DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

DAWASA Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na ushauri

Nashauri Maji msisubiri atokee mwarabu achukue hii idea. Maji taka tengenezeni system watu wasichimbe mashimo ya vyoo, ninyi Muwe na main system maeneo maeneo mkusanye Kodi ya huduma maji taka tu kila mwezi...watu tumechoka kuishi na Vinyesi nyumban...hamjifunzi kwa wenzetu! Khaa!!



"Vyoo vyote viunganishwe na mfumo wa maji taka. Kusiwe na mambo ya kuchimba shimo la choo. Wewe ukijenga nyumba yako utawaita watu wa maji taka ili waje wakupe ramani ya kuunganisha choo chako na mfumo au bomba la maji taka"(konda msafi,2021)
Hl wazo n nzuri ila wasikurupuke mana hua naona wakat wa kutengeneza barabara jins mabomba yanavokatwa ovyo ovyo na maji kumwagika najiuliza je vp yangekua ndo mabomba ya majitaka?[emoji12]
 
Dawasco Kimara naona ni mwezi wa pili sasa mara nyingi inapofika weekend siku hasa za ijumaa na jmosi mnakata maji.

Yaani watu wapo nyumbani weekend kifamilia matumizi ya maji ni makubwa nyinyi mnaona ndio wakati muafaka wa kuwanyima watu maji?
 
Kweli nawakubali kwakutojali wateja wenu mnaongoza mnajua tuu kudai bili. Siku ya 3 leo tabata changombe hakuna maji na hakuna maelezo ili tujipange
 
Za jumapili wadau wote wa jf.
Nimekuwa nikipata kero sana kila ikifika mwsho wa mwez ni lazima hawa jamaa wakate maji siku tatu mpaka nne.

Nimekaa nikatafakari nimekuja kujua hawa jamaa wanatumia hii njia kama mbinu mbadala ya kushinikiza watu walipe maji kwa wakati bila kufikiri kuna watu kulipa bills zao mapema ni wajibu wao kwa vile hawataki kabisa hizi shida za namna hii.

Manager dawasco upande wa kimara tafuta njia mbadala ya kudeal na wasumbufu wa kulipa ila sio hii bhana karne ya sasa matumiz ya maji ni kila mahali chooni, jikoni na kadharika ukiyakata kwa siku tatu mnataka watu wafanyaje alafu wamelipia hayo maji?

Nawasilisha
 
Tabata mwananchi Kuna tatizo gani mbona maji hamna Toka juzi, watu tunateseka, kwanini mnatufanyia hivi?
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu yaliyo Jijini Dar es salaam , miji ya Kibaha na Bagamoyo Mkoani pwani. DAWASCO inapokea maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Ndugu wana jukwaa, DAWASCO inajipambanua kwa kusimamia maadili ,kutoa huduma iliyotukuka pamoja na kuhakikisha huduma ya Maji inapatikana kwa kila mwananchi.

Kama kutatokea kuharibika kwa bomba, wizi wa Maji, umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: DAWASCO - Welcome to new site
2. Kupitia mitandao yetu ya kijamii ikiwa ni pamoja na Twitter|DawascoOfficial..Facebook|DawascoOfficial ...Instagram|DawascoOfficial
3. Kwa mwananchiposta ; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu
DAWASCO
P. O. Box 5340
Sokoine Drive
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu huduma kwa wateja dawasco
0800110064 /022 2164800 ( Kupiga namba hizi ni Bure)

DAWASCO HUDUMA KWA WATEJA 0800110064
DAWASCO ILALA 0743 451879
DAWASCO KAWE 0743 451861
DAWASCO KIBAHA 0743 451875
DAWASCO KIMARA 0743 451865
DAWASCO KINONDONI 0743 451863
DAWASCO BAGAMOYO 0743 451877
DAWASCO MAGOMENI 0743 451862
DAWASCO TEGETA 0743 451881
DAWASCO TABATA 0743 451867
DAWASCO TEMEKE 0743 451866

Yaaani mnachekesha Sana....mnapitisha mabomba kwa kuangalia sura!?¿?
 
Bomba lime pasuka Tabata bangulo na huwa lina pasuka mara kwamara cjui tatzo nn watu wa Dawasa
 
DAWASA naomba kujua taratibu za kufungiwa maji pale ambapo mnaishi kwenye eneo moja ila lina nyumba za kujitegemea.

Tatizo la hapo ni kuwa hakuna maji. Yani hakuna bomba kwa sababu wapangaji hawataki kushea bomba moja.

Mita iko moja na ni ya mwenye nyumba hizo na anaitumia yeye binafsi. Kila mpangaji anataka kuwa na mita yake ya maji kitendo ambaco DAWASA wamesema hakiwezekani. Sasa mimi nataka bomba langu, nafanyaje?
 
Kwenu nyie wahusika wa dawasa,nimeisha toa malalamiko yangu kwenu kupitia huduma Kwa wateja,lakini utatuzi wake bado kabisa.

Tatizo langu kubwa ni kuhusu mita yangu ya maji hapa nyumbani kwangu,mita hii ukiiangalia ina ukungu na hii hupelekea usomaji wake kuwa mgumu, na hata hii imepelekea bili ya miezi miwili yaani mwezi July na august kuwa kubwa kupita kiasi.

Nashindwa kuelewa kwani hata ukienda kuangalia mita yenyewe ukitaka kusoma namba hazionekani, NAWEZA KUSEMA HUU NI UBABAISHAJI WA HALI YA JUU KWA HUYU MSOMA MITA KWANI INAWEZEKANA ANAKADIRIA KADIRIA TU NA SIO UHALISIA WA MITA YENYEWE.
 
Dawasa iendane na mabadiliko.
Mimi ni mteja mwenye account namba 90024389 iliopo mtoni mtongani kata ya kunduchi, Nina tatizo na wasoma meter wa eneo hilo ambao weledi wa kazi yao unanitia shaka na niwashauri wakuu wa taasisi wawe wanawapeleka kwenye mafunzo ya 'huduma kwa wateja' kwa watumishi wao, sio uungwana kuona kuwa mwenendo wa malipo ya mteja kila mwezi kwa wastani huwa hayazidi elfu 40.

Halafu ghafla mita inasoma matumizi makubwa yanayokadiria kufika laki mbili halafu mhudumu wa dawasco anakuja kufanya mawasiliano na wewe siku ya kukata maji, na wala hazungumzii ongezeko la ghafla la matumizi limesababishwa na nn, kibaya zaidi ni kitendo cha kukata maji bila maelezo yoyote na unapotaka kujua sababu unalazimishwa kuja ofisini, sasa huko ofisini kwenu mji mzima tukija itakuaje? hivi hamuwezi kuwa na Tija mpaka mtu aje ofisini?

Naomba mbadilike kwenye huduma kwa mteja, na si busara kumkatia mtu maji wakati haja wacha kufanya malipo kila mwezo, huku sio kuisaidia serikali Bali ni kupoteza mapato ya serikali, niseme tu kuwa hali hii isipobadilika nita lodge complaints na Regulator.
 
Jana nimelipa Bill ya maji 14,000 nimekatwa 2200 imekaaje hii?
 
Hivi bei ya maji imeongezeka? Mbona mwezi huu bill imekuwa kubwa sana, nimejaribu kuuliza na majirani zangu nao wanashangaa...mmepandisha kimya kimya au kuna taarifa rasmi
 
DAWASA ,Jirani yangu hana bomba je ni kosa mimi kumsaidia maji?
Mmoja wa maajenti wenu huku Manzese anatishia kunikatia huduma akidai ni kosa.
Nahisi anajenga mazingira ya kupewa rushwa
 
Watu hawataki kawajibu wateja, nawachukia sana.

Bomba linatakiwa liwekwe. Mteja anaingiwallzwa
 
jamani hii pressure ya maji toka jana ni kali sana, mtatupasulia mabomba
 
meter number 00582001 tangu walipobadilisha mita tarehe 19 mwezi wa nane, inavuja maji kidogo kidogo hapo kwenye mita, na leo yameongezeka zaidi.
 
Habari dawasa Kuna bomba limepasuka
eneo la Sinza D MAGOLI MATATU (Uwanja wa mpira) naona tatizo hili limekuwa sugu kiasi kupelekea kupotea kwa maji mengi ambao yanaingizia hasara mamlaka
ushauri : bomba linakatiza barabara kwahiyo joint zihamishwe kwa maana ya kwamba ipelekwe kwenye position ambazo gari hazipiti.
 
Dawasa huduma kwa wateja 0800110064 aliyekuwa zamu leo kuanzia asubuhi mpaka sasa hajui nini maana ya customer care, nimepiga simu kuripoti kukosekana kwa maji maeneo ya kwetu kwa wiki nzima akachukua namba yangu na pia wakanitumia reference number kwa ajili ya ufatiliaji, nimekaa masaa matano sijapigiwa kupewa nini tatizo,nikapiga simu call center nikawapa reference number ,dada alikuwepo akaniambia nieleze tena tatizo lilikuwa ni nini?

Nikamwambia kwanini nieleze tatizo tena wakati kuna reference namba? Naomba nikutajie referenve ili unipe update tatizo ni nini na mmefikia wapi?

Kabla hata ajajibu nikatumiwa ticket namba nyingine tena ya wilaya tofauti niliyokuwepo mimi,nikahoji ina maana week nzima mtaani kwetu hakuna maji ni mimi tu ndiye niliyereport mpaka msijue tatizo ni nni?

Dada akakata simu, kiukweli huduma kwa wateja hasa za umma ni shida, yaani waliyokuwepo hawajui hata wanafanya nini.
 
Back
Top Bottom