DAWASCO Kimara fungueni Maji, Hali ni Mbaya

DAWASCO Kimara fungueni Maji, Hali ni Mbaya

Mlishindwa kukinga maji ya mvua? wale ambao hawajawahi kuunganishiwa maji na wananunua maji kila siku wasemeje? vipi wale wanaochangia maji na mifugo hasa maeneo ya vijijini nao wasemeje?
 
Habari wanabodi, kama Kuna mtu anamfaham Meneja wa DAWASCO Kimara, tafadhali amjulishe kuwa afungue maji mchana huu kwani Hali huku mtaani ni Mbaya Sana. Siku ya 4 leo inaenda maji hakuna, na hata watu wanaouza toka kwenye matanki yao wameishiwa maji, hivyo, Hali sio ya mchezo kabisa.

Kuna Ndugu yangu anaishi hapa Nyuma ya Ukuta Wa Dawasco Kimara, anasema yaani Mtaa Mzima hakuna mwenye akiba ya Maji ndani. Watu wameshindwa kufua wikend hii kisa hakuna maji.

Kama huu ni uzembe wa Mtu fulani nashauri Waziri wa Maji amtumbue mapema Ili wezembe wengine wajifunze pia. Hali zipoje maeneo mengine Dar leo kuhusu maji.
Leo nimepita maeneo mengi maeneo ya Manispaa ya Temeke na Ilala kiukweli huko tatizo la maji halipo maana watu wenye visima binafsi ni wengi na wamechukua nafasi ya DAWASCO maana hawaonekani kuwaza maji kabisa.
 
Nini sababu ya tatizo la baadhi ya wakazi hasa wa Dar es Salaam hasa Ubungo kukosa maji kwa wiki mbili mfululizo. Hakuna maelezo na wewe Mkuu wa mkoa umetulia tu kwenye AC hata kuwatingisha hao DAWASCO huwezi mbona mtangulizi wako Makonda alikuwa angalau alikuwa anakemea
 
Back
Top Bottom