Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basilla Mwanukuzi ameandika waraka mzito kuhusu utendaji dhaifu wa watumishi wa Halmashauri ambao wanahujumu miradi huku wakiendelea kukingiwa kifua na mamlaka husika.
Na basillamwanukuzi
Hongera sana @dndejembi kwa kuamniniwa na Rais kua Naibu Waziri TAMISEMI ninakupongeze sana ndugu nikuombe utusaidie kama Watanzania hasa kwenye miradi ya maendeleo nchi nzima umsaidie Mhe Rais @Samia_suluhu_hassan na Serikali ya awamu ya 6 inayo elekeza mabillion ya fedha kwenye miradi ya maendeleo kwa ajili ya Watanzania kwenye miundombinu ya Afya , Elimu, Maji, barabara ,miradi ya kimkakati kwa ajili ya mapato ya Halmashauri etc lakini mambo hayaendi kama ilivyopangwa
Hali ni TETE , hali ni MBAYA wananchi wamekata tamaa. Wananchi wanateseka Fedha zinakuja kwa wingi kutoka Serikali kuu zikifika halmashauri fedha hazimalizi miradi , na fedha zingine zinakuja zinakaa tu kwenye account miradi haianzi , nikuombe katika ziara zako za mwanzo anza na KOROGWE
HALI NI MBAYAAAA . Na hakuna mwenye ujasiri wa kusema au kuchukua hatua
Wewe ni kijana mchapakazi na bahati nzuri umeshawahi kua DC .
Korogwe is a special case iko ICU kwenye swala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo ukiacha madarasa. Niko tayari kukupa ushirikiano kumsaidia Rais wangu, Chama Changu na Taifa langu na zaidi wananchi wanaodhulumiwa haki yao inayotekelezwa kwa uaminifu na Serikali yao inayoongozwa na mama mwenye kufahamu 'uchungu wa mwana' na ndio sababu anaelekeza fedha hizi zikasaidie wananchi.
Matokeo yake hakuna manufaa kwa sababu fedha zinaisha , miradi haiishi Wananchi hawapati huduma.
Ni bora kua na mradi mmoja ukaisha kuliko kua na miradi kumi ambayo hakuna hata mmoja umeisha. Miongozo ya TAMISEMI haifuatwi, Maelekezo hayafuatwi mamlaka husika hazichukui hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.
TUNAKWENDA WAPI???🇹🇿
HAIKUBALIKI DUNIANI WALA MBINGUNI
#MbelekoYaBasilla #kiongoziWaWananchi #sautiYaWatu #MzalendoDamu
Edited · 3dSee translation