Daz Baba haki yako iliyodhulumiwa na Bongo Records italipwa hapa hapa duniani

sinza pazuri

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
3,344
Reaction score
9,066
20220719_145139.jpg

Msanii wa Bongo Records aitwae Daz Baba ambae alitoa nyimbo kali kama Nipe tano, umbo namba 8, wife nk.

Alituletea album classic ya Elimu Dunia kinachosikitisha ni kwamba hajawai kufaidika na mauzo ya album yake hela za mauzo anachukua P Funk Majani ambae alitengeneza mikataba ya ujanja ujanja hivyo maisha yote atakuwa anamiliki kazi za Daz Baba.

Pamoja na ngumi pamoja na mitama mliyokuwa mnapigwa ila hela anachukua Majani mpaka leo na milele.

Tuendelee kumuombea Daz Baba malipo yake Mungu ataingilia kati siku moja.
 
Majani kakanyaga pabaya, muda umefika kwa yeye kuachia kazi za wasanii nao wafaidike na kazi zao.

Yani maramia hao wasanii wa WCB wananyonywa huku wakiwezeshwa, hivyo hata wanavyotoka utumwani wanakuwa na uwezo wa kununua haki miliki zao.

Wasanii waliopokwa haki zao na Majani, hawakufanyiwa uwekezaji wowote, ndio maana wengi wao leo wapo choka mbaya.
 
View attachment 2296599

Sa hivi kawa mlevi balaa hadi kwenye interview anaenda amelewa halafu ivi hakuna wasimamizi wa izi media houses maana wamezidi badala ya kuwasaidia watu wao wanaangalia contents tu, clouds walishamfanyisha interview marehemu Godzilla akiwa amelewa na kwenye interview wakina mchomvu wakawa mdhihaki na kumkejeli na full kumenjoy badala ya ya kumpeleka ata rehab aka sober houses , GLOBAL TV niliona interview moja wamemfanyia daz baba akiwa amelewa kisenge😀😀siku tutaamka na kusikia daz kadanja kisha tunaanza kujiliza na kumsifia
 
Hivi Daz kakosa kabisa mtu wa kumsaidia au ni namna gani. Maana ni muda sasa naskiaga tu jamaa anakula dawa ila sijawai kuskia mtu kajitokeza kumsaidia. Au labda wapo ni mimi ndio sijawai tu kuskia
 
Nilimwona mara mbili Kkoo na maeneo ya Tabata daah anatia huruma,ila yote kwa yote Bongo records imetoa mateja wengi kwani na kumbuka hata Majani alishawahi kukiri ktk kipindi cha mikasi alikuwa anatumia madawa, ila alifanikiwa kuacha baada ya kwenda sober house. Sasa sijui nani alikuwa anawafundisha wenzake.
 
leo alikuwa na interview mchana na tbc kiukweli jamaa limebaki jina tu, mwisho wa siku ametaja namba zake hadharani tena amesisitiza ndio anatumia whatsp
 
Majani kakanyaga pabaya, muda umefika kwa yeye kuachia kazi za wasanii nao wafaidike na kazi zao.

Yani maramia hao wasanii wa WCB wananyonywa huku wakiwezeshwa, hivyo hata wanavyotoka utumwani wanakuwa na uwezo wa kununua haki miliki zao.

Wasanii waliopokwa haki zao na Majani, hawakufanyiwa uwekezaji wowote, ndio maana wengi wao leo wapo choka mbaya.
Huu ndiyo ukweli mchungu kwa machawa wa P Fun(Majani).
WCB nadhani ndiyo record label pekee inayowainua kimaisha regardless aina za mikataba kati yao na wasanii walio chini yao, hivi kwa nini record labels nyingine Tz wasanii wanabaki kuwa underground miaka nenda rudi? Uwekezaji na mikataba yao ikoje?
Ukiona mtu anapambania msanii mpaka anakua inafikia fans wanaanza kuwashindanisha ujue huyo anawekeza na kumuwezesha msanii wake kwa nguvu na nia dhabiti.
 
Dunia bana,tutasubiri afe ndio tuanze kumsifia na kuomboleza na michango mingi ya kusindikiza kwa amani.
Utashangaa kwanza siku io unasikia ngoma zake zinapigwa sana redioni halafu sina nyingi. Wakati alikuepo walikua wanamuangalia tu
 
Huu ndiyo ukweli mchungu kwa machawa wa P Fun(Majani).
WCB nadhani ndiyo record label pekee inayowainua kimaisha regardless aina za mikataba kati yao na wasanii walio chini yao, hivi kwa nini record labels nyingine Tz wasanii wanabaki kuwa underground miaka nenda rudi? Uwekezaji na mikataba yao ikoje?
Ukiona mtu anapambania msanii mpaka anakua inafikia fans wanaanza kuwashindanisha ujue huyo anawekeza na kumuwezesha msanii wake kwa nguvu na nia dhabiti.
Kwahiyo hawakuwahi kulipwa hata mia huko bongo reçodrs?
 
Back
Top Bottom