Afrika ni bara lenye wasomi wengi wapumbavu sana .
Wasomi walevi TU wanaokesha kwenye mabaa .
Wasomi makahaba na Wazinzi wanapokutana kwenye semina na makongamano wanawaza ulevi na uzinzi.
Wasomi wanaowaza Madili na mbinu za kufuja fedha za umma.
Wasomi wasiowaza kuondoa matatizo yaliyoko kwenye jamii Bali kuyatumia kama Fursa ya Kupiga pesa za umma.
Hivi pale Ruvu ni sehemu kweli ya kukosa maji ya kuwapeleka wananchi maji.?Nini MAANA ya Teknolojia kama Bado tutatumia mbinu na mitambo Ile Ile ya mkoloni kuvuna Maji na kuyatibu Kisha kuwapelekea wananchi. Mitambo tangu enzi ya Mwalimu mpaka Leo kiwango ni kile kile.
Ukipitia Bagamoyo maji yanatokea Ruvu Kwa mamilioni ya Lita yanakwenda kumwagikia baharini halafu kilomita Kama 30 nyuma unaambiwa hakuna maji ya kupeleka kwenye mitambo.
Hayo maji mnayaacha yaende baharini kufanya Nini wakati Kuna ukame au mnaogopa bahati itakauka?
Hivi hata kuyazuia yote yaende kiwandani nayo ni mpaka aje mchina?
Ok ,basi wakabidhini wachina hiyo miradi ya maji na umeme kama Kuna tone la maji litapotea.
Hivi mnataka Mungu au mzungu aje Tena Afrika kuondoa changamoto zetu .?Miaka 60 ya uhuru Bado tuna viongozi wanaodanganywa wakadanganyika.
Ukifika kwenye Afya ni hivyo hivyo mamilioni ya dawa zinaishia kwenye magospitali na maduka binafsi ya dawa . Hospitalini hakuna lakini kila mwaka bajeti ya Afya inaongezeka. Inaongezeka kwenye nini wakati Matibabu Sasa yamekua ni biashara. ? Kwa Nini huduma ni duni sana Kwa umma lakini binafsi wezi wananufaika Kwa bajeti ya Kodi za wanyonge na rasilimali za umma?
Ukienda kwenye Shirika la nyumba na Wizara yake ni hovyo kabisa . Wananchi wanahaha na kuwa watumwa wa kupanga nyumba zisizo na ubora Wala miundo mbinu mizuri Kwa Kodi kubwa inayoongezeka bila udhibiti ! Kwa ujuha mkubwa wabunge na serikali wanawaza kuchukua Kodi Kwa wapangaji Tena badala ya kudhibiti soko holela la nyumba Kwa kujenga nyumba Kwa ajili ya watu wa Chini, SIO majumba ya Mawaziri,makatibu, wabunge , mabalozi, Wakurugenzi,majaji n.k. watu Wenye vipato vikubwa Lakini eti Mchechu ndio anakimbilia Tenda za serikali kujenga majumba ya Serikali . Kodi wanazochukukua Kwa wahindi Kule mijini zinaishia mifumoni Kwao. Watanzania Hawana nyumba za kupanga Kwa Bei nafuu lakini wahindi wanapanga Kwa Bei Sawa na Bure.
Wanasema Kila MTU apambane ajenge nyumba. Watu Wa ajabu sana. Watu mil. 61 na moja wakiachwa kujenga na Kila mmoja amiliki kijumba chake hiyo misitu itatoka wapi . Hiyo hifadhi itakua wapi? Open space zitakuwa wapi? Mashamba yatakua wapi? Kila Mahali patakua ni makazi. Dunia yenye Maendeleo ya uhakika ni Lazima pawe na makazi Bora . Ujenzi uwe planed Kwa kujenga maghorofa Ili makazi yasitanuke sana na kumaliza Matumizi mengine ya Ardhi.
Ukienda kwenye Elimu ni hivyo hivyo . Shule binafsi ni za wale wale na hazina chombo Cha kudhibiti na kuangalia huduma na ubora wake kulingana na ongezeko la ada na michango kila muhula.
Falme za Kiarabu ni watu kama sisi tofauti ni kuamua kwao kuwatumikia wananchi maskini.
Waarabu hao wanaotokana na Koo za kifalme wamejitolea kuondoa kabisa Changamoto zinazowagusa watu wa chini kwenye mahitaji ya msingi ya binadamu.
Serikali kazi yake ndio hiyo bila kuangalia Mambo ya kisiasa tuu na utawala tuu. Ndio maana ya Mungu kuumba watu na kuwapa akili na rasilimali za asili. Zitumike kuhakikisha watu wanapata chakula na maji, nguo na makazi Bora.
Hivi Kwa maisha ya Kitanzania Janyuali na Lizi one ni watu wanaowaza njaa ya kuwaibia au kuiba Mali za umma na kukwepa Kodi. ?
Hivi Hawana hata chembe ya huruma ya kuwaza kuondoa kabisa Changamoto zinazogusa Mahitaji ya msingi ya binadamu.?
Kila idara ni uovu mtupu. Serikali ipo imewaachia wezi wakwapue kila wanachokiona mbele ya kamba zao . Na wengine Sasa hawana hata kamba Wanakwenda kula kulingana na wanachokiona mbele yao.
Shame on you wasomi mlioumbuliwa na Wavuvi Darasa la Saba Kule Bukoba , kuwa uzalendo sio vyeti na majengo na viyoyozi na Magari makubwa ya anasa Bali ni Moyo na utayari Wa kuwapigania wananchi.
Hata Nigeria Kwa muda mrefu wanajeshi walisumbuliwa sana na Boko HARAMU Kwa Sababu walijichanganya kuwa jeshi linahitaji wasomi Pekee. KUMBE wasomi hawapo tayari kufa na kuacha starehe zao za kimtandao .
Wasomi na Wanasiasa wasipodhibitiwa wanageuka kuwa wezi na waiga dili tu nawajanja Wajanja maana wengi ni marafiki waliosoma pamoja na kuishi pamoja.
Leo Kila Mahali ni makongamano tu na semina . Sasa hiyo hela ya semina Kwa nini isiende kwenye ahicho kinachojadiliwa moja Kwa Moja.
Watu hawataki Katiba mpya Lakini Mapesa lukuki yanakwenda kujadili eti iwepo Katiba mpya Lini ? Wanajua ni Lazima ije Sasa si Bora tu kusema pesa ziende kwenye Maendeleo basi na SIO kutumia pesa nyingi kuahirisha Jambo ambalo lingewezeka kuahirishwa Kwa tamko moja tu basi.
Ni Lazima watokee Viongozi wasio na masihara Wala mitandao na urafiki . Viongozi wasiovumilia uhalifu Hata kama ni Ndugu .
Tumuombe Mungu atuondolee viongozi wasio na maono mema Kwa Taifa hili.