbaya mno basi mtuletee maji hata kwa bozzer
 
Dawasa tupeni majibu kuhusu mgao wa maji maeneo haya ya kimara baruti
maana yakitoka maji siku moja inawalazimu mkae siku tatu bila maji.
sasa swali langu ni hili.
Hii vita yakupambana na corona tutaiweza kweli?

Au waziri wa afya anapotangaza kunawa na maji tiririka kila wakati je mmeshamwambia kuhusu huu mgao?

Hamuoni kwamba mnachangia kurudisha nyuma mapambano ya corona?

kunashida gani kwenye huduma hii ya maji wakati tanzania ni mafuriko nchi nzima?

kunashida gani wakati viwanda vya mabomba vipo nchini?

kunashida gani kuhusu rasilimari watu wakati watu wanahitim kila siku?

tupeni maji kimara baruti nahuu mgao usimame sasa, tumechoka kupokea sms za kusisitizwa kunawa wakati hakuna maji.
 
Tupeni maji kimara baruti leo siku ya 7 hakuna maji!
Tatizo ni nini?
 
leteni maji kimara baruti, au kwakuwa tunakaa wachanga wengi huku? Mnataka tukomeee?
tupeni maji bwana wiki nzima tunaishije sasa?
 
Je, mpaka WHO waje watoe ushauri kuwa huduma ya maji safi na salama ni ya muhimu ndiyo mamlaka za maji hapa nchini zitajuwa kuwa siyo hekima kuwakatia wananchi maji wakati huu tunaosisitiza watu wawe safi kwa kuosha mikono?

Serikali iingilie kati na kutoa amri kwa mamlaka zote kusitisha zoezi hilo la kukatia maji watu na taasisi hadi kampeni hii ya NAWA MIKONO itakapokwisha kwa gonjwa hili kudhibitiwa.
 
Back
Top Bottom