Nawapongeza Dawasco kwa kazi kubwa , kuna mabadiliko ktk utendaji ila kuna mambo ya kuboresha mengi kadiri ya maoni mbalimbali ya wadau .
Mimi langu ni kuhusu bills za maji . Inavyoelekea wasoma mita hawazungukii wateja wote kusoma mita ; matokeo yake sasa :-
1 . Units zinazokuja kutumwa ni nyingi kuliko zilizo ktk mita .
Madhara yake ni mateso ya kisaikolojia kwa mteja na mteja ana uwezo akiamua kuwashitaki kwa usumbufu .
2 . Mteja anaweza kukatiwa maji kwa ankara isiyo halisi na kumletea usumbufu.
3 . Inampotezea muda mteja kuja ofisini kwenu kuripoti kosa lilelile lisilofanyiwa kazi na linalojirudia.
Mara kadhaa nimefika ofisini kwenu kuripoti huu usumbufu bila mafanikio na mwezi huu mmerudia kosa lile lile . Kama hamtajirekebisha nitajiaandaa kuchukua hatua za kisheria na nitahakikisha haki inapatikana hata kama itachukua muda mrefu . Najua wenye kesi kama yangu ni wengi na hao nd'o watakuwa mashahidi muhimu mahakamani