DC Alberto Msando akopa milioni106 benki ili kuwajengea wamachinga sehemu ya kufanyia biashara

Anatakatisha pesa zake huwajui mawakili wa Arusha wana utajiri ambao huwezi kuutolea maelezo.
 
Mimi bado sijaelewa namna miji inaendeshwa na hasa hili la wamachinga. Sasa, tatizo la wamachinga ni kuwa na eneo maalumu la kufanyia biashara? Mbona tumeona mifano kadhaa, wanajengewa na wanalitosa eneo? Baada ya hilo jengo la Msando kukamilika, atahakikishaje wamachinga wataondoka stendi hiyo ya Msamvu?

Nionavyo, bila ya ubabe wenye manufaa (wa kuzima tabia zetu za maisha holela) hatuwezi maliza hili la wamachinga. Nina hakika, hilo jengo halitofanya lolote kama halitokidhi mahitaji ya machinga na tabia ya mnunuzi wa kibongo ipo palepale. Tumlazimishe mteja aende sehemu husika kufanya manunuzi. Ukienda Kigali, mji umetuliaaaaaaaaa.

Si kwamba machinga hawapo,lakini, utakutana nae kama mwizi hivi. Yani ni kama vile bodaboda walipozuiwa kuingia mjini pale Dar. Ukimpata anaeingia downtown, basi ana maisha kama mkia wa digidigi. Huwezi amini, Kigali kuna usafiri hadi wa baiskeli (zile zimewekwa chushion), kwakuwa mji na miundombinu inaruhusu kufanya hivyo. Dawa namba moja ni ubabe wa akili na wenye manufaa, si ubabe wa kuwafanya watu kuwa masikini.

Wajengee jengo/wape eneo, kisha hakikisha wateja wanafika huko. Hapo machinga hatokuwa na shida na wewe

Angalizo
Kuhusu Kigali, nimetoa uzoefu wangu wa miaka kama mitano hivi iliyopita. Sina hakika kwa sasa kupoje, kama wameendelea na utaratibu uleule ama wamebadilisha
 
Kupata hizo hela ambazo ni kidogo sana ni aspect moja, kufikia lengo ni aspect nyingine.

Kufanya jambo ni kitu kimoja, kufanikisha ni kitu kingine. Apongezwe kwa uthubutu na tumtakie mafanikio zaidi ya kutamani aanguke
 
Ni UWONGO mkopaji lazima abakiwe na 1/3 ya mshahara wake 1/3 ya 3.1m ni 1m yeye anasema nanakwatwa 2.8 take home ni 300k wakati take home inatakiwa 1/3 ya mshahara wake 1m
 
Mkuu wa wilaya ya Morogoro amekopa milioni 106 eti za kuwajengea maeneo wamachinga kufanya biashara.Haya ni makosa makubwa.Je anajua wamachinga wapo wangapi?Soko la kisasa la Kingalu lina nafasi ya kutosha?Kubwa zaidi kiongozi huyu kakiuka utaratibu wa kiongozi serikalini kukopa benki.Ameweka dhamana gani?Ukuu wa wilaya wake moja kwa moja unamtia mashakani kwani kama kiongozi wa umma tena mteule wa Mh Rais benki gani itakataa kumkopesha?Je hakuna Halmashauri ya Manispaa?Tunamwomba waziri wa Tamisemi aingilie kati la sivyo wasiopata hicho alichokitaka huyo mkuu wa wilaya kitamrudia MWENYEWE.MKUU WA MKOA UPO WAPI?Huyu mkuu wa wilaya ameshatibua tibua kila sehemu.Nashangazwa sana na mambo yanavyoenda siku hizi.Ina maana mkuu wa wilaya ya Ilala akakope kiasi gani?Wa Ilemela naye kiasi gani?Mama Ummy zuia mara moja utaratibu huu.Watakopa mabilioni mwishowe Matozo yatatuangukia waliokuwemo na wasiokuwemo ili kulipa,maana benki hazina huruma.
 
ni UWONGO mkopaji lazima abakiwe na 1/3 ya mshahara wake 1/3 ya 3.1m ni 1m yeye anasema nanakwatwa 2.8 take home ni 300k wakati take home inatakiwa 1/3 ya mshahara wake 1m
Simple calculation.

Mkopo wa Unsecured wanaochukua unatakiwa kukatwa 2/3 na yeye anatakiwa kubaki na 1 third..
 
Lakini kaonesha concern yake!

Kama dhamira yake njema Mungu amlinde maana ametoa sehemu ya utajiri wake kwa ajili ya wengine.
 
Kila mtu ana huo ujuzi ila wa kushika lichupi tofauti ni kwamba yeye alishika la Gigi Money wakati wewe unashika la chausiku

Halafu haya mambo si yalishapita swahiba!? Acha kazi iendelee
Yalishaisha....

Sema tu lile chupia Gigi Money lilitisha.... sijui alilishonea wapi wallah
 
Ni UWONGO mkopaji lazima abakiwe na 1/3 ya mshahara wake 1/3 ya 3.1m ni 1m yeye anasema nanakwatwa 2.8 take home ni 300k wakati take home inatakiwa 1/3 ya mshahara wake 1m
Hawezi sema mshahara wa DC kwenye kadamnasi.
Yeye ametaja kiasi anachochukuwa baada ya kukatwa kodi.
Chunguza vizuri ujue DC anachukua kiasi gani ndiyo uje hapa. Wapo above 4.5M kwa mwezi

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Hawezi sema mshahara wa DC kwenye kadamnasi.
Yeye ametaja kiasi anachochukuwa baada ya kukatwa kodi.
Chunguza vizuri ujue DC anachukua kiasi gani ndiyo uje hapa. Wapo above 4.5M kwa mwezi

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
labda kama wamekutoa sehemu ulikua unalipwa 4.5m hawezi kukushusha ila kada tu wa ccm kawaida 3m inakuhusu
 
Yawezekana ana nia njema lakini sijuhi kwanini n I have lots of questions!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…