DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Lipa bili wewe..! Kipi bora , washindwe kutoa huduma kwa umma kwa sababu mmoja au wawili hawajalipa na hivyo kushindwa gharama za kusukuma maji au wakate kwa yule asiyelipa ?
 
Lipia bill zako mkuu usisingizie korona.
Mimi nikilipia wewe na ugumu wako wa kiuchumi ukashindwa kulipa hivyo ukawa hunawi mikono Mimi tunayekutana mtaani nitaponea wapi?
Wanao wachezao jirani na wangu ninayeweza kulipa tutawatengaje?
 
Lipa bili wewe..! Kipi bora , washindwe kutoa huduma kwa umma kwa sababu mmoja au wawili hawajalipa na hivyo kushindwa gharama za kusukuma maji au wakate kwa yule asiyelipa ?
Usitishaji huo ni wa muda huu mfupi wenye lengo LA kutokomeza gonjwa hili. Jambo hill haliwezi kuwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja
 
Hamna kitu. Huduma ovyo sana. Najiuliza hawa jamaa wanaokuja kwenye issues mtaani tukiripoti wana posho ya ziada au? Maana tatizo dogo tu plumbing mpk wamalize siku 3 au 4. Hapa tuna siku 8. Wanakuja wanaangalia na kuondoka. Nimepiga simu hadi nimechoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tufahamishe zaidi juu ya tatizo lako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani DAWASA nauliza hapa kwetu maji yanapita jirani kabisaa, kama mita 30 ndo kuna bomba na lina maji, nifanyeje ili niweze kuunganishiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani DAWASA nauliza hapa kwetu maji yanapita jirani kabisaa, kama mita 30 ndo kuna bomba na lina maji, nifanyeje ili niweze kuunganishiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Fika ofisi ya dawasa iliyo karibu ukiwa na. Koi ya kitambulisho chako cha ama kura, Nida. Passport size mbili, barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa na barua ya kuomba huduma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawasiliano rasmi ya simu katika Mikoa ya kihuduma Dawasa . Wasiliana nasi kupitia mfumo rasmi wa mawasiliano huu ili uweze kuhudumiwa kwa uhakika zaidi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna maeneo kadhaa Dsm hayana mfumo wa majitaka lakini hutozwa gharama za majitaka. Huu ni wizi wa wazi kabisa.
 
Inakuwaje kipindi hiki mvua zinanyesha,maji ni mengi kwenye vyanzo.watu kinyerezi tunapata maji kwa mgao wa siku 3 kwa wiki.hivi na janga hili bado dawasco mko nyuma kiasi hiki.ni aibu sana kwa kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HIVI KWELI PAMOJA NA JANGA HILI LA CORONA MNAPITA MNAKATA MAJI MAJUMBANI???MNATEGEMEA NINI???
nchi zingine umeme maji bure kipindi hiki cha maradhi ya corona.
Hili litaiondoa ccm madarakani
 

DAWASA TUNAOMBA KUFAHAMISHWA KIMARA BONYOKWA TUMERUDI KWENYE MGAO WA MAJI ?MAANA MLIJIGAMBA HAKUNA TENA SHIDA YA MAJI KIMARA TUMEKUWA NA KUKATIKA KATIKA KWA MAJI WIKI YA TATU SASA NA HIVI NINAVYOANDIKA TANGU JUMAMOSI HATUNA MAJI SASA SIJUI KUNA SHIDA GANI NA HATUTANGAZIWI, MUWE MNATOA TAARIFA BASI TUJUE KAMA NI MGAO AU KUNA HITILAFU MAHALI TUJUE.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…